Bomoa bomoa; Rwakatare na Mengi wapeta

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,859
Hii ni habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Jambo leo la leo tarehe 06/01/2016 ambalo limeandika "Lwakatare, Mengi waponea tundu la sindano."

Gazeti hili pia limenunuliwa na Manji.

Chanzo: Jamboleo

Hii ndio Tanzania bwana!

UKAWA, tunataka kusikia maoni yenu maana Dar kwa sasa ni kama iko chini yenu mkiwa na madiwani wengi.

Madiwani wa UKAWA katika vikao muwabane wakurugenzi watoe sababu za hizo nyumba kutovunjwa.
 
Last edited by a moderator:
Hii ni habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Jambo leo la leo tarehe 06/01/2016 ambalo limeandika "Lwakatare,Mengi waponea tundu la sindano."

Gazeti hili pia limenunuliwa na Manji.

Chanzo:Jamboleo
Hii ndio Tanzania bwana!

UKAWA, tunataka kusikia maoni yenu maana Dar kwa sasa iko chini yenu.
a iseee...kumbe bomoa bomoa inasimamiwa na UKAWA
 
Bavicha kwanini usilete habari kamili? kwanini unaleta kidaku? Bomoa bomoa haifanywi kuwakomoa watu..
 
nI
Hii ni habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Jambo leo la leo tarehe 06/01/2016 ambalo limeandika "Lwakatare, Mengi waponea tundu la sindano."

Gazeti hili pia limenunuliwa na Manji.

Chanzo: Jamboleo

Hii ndio Tanzania bwana!

UKAWA, tunataka kusikia maoni yenu maana Dar kwa sasa ni kama iko chini yenu mkiwa na madiwani wengi.

Madiwani wa UKAWA katika vikao muwabane wakurugenzi watoe sababu za hizo nyumba kutovunjwa.
Nilijua kuwa zoezi lile ni kuwakomoa WALALA HOI TU tutaisoma namba mwaka huu
 
Wasio na sauti ndo wanaoumia, wamewatumia kipindi cha uchaguzi sasa hawana thamani hadi 2020
 
Kama ulifikiri Mengi angebomolewa nyumba utakuwa una tatizo la akili
 
Kwa Lwakatare huu ni sehemu ya MUUJIZA kwa waumini wake, ategemee kuongeza sadaka na waumini kwenye kanisa lake, BWANA AMETENDA, NGUVU ZA MAGUFULI ZIMESHINDWA.
 
Shukrani kwa wema gani mlimfanyia? Nyie someni namba...Hakuna namna. Wambieni UKAWA wawajengee nyumba kwenye maeneo yaliyopimwa....Hatutaki wavunja sheria hapa Dar. Mlimchagua Mamvi ili aendelee kulea lea genge la wavunja sheria sio?
Wakati wanavunja sheria mlikuwa wapi?Nani wa kusimamia sheria?Mko madarakani kusimamia sheria au kusubiri watu wavunje sheria na kisha muwaazibu?Hao wenye hela hawajavunja sheria?Ovyo kabisa nyie watu!
 
Shukrani kwa wema gani mlimfanyia? Nyie someni namba...Hakuna namna. Wambieni UKAWA wawajengee nyumba kwenye maeneo yaliyopimwa....Hatutaki wavunja sheria hapa Dar. Mlimchagua Mamvi ili aendelee kulea lea genge la wavunja sheria sio?
Shukrani kwa wema gani mlimfanyia? Nyie someni namba...Hakuna namna. Wambieni UKAWA wawajengee nyumba kwenye maeneo yaliyopimwa....Hatutaki wavunja sheria hapa Dar. Mlimchagua Mamvi ili aendelee kulea lea genge la wavunja sheria sio?

koma ukomae aliyesema nyumba za ukawa zinabolewa tu nani? Nyie ndo mnajenga chuki.
 
Kanywe VIROBA,Unajivunia kuwa MLALAHOI..............
Najivunia ULALAHOI kwa vile nimefanywa niwe hivyo na sina njia ya kujivua.......hata hicho kiroba cha kuzidi kuuvaa huo ulalahoi bahati mbaya sina uwezo nacho! mie sio mwana wa mbele kwa mbele!
 
Wasio na sauti ndo wanaoumia, wamewatumia kipindi cha uchaguzi sasa hawana thamani hadi 2020

Well, naamini hao wasio na sauti itakuwa wakati wao mwafaka wa kujitafakari na kujielewa na kujitambua kuwa nani anajali masalahi yao.

Vinginevyo wataendelea kutumika kama hadithi ya karai katika ujenzi wa Gorofa ama hekalu (palace). Linanunuliwa likuwa jipya kabisa na kutumika kubebea zege mpka linabondeka bondeka kabisa. Na inapokuj siku ya ufunguzi wa jengo karai huwa kazi yake imekwisha na ni uchafu. Huwa halitakiwi hata kuonekana upenuni mwa uwanja wa jengo lisije kuabisha mbele ya watu maarufu (VIP) na wageni waalikwa.

Hivyo imefika mahali hao wanyonge wajielewe kwanza na ikibidi wajipange kupambana kivya vyao. Vinginevyo wataendelea kutumika sana na CCM mpaka watie akili.
 
Back
Top Bottom