Bomu la Arusha-Ni Victor Ambrose pekee, wengine wote waachiwa

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
1,334
Reaction score
1,466
Polisi wamewaachia wote waliokamatwa kuhusika na kulipuwa waumini wa kanisa katoliki Arusha na kubakiwa na mmoja Victor Ambrose ambaye sasa anatuhumiwa na kushtakiwa kwa kupanga njama, kupata bomu, kurusha bomu na kuuwa na kujeruhi. Kijana mwenye miaka 20 ambaye elimu yake darasa la saba, mwendesha bodaboda ameweza kujipatia bomu la kutengenezwa kiwandani, kujua kulitumia bila mafunzo, kulirusha na kuuwa. Je alikuwa ana motives gani? Kwanini? Alinunua au alipata bomu wapi? Nani alimletea Arusha au alilipata Arusha?

Je Victor alikwenda na nani kanisani? nani alikuwa abiria na yuko wapi? Kwanini polisi hawataki kugusia kuhusu abiria wa Victor?
sabas-may10-2013%282%29%283%29.jpg

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewaachia kwa dhamana watuhumiwa wanaodaiwa kurusha bomu kwa waumini waliokuwa wamekusanyika kuanza ibada ya uzinduzi wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Mei 5, mwaka huu, jijini Arusha.

Hata hivyo, watuhumiwa hao wamepewa sharti la kuripoti polisi, pindi watakapohitajika kufanya hivyo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema wamelazimika kuwaachia kwa dhamana kwa kuwa sheria haiwaruhusu kuendelea kuwaweka mahabusu kwa muda mrefu bila kuwafikisha mahakamani.

Hata hivyo, alisema wakiwa nje kwa dhamana, jeshi lake litaendelea na upelelezi na kuwahoji kila litakapokuwa likihitaji kufanya hivyo.

“Tumeamua kuwaachia sababu sheria haituruhusu kuendelea kuwashikilia muda mrefu na lengo letu hasa katika hili tukio hatutaki kumwonea mtu yeyote, ndiyo sababu tunafanya uchunguzi wa kina,” alisema.

Alisema hadi sasa hakuna ongezeko la mtu mwingine aliyefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo zaidi ya Victor Ambrose Kalist (20).

Victor alifikishwa mahakamani Mei 13 mwaka huu, mbele ya Kaimu Hakimu Mwandamizi Mkazi wa Arusha, Devotha Kamuzora, kujibu mashtaka mawili ya kuua na kujaribu kuua na kesi yake itatajwa tena Mei 27, mwaka huu.

Watuhumiwa walioachiwa kwa dhamana ni Jassin Mbarak (29) mkazi wa Bondeni Arusha, Joseph Lomayani (18)

dereva wa pikipiki na mkazi wa Kwa Mrombo Arusha, George Batholomeo Silayo (23) mfanyabishara mkazi wa Olasiti na Mohamed Suleiman Said (38) mkazi wa Ilala Dar es Salaam.

Mei 13 mwaka huu, Kamanda Sabas, alisema watuhumiwa watatu raia wa UAE ambao ni Abdul Aziz Mubarak (30) mfanyakazi Mamlaka ya Mapato, Fouad Saleem Ahmed al Hareez al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha Zimamoto na Saeed Abdulla Saad (28) ambaye ni askari polisi wa kitengo cha usalama barabarani, pamoja na raia wa Saudi Arabia, Al-Mahri Saeed Mohseens (29) waliachiwa huru baada ya kubainika kuwa hawakuwakupatikana na kosa la kuwafungulia mashitaka.

Tukio la kurushwa kwa bomu hilo lilisababisha mauaji ya watu watatu na wengine zaidi ya 67 kujeruhiwa.

CHANZO: NIPASHE

Duh mwendesha bodaboda amwombe Mungu atende miujiza nchi ya wenye vituko
 
kama kahusika Mungu hawezi kushiriki uovu huo.
 
