Bomoabomoa Dar sasa kubaki ndoto

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,665
239,161
Kauli hii imetolewa na Mstahiki Meya wa jiji hilo Mh Isaya Mwita alipowahakikishia wakazi wa jiji usalama wa nyumba zao .

amesema hatabomoa nyumba iwapo mamlaka zilizopo zilishindwa kusitisha ujenzi wake tangu awali .

" sikubaliani na suala la Bomoabomoa maana linawaumiza sana wananchi masikini " alisema .

chanzo - nipashe .

My Take - Hatimaye kilio cha masikini kimesikika .
 
Hapo sasa ndo atajulikana mamba mana kuna jamaa mmoja wa ccm nilisikia akiongea chadema hairuhusiwi kutekeleza ilani ya chadema ni lazima itekeleze ilani ya ccm sababu ndio serikali iliyopo madarakani hapo sasa
 
Wanaofurahia hili ni wajinga, kama mtu alijenga sehemu isiyotakiwa aondolewe.... twajitaji mji uliopangiliwa, mji wenye barabara nzuri na zenye kupitika, twahitaji nyumba za mjini zionekane kweli za mjini....
Hawa wamachinga na boda boda hawatakiwi city center..... waondolewe
Twajitaji nchi yetu iwe nzuri...
 
kama ni hivyo mbona mamlaka zilitumbua macho tu wakati ujenzi unaanza ? na hatimaye dawasco na Tanesco wakasambaza huduma .
 
Mimi rai yangu ni kwamba hata kama halimashauri zipo chini ya Ukawa...kinachotakiwa ni utawala wa kisheria....lazima sheria za makazi zifuatwe.....kutokufuatwa kwa sheria kwa utawala uliopita hakuhalalishwi kuvunjwa sheria kwa utawala huu....

Hii kama ni kauli ya mstahiki meya basi imekaa kisiasa zaidi kuliko kiutendaji....nadhani anachoangalia ni mtaji wa wapiga kura waliopo kwenye makazi holela kuliko sheria inavyosema......ni jambo lisilokubalika katika nchi inayoendeshwa katika misingi ya sheria na utawala bora......

Anachotakiwa meya ni kusimamia utawala wa sheria bila ya kuangalia masalahi ya chama......

Ina maana meya hatawawajibisha tena wale wavamizi wa maeneo ya wazi kwa kuwa waliachwa katika utawala uliopita....ina maana meya hatawabomolea wale wakazi wakorofi waliojenga nyumba zao kwenye hifadhi za barabara kwa makusudi......Ina maana meya hatawatimua wamachinga wanaopanga bidhaa barabarani hivyo kuleta usumbufu kwa wapita njia..kwa kuwa tu hawakushughulikiwa na utawala uliopita..???

Hii haipaswi kuwa kauli ya meya tuliyemchagua wana DSM kwa ajili ya kutuletea mabadiliko katika jiji letu...yakiwamo hayo ya mpangilio bora wa makazi ya jiji letu........

Mimi nadhani mstahiki meya aweke mihemko ya kisiasa na kichama pembeni na asimame kama mzalendo asimamie sheria bila ya kumuangalia mtu usoni.....kwani mwisho wa siku wananchi hao hao watakuja kumlaumu kwa mpangilio mbaya wa mji wakati wa utawala wake....
 
Ingekuwa ni rahisi kama unavyofikiria hapa zoezi lisingesimamishwa.
 
kama ni hivyo mbona mamlaka zilitumbua macho tu wakati ujenzi unaanza ? na hatimaye dawasco na Tanesco wakasambaza huduma .
Kwa hiyo mkuu kuharibika kwa utawala uliopita hadi kutuletea matokeo haya ndio kunahalalisha utawala huu kuendelea na uharibifu ule ule na kuendelea kupata matokeo yale yale...sasa mantiki ya wananchi kuwapa jiji UKAWA ilikuwa ni nini labda kama mambo yataendelea kuwa vile vile....
 
Mimi rai yangu ni kwamba hata kama halimashauri zipo chini ya Ukawa...kinachotakiwa ni utawala wa kisheria....lazima sheria za makazi zifuatwe.....kutokufuatwa kwa sheria kwa utawala uliopita hakuhalalishwi kuvunjwa sheria kwa utawala huu....

Hii kama ni kauli ya mstahiki meya basi imekaa kisiasa zaidi kuliko kiutendaji....nadhani anachoangalia ni mtaji wa wapiga kura waliopo kwenye makazi holela kuliko sheria inavyosema......ni jambo lisilokubalika katika nchi inayoendeshwa katika misingi ya sheria na utawala bora......

Anachotakiwa meya ni kusimamia utawala wa sheria bila ya kuangalia masalahi ya chama......

