Bomu la kivita lililomwua Daud? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomu la kivita lililomwua Daud?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Sep 10, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tunataka tume huru na uwajibishwaji wa wote wanaohusika kwa njia yoyote!
   
 3. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni bomu la kivita au la machozi? Maana kama ni bomu la kivita lingeua watu wengi. Na bomu la kivita haliwezi kufyatuliwa na mtambo wa kipolisi unaotumika kufyatulia mabomu ya machozi.
   
 4. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 646
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hata lingekuwa la kivita, la machozi, la michezo, bomu ni bomu tu tunalaani mtindo huu wa Polisi kuua raia kwa mgongo wa kodi zetu!!!
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Naona ni bomu la machozi na si la kivita mkuu kama unavyomweleza mleta mada. La kivita hata wale polis pale wote wangekuwa vumbi tena na kuzikwa mta nyingi chini ya ardhi. Ni la machozi lililolipuliwa bila kuzingatia taratibu zake.
   
 6. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Aisee kweli hapa polisi wana kesi ya kujibu.

  Halafu mabomu ya kivita yapo ya aina mbalimbali na pia inategemea yamefyatuliwa na mtutu wenye ukubwa wa kiasi gani(launcher) au pia hand grenade ambayo kwa mkasa huu halikuhusika

  Kuna bomu la kivita linaloweza kufyatuliwa na zile bunduki zinazoonekana kwenye picha ya wauaji wa Daudi Mwangosi. Mfano wa bomu la kivita linaloweza kulipuliwa na bunduki ya aina ile ni 40mm caliber low velocity high explosive airburst grenade

  Sasa kama wewe unategemea bomu la kivita la 40mm liporomoshe ghorofa basi utakuwa uko sawa.

  Cha msingi hilo ni bomu la kivita. Kwamba limefanya madhara kiasi gani inategemeana namazingira
   
 7. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Asante sana kwa elimu hiyo mkuu.sijaelewa polisi wanahujumu ccm au CDM?kama wanahujumu CDM wahesabu wameumia maana CDM ni sawa na moto wa petroli.ukifuata unalipuka.CCM NA CUF WATAGAWANA KURA.CDM KIDEDEA.
   
 8. k

  kwitega Senior Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bomu lililotumika linaitwa la kishindo ambalo Polisi hawaruhusiwi kulitumia. Haijulikani kulikuwa na mantiki gani ya kutumia bomu hilo. Nani aliidhinisha bomu hilo litoke kwenye ghala la silaha na kwa sababu gani? Hakika hapo inaingia kabisa akilini kuwa mauaji hayo yalipangwa; kwamba kwa risasi moja angeweza kukoswa koswa akapona, dawa ni kutumia bomu hilo ili kumsambaratisha kabisa. Unyama, ushenzi na ukatili wa kishetani.
   
 9. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Tusubiri kamati ya Nchimbi kutufafanulia ni bomu la aina gani?
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mabomu yapo ya aina na viwango mbalimbali. Risasi ya kawaida ukaribu ule lingepitiliza na lisingeweza kuleta madhara makubwa ya kuvumua mwili wote kwa kiwango kile.

  Bomu la machozi haliwezi kuwa na madhara ya kutisha kama yale kwa vile limeandaliwa sio kwa kudhuru ila kuchafua hewa.

  Pamoja na kwamba sina ujuzi na silaha, nilijaribu kumwonyesha mzungu mmoja mzoefu na mambo ya vita aliniambia
  1. hilo ni bomu la masafa ya wastani vitani,
  2. kama lingelenga umbali kuanzia 15 mita wengi pale katika kundi la askari na marehemu wangekufa,
  3. Katika tukio lile mlengaji alitumia mlengo wa karibu zaidi kuepusha madhara kwa wengine, ni mpango ulioandaliwa.
  4. Aliniuliza kama yule askari aliyeshikwa kiunoni na marehemu kama hakupata majeraha, nikamwambia anaugulia hospitalini, akasema kwa kiwango kile cha upigaji lazima yule askari angeadhirika tu.
  5. Pili amesema yule askari aliyevaa kiraia iwapo bomu lingemlenga kichani marehemu basi naye angekuwa victim.

  Huyo mzungu ni mwanajeshi na amesema bunbduki ile iliyotumika ni rasmi kwa mabomu.
  Mabomu yanaweza kuwa ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na
  • Yasiyo na madhara kwa kuharibu mwili wa binadamu ila kuchafua hewa kwa moshi na madawa ili watu wakimbie, kama ni kwa karibu basi michubuko na kugeguka viungo lakini si kwa kiwango cha uharibufu kiasi kile
  • Mabomu ya ukubwa ule ule lakini ni ya moto ambayo madhara yake kwa karibu ni kufumua kabisa mwili wote kama ilivyotokea kwa marehemu.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Jamaa alivyoniambia bomu lisilo na madhara makubwa ambalo ni la machozi huwa halina kishindo kikubwa. alitoa maelezo mengi, kwa wenye uzoefu wa matumizi ya silaha za kivita wangemwelewa vizuri zaidi.
   
 12. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mi nashangaa hili Bomu waliomzunguka wali survive vipi ? Ni Bomu la aina yake kama sio la Machozi.

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu wangu. Maana wengne mambo ya silaha hatujui, kwanza naziogopa sana. Ufafanuzi huu utasaidia wengi.
   
 14. Monyiaichi

  Monyiaichi JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 1,825
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ina maana kulikuwa na mpango wa kushughulikia watu fulani, hasira zikaishia kwa Mwangosi? ila kuna watu wana mioyo tofauti na ya wanadamu wenzao, amini usiamini, ukiambia shika silaha na adui yako mkubwa huyu hapa muue, bado sio rahisi sembuse mtu hajakukosea unatoa uhai wake kwa kisingizio cha uaskari-nafikiri na kuchanganyikiwa nako kumo.
   
Loading...