Uchaguzi 2020 Namba 06: Aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita amechukua fomu kuomba ridhaa kuwania Urais kupitia CHADEMA

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Aliyewahi kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita amekuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania nafasi ya Urais Tanzania kupitia CHADEMA

Isaya anayekuwa mgombea wa 6 kuchukua fomu hiyo Kaulimbiu yake ni "Mageuzi ya mfumo wa elimu, upanuaji na uongezaji wa ajira kwa vijana na mchakato wa Katiba Mpya"

EceawwIWsAAUmkm.jpg

Isaya Mwita amesema haya

Mipango mibaya ya Chama kilichopo madarakani ndio maana vijana wengi nchini hawana ajira, kilimo ndio sekta pekee inayoweza kuajiri Watanzania wengi, nikichaguliwa nitalisimamia kuhakikisha vijana wanaomaliza vyuo vikuu wanapata ajira.

Taifa letu lina changamoto kimataifa na hata ndani, kazi yangu kubwa ni kwenda kuhakikisha nchi ina mahusiano mazuri na wadau wa Maendeleo ndani na nje.

Katiba mpya ndio jambo la kwanza nitakaloanza nalo endapo Chama changu kitaniamini na kunipitisha na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania, Katiba itaheshimiwa na kila mtu
 
Lisu huko aliko atatamani kuangua kilio alikuwa aki ji overstate kuwa yeye ndio yeye hakuna mwingine hiyo nafasi ona sasa watu kibao wanainuka.Meseji sent kwake
Hakuwahi kujisifu popote, tatizo Lumumba mnamuogopa sana Lissu, na dalili zinaonesha bora mjiandae kisaikolojia mapema.
 
Aliyewahi kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita amekuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania nafasi ya Urais Tanzania kupitia CHADEMA

Isaya anayekuwa mgombea wa 6 kuchukua fomu hiyo Kaulimbiu yake ni "Mageuzi ya mfumo wa elimu, upanuaji na uongezaji wa ajira kwa vijana na mchakato wa Katiba Mpya"

Isaya Mwita amesema haya

Mipango mibaya ya Chama kilichopo madarakani ndio maana vijana wengi nchini hawana ajira, kilimo ndio sekta pekee inayoweza kuajiri Watanzania wengi, nikichaguliwa nitalisimamia kuhakikisha vijana wanaomaliza vyuo vikuu wanapata ajira.

Taifa letu lina changamoto kimataifa na hata ndani, kazi yangu kubwa ni kwenda kuhakikisha nchi ina mahusiano mazuri na wadau wa Maendeleo ndani na nje.

Katiba mpya ndio jambo la kwanza nitakaloanza nalo endapo Chama changu kitaniamini na kunipitisha na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania, Katiba itaheshimiwa na kila mtu
Mungu ibariki Chadema
 
Kwani hawa viongozi wa CDM nafasi ya Urais wa Jamhuri wameionaje. Kama kutoka Sinza madukani kwenda Club Ambiance au?

Waache kuivunjia heshma hii ofisi ya 60m heads + it's blessed natural resources.
 
Mwita angechukua form ya Ubunge tu. Mimi sina undugu na shekhe Yahya lakini sioni huyu ndugu akipitishwa na Chama. Urais haufanyiwi majaribio
 
Tuna imani naye sana hasa sisi wakazi wa Vijibweni baada ya kukesha naye siku 3 tukilinda kura.....hajatuangusha.... kapitia mengi kiasi cha hata kuugomea hata mzigo uliokuwa mezani.
 
Mwita angechukua form ya Ubunge tu. Mimi sina undugu na shekhe Yahya lakini sioni huyu ndugu akipitishwa na Chama. Urais haufanyiwi majaribio
kanuni zinasemaje mkuu, kwamba ukiomba urais kura zikigoma huwezi kurudi kuchukua ya Ubunge? maana uchaguzi ni karata
 
Back
Top Bottom