Bomoabomoa TAZARA muda huu, ambulance nazo zipo

Bomoabomoa TAZARA muda huu, ambulance nazo zipo

Mkuu Tazara ipi hiyo maana ninachofahamu kuna kesi Mahakamani iliyofunguliwa na Wananchi hao kupinga kubomolewa bila fidia.
Kesi!?
Nchi hii kwa sasa ni mwendo wa matamko na kushtukizana, sheria pembeni kwanza ....sijui kwa muda gani!
 
Umeongea ki utu uzima sana mkuu, sasa unambomolea mtu nyumba sasa hivi, hiyo master plan yenyewe ndio kwanza wamesema itatolewa June 2016. Ina maana unaweza kununua kiwanja sasa hivi na bado kikawa kwenye eneo lisiloruhusiwa kwa makazi.

Upimaji wa viwanja na mipango miji ilitakiwa viwe miongoni mwa vipaumbele vya nchi. Mbaya zaidi, hata huko ambako hakuna makazi sasa hivi, bado ujenzi holela usiozingatia mpangilio unaendelea na serikali ipo kimya.

Hili zoezi la bomoabomoa limekaa kibabe sana.

Hatuna fursa hata za kujua hiyo master plan inafananaje. Wamezifungia kwenye makabati yao.

Inamaana wananchi waote kuwa hii sehemu sio sahihi kujenga?
 
Kesi!?
Nchi hii kwa sasa ni mwendo wa matamko na kushtukizana, sheria pembeni kwanza ....sijui kwa muda gani!

Mbaya zaidi sheria inakuja kutoa maamuzi wanakutangazia kwamba wanasitisha na zoezi ila kasoro wakati huo tayari kuna watu hawana makazi.
 
Leo tarehe 14.1.2016 Bomoabomoa imeanza kwa wakazi waliopo jirani ya reli ya TAZARA ambapo moja ya vifaa vilivyowasili havitofautiani sana na vile vya ujenzi wa barabara, kilichoongezeka ni ambulance ambayo itakuwa ikibeba wale ambao watapata mshituko.

Wakazi hawa waliwekewa alama ya X tarehe 20/12/2015. They had Only 21 days kutafuta maeneo Mapya.


HAPA NI KAZI TU!!
mwanzo wa ujenzi ni lazima kubomoa, bomoa bovu weka zuri.
 
Back
Top Bottom