Bomoa bomoa kwa walala hoi wakati waishio NHC asilimia 70 ni matajiri

UncleBen

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
9,668
12,256
Heshima kwenu wakuu,

Nipende kusema tu wazi kwamba mimi ni mmoja wa watu wanaopenda kutii/kufuata sheria taratibu za mamlaka yeyote halali.

Leo tume sikia kuna mtanzania mwenzetu amefungua kesi mahakamani kupinga zoezi la ubomoaji wa nyumba unaofanywa na serikali yetu inayojiita ni sikivu na rafiki wa maskini ,sio nia yangu kupinga linalofanywa na serikali yetu lakini kuna mambo inabidi iyazingatie , unavunja nyumba ya mtu unampa kiwanja mabwepande sehemu ambayo kwa vyovote vile huduma za kijamii hazijaratibiwa vizuri, hakuna nyumba akalale kwenye majani?

Naomba nitoe pendekezo badala ya kuwapeleka mabwe pande sasa ni wakati muafaka wa kuwaondoa matajiri wote wanaoishi NATIONAL HOUSING na kuwapa maskini nyumba hizo.
IMEFIKIA MAHALI KWAMBA NI RAHISI SANA KUTEMBEA NA MKE WA RAISI KULIKO KWA MWANANCHI WA KAWAIDA KUPATA NYUMBA HIZO.

NHC SIO JIPU TU BALI NI KANSA AMBAYO HATA MABINGWA WA OCEAN RD HAWALIWEZI SERIKALI HII AMBAYO INAJIPAMBANUA NI SIKIVU NAOMBA MLIANGALIE HILI ..
 
Unataka iwajengee iwalipie ifilisike, wangapi wataweza kulipa 10% deposit kama m 6 mpaka 8 na baada ya hapo walipe laki 2 kila mwezi , your options are sympathetic but not realistic otherwise NHC itafirisika , middle class ndo inapata nyumba for now
 
nyumba za NHC ulizo kariri ni hizi zinazojengwa sasa hivi ,hao wahindi na waswahili walio jazana kwenye hizo nyumba wanalipa hiyo deposit ya 10% ??? Au ni rent tu tena rent yenyewe hata mmachinga anaweza kulipa Hiyo kauli yako ya midle class ndio wanapata imenitia kichefu chefu ,kwa hiyo maskini waendelee kuteseka?? Wakati majority ya nyumba za NHC kodi yake walau maskini wanaweza kulipa japo wanao ishi ni matajiri ,sasa nyie mnaojiita midle class muondoke kwenye hizo nyumba Low cost ,mkalipie hizo unazo sema za deposit ya 10% na rent laki mbili
 
Last edited:
NHC ni zaidi ya jipu, wahindi wanafanya kuachiana nyumba tu, mtu alieweka mkataba na NHC miaka ya 70 amnamuachia rafiki baada ya yeye kuhujumu uchumi na kupata hela za kwenda canada na uingereza, anakaa mtoto hadi kitukuu, kwa kifupi hakuna muhindi aliehama nchi akarudisha ufunguo wa nyumba NHC, Wazawa wakienda kuuliza nyumba nyumba NHC inaonekana kama chizi vile, anatafuta kisicho wezekana n.
 
Nasikia kabla ya uhuru wahindi wengi walikua wanamiliki hizi nyumba za NHC after uhuru ikaingiwa contract kwamba ziwe chini ya serikali then hawa jamaa wapangishiwe!!!ndio mana mpaka leo Tanzania nzima wahindi wanakaa nyumba za NHC zilizopo city centers (NASIKIA)
 
Na hili ndio linatokea hata kwa wazawa waliopewa hizo Nyumba hawaziachii na wakiziacha huwapa ndugu zao ,ifike mahali serikali iweke limit ya mtu kuishi nyumba hizo walau miaka kumi na pia waangalie upya utaratibu wa kuwapa watu hizi nyumba
 
Nasikia kabla ya uhuru wahindi wengi walikua wanamiliki hizi nyumba za NHC after uhuru ikaingiwa contract kwamba ziwe chini ya serikali then hawa jamaa wapangishiwe!!!ndio mana mpaka leo Tanzania nzima wahindi wanakaa nyumba za NHC zilizopo city centers (NASIKIA)
Inaweza ikawa ulichoskia ni sahihi mkuu ,yaani nyumba ni za serikali ila umiliki ulikua kwa wahindi ?? Ni ubia waliingia na serikali au ilikuaje ??
 
