KERO Karavati ya wananchi imesahaulika?

KERO Karavati ya wananchi imesahaulika?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Karavati hili lilijengwa kwa nguvu na mchango wa wananchi miaka mingi iliyopita, lakini hadi leo bado lipo katika hali inayotia wasiwasi mkubwa.

📍 Mahali: Mkoa wa Pwani, Mkuranga, Kata ya Vikindu, Kitongoji cha Madafu.

📍 Linaunganisha maeneo ya Chatembo na Madafu kupitia kiwanda cha samaki.
Kinachoumiza zaidi, eneo hili lipo ndani ya Jimbo la Waziri wa Ujenzi, lakini wananchi bado wanapita kwenye mazingira yenye hatari na miundombinu isiyo salama.

Wananchi wanauliza:
âť“ Je, mpaka litokee janga ndipo hatua zichukuliwe?
âť“ Mbona miundombinu muhimu kama hii imeachwa kwa muda mrefu?
âť“ Sauti za wananchi wa Madafu na Chatembo zinasikika kweli?

Tunaomba mamlaka husika, viongozi wa jimbo na wizara ya ujenzi wafike eneo hili na kutoa suluhisho la haraka kwa wananchi.

PXL_20260519_142857813.jpg
 
Back
Top Bottom