Uwezo wa kufikiri wa vyombo vyetu vya usalama ndio umeishia hapo, wanachotafuta sasa ni kumjenga Kijana Ambrose na kumuhaidi maisha mazuri na kumlazimisha ataje wanasiasa kadhaa wa upinzani kuwa ndo walimtafutia mabomu na kumtuma kwenda kulipua Kanisa wao wakidhani watakuwa wanaisaidia CCM kumbe hakuna na kamwe uongo hauwezi kuwa ukweli hadi mwisho lazima itabainika.
 
kama kahusika mungu hawezi kushiriki uovu huo.

SOMA HABARI HII HALAFU TAFAKARI!

ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipuabomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijiniArusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwaameibuka.
Kijana huyo ambaye wakatiakizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.
Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watuwengine kumkimbiza.
“Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukatitamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisiwalitusaidia sana,”alisema shujaa huyo.
Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo
walimkuta na mfuko wa rambo,walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia!
Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda nayekituoni.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwastaa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo chakishujaa.
“Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa,si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote,” alisema mtu mmoja aliyejiitaMassawe na kuungwa mkono na wenzake.
 
He he he he, what a multi talented, criminal poor boy.
Only in Tz.
 
Hawa FBI nao kumbe wasanii tu,wameshindwa kutegua hiki kitendawili.?
 
Polisi wamewaachia wote waliokamatwa kuhusika na kulipuwa waumini wa kanisa katoliki Arusha na kubakiwa na mmoja Victor Ambrose ambaye sasa anatuhumiwa na kushtakiwa kwa kupanga njama, kupata bomu, kurusha bomu na kuuwa na kujeruhi. Kijana mwenye miaka 20 ambaye elimu yake darasa la saba, mwendesha bodaboda ameweza kujipatia bomu la kutengenezwa kiwandani, kujua kulitumia bila mafunzo, kulirusha na kuuwa. Je alikuwa ana motives gani? Kwanini? Alinunua au alipata bomu wapi? Nani alimletea Arusha au alilipata Arusha?

Je Victor alikwenda na nani kanisani? nani alikuwa abiria na yuko wapi? Kwanini polisi hawataki kugusia kuhusu abiria wa Victor?
sabas-may10-2013(2)(3).jpg

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewaachia kwa dhamana watuhumiwa wanaodaiwa kurusha bomu kwa waumini waliokuwa wamekusanyika kuanza ibada ya uzinduzi wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Mei 5, mwaka huu, jijini Arusha.

Hata hivyo, watuhumiwa hao wamepewa sharti la kuripoti polisi, pindi watakapohitajika kufanya hivyo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema wamelazimika kuwaachia kwa dhamana kwa kuwa sheria haiwaruhusu kuendelea kuwaweka mahabusu kwa muda mrefu bila kuwafikisha mahakamani.

Hata hivyo, alisema wakiwa nje kwa dhamana, jeshi lake litaendelea na upelelezi na kuwahoji kila litakapokuwa likihitaji kufanya hivyo.

"Tumeamua kuwaachia sababu sheria haituruhusu kuendelea kuwashikilia muda mrefu na lengo letu hasa katika hili tukio hatutaki kumwonea mtu yeyote, ndiyo sababu tunafanya uchunguzi wa kina," alisema.

Alisema hadi sasa hakuna ongezeko la mtu mwingine aliyefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo zaidi ya Victor Ambrose Kalist (20).

Victor alifikishwa mahakamani Mei 13 mwaka huu, mbele ya Kaimu Hakimu Mwandamizi Mkazi wa Arusha, Devotha Kamuzora, kujibu mashtaka mawili ya kuua na kujaribu kuua na kesi yake itatajwa tena Mei 27, mwaka huu.

Watuhumiwa walioachiwa kwa dhamana ni Jassin Mbarak (29) mkazi wa Bondeni Arusha, Joseph Lomayani (18)

dereva wa pikipiki na mkazi wa Kwa Mrombo Arusha, George Batholomeo Silayo (23) mfanyabishara mkazi wa Olasiti na Mohamed Suleiman Said (38) mkazi wa Ilala Dar es Salaam.