Ina maana meya hatawawajibisha tena wale wavamizi wa maeneo ya wazi kwa kuwa waliachwa katika utawala uliopita....ina maana meya hatawabomolea wale wakazi wakorofi waliojenga nyumba zao kwenye hifadhi za barabara kwa makusudi......Ina maana meya hatawatimua wamachinga wanaopanga bidhaa barabarani hivyo kuleta usumbufu kwa wapita njia..kwa kuwa tu hawakushughulikiwa na utawala uliopita..???

Hii haipaswi kuwa kauli ya meya tuliyemchagua wana DSM kwa ajili ya kutuletea mabadiliko katika jiji letu...yakiwamo hayo ya mpangilio bora wa makazi ya jiji letu........

Mimi nadhani mstahiki meya aweke mihemko ya kisiasa na kichama pembeni na asimame kama mzalendo asimamie sheria bila ya kumuangalia mtu usoni.....kwani mwisho wa siku wananchi hao hao watakuja kumlaumu kwa mpangilio mbaya wa mji wakati wa utawala wake....
hata kama sheria ztafuatwa lakini ubinadamu utaangaliwa kwa jicho kali sana , wananchi hawatadhalilishwa kwa malengo ya mtu kupata sifa .
 
Tatizo sheria yoyote itakayopinga na KATIBA inakuwa batili hiyo kujenga kwenye viazio vya maji itakuwaje?
 
Kwa hiyo mkuu kuharibika kwa utawala uliopita hadi kutuletea matokeo haya ndio kunahalalisha utawala huu kuendelea na uharibifu ule ule na kuendelea kupata matokeo yale yale...sasa mantiki ya wananchi kuwapa jiji UKAWA ilikuwa ni nini labda kama mambo yataendelea kuwa vile vile....
kwa mfano unaweza kunitajia hapa faida ambayo serikali imepata kwa kuwabomolea kishenzi namna ile wananchi wa mkwajuni ? au chochote kile ambacho serikali imefaidi kwa unyama ule , kwanini hakukuwa na uungwana katika zoezi lile ? serikali ilisukumwa na nini kuwa na haraka kiasi kile ?
 
Kauli hii imetolewa na Mstahiki Meya wa jiji hilo Mh Isaya Mwita alipowahakikishia wakazi wa jiji usalama wa nyumba zao .

amesema hatabomoa nyumba iwapo mamlaka zilizopo zilishindwa kusitisha ujenzi wake tangu awali .

" sikubaliani na suala la Bomoabomoa maana linawaumiza sana wananchi masikini " alisema .

chanzo - nipashe .

My Take - Hatimaye kilio cha masikini kimesikika .
Tuache siasa za kitoto kwenye mambo yanayohusu sheria
 
Kauli hii imetolewa na Mstahiki Meya wa jiji hilo Mh Isaya Mwita alipowahakikishia wakazi wa jiji usalama wa nyumba zao .

amesema hatabomoa nyumba iwapo mamlaka zilizopo zilishindwa kusitisha ujenzi wake tangu awali .

" sikubaliani na suala la Bomoabomoa maana linawaumiza sana wananchi masikini " alisema .

chanzo - nipashe .

My Take - Hatimaye kilio cha masikini kimesikika .
Huyo Meya wenu taka taka hajui kama hana mamlaka ya kuzuia bomoa bomoa! Tena asianze kujichanganya atatandikwa...
 
kwa mfano unaweza kunitajia hapa faida ambayo serikali imepata kwa kuwabomolea kishenzi namna ile wananchi wa mkwajuni ? au chochote kile ambacho serikali imefaidi kwa unyama ule , kwanini hakukuwa na uungwana katika zoezi lile ? serikali ilisukumwa na nini kuwa na haraka kiasi kile ?
Hata mimi sikupendezwa na namna serikali ilivyolichukulia suala la bomoa bomoa ya wakazi wa mkwajuni ingawa wale wananchi wananchi walikiuka sheria ya makazi.....Hadi kufikia pale ina manisha kuwa kulikwa na uzembe wa kiutendaji katika manispaa zetu kwani yale makazi hayakuota kama uyoga.....na kwa uzembe huo huo uliokuwa ukifanyika katika manispaa za miji mbali mbali ndio sababu wananchi wengi wakawachagua UKAWA mimi nikiwa mmoja wapo.....shauku kubwa ni kuiona miji ikiwa katika hali ya mabadiliko makubwa.....

Makazi holela ni changamoto kubwa inayoikumba manispaa za jiji la Dar es salaaam na kuishughulikia kwake kunahitajika busara za hali ya juu kwani inagusa maisha ya wananchi wengi wenye vipato vya hali ya chini...lakini pamoja na hayo mambo hayapaswi kuachws hivyo bali yanatakiwa yachukuliwe hatua za busara......

Alichotakiwa kutuambia mstahiki meya ni ambavyo yeye angeshughulikia hayo mambo tofauti na uatawala uliopita....
 
ni hivi , labda kwa lugha rahisi ni kwamba hakuna mwananchi atakayekomolewa .
 
Back
Top Bottom