Bomoa bomoa yaja waliovamia kiwanda cha cement

dinongo

JF-Expert Member
Jun 25, 2022
814
1,047
Bomoabomoa yaja waliovamia kiwanda cha Wazo
Wednesday August 31, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akizungumza na baadhi ya wakazi wa maeneo ya Chasimba, Chatembo na Chachui katika Kata ya Wazo.

Bomoabomoa kubwa inakuja kwa waliovamia maeneo yanayomilikiwa na kiwanda cha Wazo.

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Bomoabomoa kubwa inakuja kwa waliovamia maeneo yanayomilikiwa na kiwanda cha saruji cha Wazo kilichopo katika Kata ya Wazo jijini hapa.

Hatua hiyo inafuatia kushindwa kwa wananchi hao kulipia maeneo waliyovamia na Serikali kutangaza kujitoa.

Wakazi hao ni wale wanaoishi maeneo ya Chasimba, Chatembo na Chachui katika Kata ya Wazo jijini humo.

Licha ya Serikali kuwawekea dhamana wananchi hao wapatao 4,070 ili wayanunue maeneo hayo ndani ya miezi sita, ni wananchi 39 tu sawa na asilimia tisa tu ndio wamelipia hadi sasa.

Akizungumza leo Jumatano Agosti 2022, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla baada ya kupokea taarifa ya kufanyika kwa kazi hiyo kutoka kwa uongozi wa kiwanda.

Amesema anawapa wananchi hao mwezi mmoja kukamilisha malipo hayo.

"Katika kulitekeleza hilo watapita watu nyumba kwa nyumba kutoa ankara ya malipo na muhusika utatakiwa kusaini na kama hautaki ndio tutajua kuanzia hapo," amesema Mkuu huyo wa mkoa.

Makalla amesema baada ya hapo Novemba 1, 2022 watawakabidhi kiwanda eneo lao kwa ajili ya utekelezaji wa hukumu waliyoshinda kuwa wamiliki halali wa eneo hilo kufanya wanavyoona.

"Serikali tuliamua kutumia busara na huruma ili wananchi msiondolewe lakini mmeshindwa, tutakachokifanya ni kukabidhi majina tisa ya waliolipa na tutawapatia hati hao wengine watafute pakwenda," amesema Makalla.

Pia, ameonya suala hilo kuingiliwa na siasa na kueleza kuwa kuna watu wamekuwa wakipita kuwahadaa wananchi kuwa wasilipe na hakuna atakayewaondoa jambo ambalo halikubaliki kukaa kwenye hati ya mtu mwingine.

Kwa upande wao wananchi akiwemo, Fatma Saleh ameomba waongezewe muda kwani hata ambao hawajilipa sio kwamba wamependa bali ni kutokana na kuwa na vipato vidogo.

Stephano Kisimbo amesema uzito wa kulip umetokana na mkanganyiko ambapo awali waliambiwa wangelipa Sh1,000 hadi 2,000 kwa mita za mraba lakini ilipokuja kibadilishwa na kiwa Sh6,419 kwa mita za mraba ndio maana wakashindwa wengi kulipa.
 
Kwamba unapewa eneo alafu utalipia baadae au walivamia alafu wakapewa upendeleo wa kulipia ili yawe yao
 
Kule Kinondo yalishawakuta, sasa ni Wazo, next stop sijui itakuwa wapi, Makalla ana allergy na walalahoi..
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Wakazi was Chasimba,Chachui wengine walijenga mijumba ya kupangisha na walikuwa wanapiga pesa imekuweje kushindwa kulipa kidogo kidogo?
 
Hivi hii serikali ni ya watu au ni kwa ajili ya nan?yaani watu zaidi ya 4000 watolewe?.Tozo mmeweka kila mahali lakini kuwasaidia wananchi mnashindwa.
 
Hivi hii serikali ni ya watu au ni kwa ajili ya nan?yaani watu zaidi ya 4000 watolewe?.Tozo mmeweka kila mahali lakini kuwasaidia wananchi mnashindwa.
Watu wamevamia eneo la mtu(WAZO) mahakama imethibitisha ni eneo la waz0. Badala ya kufukuzwa na kupoteza nyumba zaowamepewa nafasi wanunue wawe waamiliki halali, wameshindwa. Bado unalaumu watu hao kuondolewa? Je lingekuwa eneo lako ungelitoa sadaka?
 
Watu hawajavamia bali waliuziwa na matapeli wa wizara ya ardhi.Watu wamekaa zaidi ya miaka 50 leo hii uwambie wamevamia? Kwanini hawakuambiwa mapema?
 
Mbona ni pesa ndogo kabisa! Wanashindwa nini jamani?
 
Watu wamevamia eneo la mtu(WAZO) mahakama imethibitisha ni eneo la waz0. Badala ya kufukuzwa na kupoteza nyumba zaowamepewa nafasi wanunue wawe waamiliki halali, wameshindwa. Bado unalaumu watu hao kuondolewa? Je lingekuwa eneo lako ungelitoa sadaka?
Ujamaa umeisumbua nchi yetu, utatusumbua sana
 
Hivi hii serikali ni ya watu au ni kwa ajili ya nan?yaani watu zaidi ya 4000 watolewe?.Tozo mmeweka kila mahali lakini kuwasaidia wananchi mnashindwa.
Wakati mnavamia mliomba muongozo wa serikali?

Iweje leo muombe msaidiwe na serikali?

Mkule jeuri yenu.

Yani 6k kwa sqm inawashinda? Bora muondoke matajiri waje kuyachukua maeneo.
 
Back
Top Bottom