Mei 13 mwaka huu, Kamanda Sabas, alisema watuhumiwa watatu raia wa UAE ambao ni Abdul Aziz Mubarak (30) mfanyakazi Mamlaka ya Mapato, Fouad Saleem Ahmed al Hareez al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha Zimamoto na Saeed Abdulla Saad (28) ambaye ni askari polisi wa kitengo cha usalama barabarani, pamoja na raia wa Saudi Arabia, Al-Mahri Saeed Mohseens (29) waliachiwa huru baada ya kubainika kuwa hawakuwakupatikana na kosa la kuwafungulia mashitaka.

Tukio la kurushwa kwa bomu hilo lilisababisha mauaji ya watu watatu na wengine zaidi ya 67 kujeruhiwa.

CHANZO: NIPASHE

...mvua inayostawisha mbigili, ndio inayokuza nafaka..polisi waliomshikilia huyo kijana ndio waliowaachia hao wengine..mambo ya sheria ni magumu kidogo kueleweka, wakati mwingine hata kwa watu wa tasnia hiyo..! tusubiri, na katika subira, kweli hudhihirika..!
 
Sarakasi nyingine ya Liberatus Sabas badaya ya ile SMS ya MULONGO kumalizika.

But for this, they are playing a bad card! Vatican has interest on this case and they are closely watching it.
 
SOMA HABARI HII HALAFU TAFAKARI!

ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipuabomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijiniArusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwaameibuka.
Kijana huyo ambaye wakatiakizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.
Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watuwengine kumkimbiza.
"Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukatitamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisiwalitusaidia sana,"alisema shujaa huyo.
Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo
walimkuta na mfuko wa rambo,walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia!
Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda nayekituoni.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwastaa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo chakishujaa.
"Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa,si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote," alisema mtu mmoja aliyejiitaMassawe na kuungwa mkono na wenzake.

Wasipoongea wanadamu mawe yazungumza kwa niaba .just matter of time
 
see the man on twitter:
Zitto Zuberi Kabwe ‏@zittokabwe 13m
Kabisa “@IsayaEmmanuel: @zittokabwe kwa iyo kazi ya jeshi imekua ikifanywa na polisi na ya polisi ikifanywa na jeshi c ndio?”

View conversation

Hawa FBI nao kumbe wasanii tu,wameshindwa kutegua hiki kitendawili.?

Hakuna cha FBI waliokuja kushughulikia hili ilikuwa ni porojo tu, Zanzbar waliacha Mchoro wa kikatuni kinawatesa hadi leo hawajui waanzie wapi kumshitaki waliyemkamata.
 
This is an example of poor police work. We have time and time again seen master minds eluding justice. It is evident that this young man could not come out with such a plot concidering his background. The man/woman in the shadow could only been uncovered if we could have police force which operates by upholding the noble profession and not this scrupulous "band" we are having. We have seen a police force killing and play the tune of criminals who come under rulling party's umbrella. Now they fail to unfoil a syndicate of hate. Shame
 
Wewe unaowajua wahusika kwanini usitoe taarifa kama unajua huyo hahusiki?

ebu kua muelewa wewe yan unataka kuamn kua kjana wa kitanzania mwenye elimu ya std7 na umri wa miaka 20 anaweza kufanya makosa alioainishwa kwenye kesi yake..tena m2 mwenyewe hana hata exposure yoyote ya kitaifa na hata kimataifa..acha ubshi wa kindez wewe kua mfikirivu
 
Huyo dogo katolewa kafara tu kwa uleule mziki waliozoea kuucheza wa watanzania kuwa na fikra changa wajitazame unapopanda mbegu mmea unaendelea kukua na kukomaa haupendi kuwa mchanga daima.:A S-fire1:
 
Back
Top Bottom