Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haiwezi kuzuia Meya wa DSM,Isaya Mwita kuondolewa kwenye nafasi yake kwa sababu hakuna uthibitisho wa uwepo wa kikao cha kumuondoa madarakani wala hasara atakayoipata endapo akiondolewa.
Yasema mwombaji hajatoa sababu za msingi za kukidhi vigezo vitatu vya kwanini abaki kwenye nafasi hiyo.
Hakimu asema maombi yamekosa ushahidi kuwa kulikuwa na kikao kinachokusudia kumwondoa madarakani.
“Mahakama hii inatupilia mbali hoja za kutaka muombaji (Mwita) kubaki madarakani kwa sababu hoja za Wakili wa muombaji hazina miguu ya kusimamia kwa kushindwa kufata vigezo ikiwemo uwepo wa kikao cha kutaka kumtoa madarakani”- Hakimu Janeth Mtega.
Uamuzi wa Mahakama kusema haiwezi kuzuia Mwita kuondolewa kwenye Umeya unatokana na maombi yake ambayo aliyawasilisha Jan 6, 2020 ya kutaka kuzuia Kikao cha Baraza la Madiwani wasijadili ajenda ya kumng’oa, kesi ya msingi ya mchakato wa kumuondoa kukiuka Utaratibu imepangwa Jan 13.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kikao Cha Jana hakikua na uhalali wa kumuondoa madarakani hivyo jumatatu nitaripoti kazini kama kawaida.
"Nakusudia kuwashtaki wote waliohusika kufoji saini ya Diwani ambaye yupo nje ya nchi na mmoja wa washtakiwa Hawa atakuwa Kigogo mkubwa tu katika Jiji la Dar es Salaam" Isaya Mwita Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
Leo asubuhi nimeripoti ofisini japo mkurugenzi ananipa gari sijui shida nini hivyo nimemuandikia Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam aniletee gari kwa haraka mno" Mstahiki Meya wa Jiji Isaya Mwita.
Pia soma
- Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Meya anyang’anywa gari, ofisi yafungwa. Adai kuwa yeye bado ni Meya halali