Nasikia kabla ya uhuru wahindi wengi walikua wanamiliki hizi nyumba za NHC after uhuru ikaingiwa contract kwamba ziwe chini ya serikali then hawa jamaa wapangishiwe!!!ndio mana mpaka leo Tanzania nzima wahindi wanakaa nyumba za NHC zilizopo city centers (NASIKIA)
Wahindi wengi ndio waliojenga zile nyumba na wakiwa wanaishi hapo ilikuwa taabu kuwahamisha, ila baada ya kutaifishwa na serikali kulikuwa na VIGEZO NA MASHARTI ambavyo ni lazima vifuatwe, ikiwa ni pamoja na kusign mkataba wa upangishwaji amabao ndio jipu, haufuatwi kabisa, na pia kuna baadhi ya wahindi walishadai nyumba zao na zikarudishwa ndio maana kuna majengo mengine mjini hayana rangi za NHC kwa kuwa yamerudishwa kwa wamiliki waliojenga. Tatizo ni kwa nini tangu 60's mpaka leo ni hao hao waliopangishwa mwanzo, hawahami?, hawafi? hawazeeki? hawahami mkoa? JIPU. Mikata iwe na UKOMO.
 
Kwa manufaa ya kizazi kijacho inabidi huu mkataba unagaliwe upya ili tuondoe haya matabaka ya kikaburu katika jamii yetu ,vinginevyo tunapo elekea naona kabisa kukiibuka vita kati ya walio nacho na wasio nacho na ole wao wale ambao hakuweza kuepusha hili
 
nyumba za NHC ulizo kariri ni hizi zinazojengwa sasa hivi ,hao wahindi na waswahili walio jazana kwenye hizo nyumba wanalipa hiyo deposit ya 10% ??? Au ni rent tu tena rent yenyewe hata mmachinga anaweza kulipa Hiyo kauli yako ya midle class ndio wanapata imenitia kichefu chefu ,kwa hiyo maskini waendelee kuteseka?? Wakati majority ya nyumba za NHC kodi yake walau maskini wanaweza kulipa japo wanao ishi ni matajiri ,sasa nyie mnaojiita midle class muondoke kwenye hizo nyumba Low cost ,mkalipie hizo unazo sema za deposit ya 10% na rent laki mbili
Ninazoongelea hapa ni NHC za kununua, huku ukilipa kodi taratibu, niambie maskini mwenye uwezo wa kulipa kodi ya laki mbili kwa mwezi akiwa tayari kishatoa m 6 ndo maana nakwambia hii ni kwa middle class
 
Mkuu mbona bado hujanielewa siongelei nyumba Mpya za NHC ,naongelea nyumba za zamani utafutwe utaratibu mpya wa kuzigawa hizi nyumba ,mimi ni maskini na sio sifa kuwa masikini ila nina flat ya national housing ninayolipa kodi ya elfu 40 tu ,ni maskini wangapi wa Tanzania wenye uwezo wa kulipia hizo nyumba lakini hawawezi kuzipata kwa sababu ya ukiritimba,ukabila ,utaifa ,ulio kithiri kwenye ugawaji wa hizi nyumba
Lengo la kuanzisha shirika hili ilikua kuwasaidia watanzania maskini ila imekua kinyume chake
 
Umaskini, kiasi kikubwa ni lawama kwa serikali kwa ukosefu wa elimu, lakini pia ni hali ya kutokuwa na maarifa ya kupata mbinu ya kukuza kipato, hivyo basi umasikini huambatana na ujinga pamoja na uzembe, na mipango mibovu - hivi ndivyo ninnayowaona maskini wengi _ japo najua wengine wamebanwa na system
 
Mkuu mbona bado hujanielewa siongelei nyumba Mpya za NHC ,naongelea nyumba za zamani utafutwe utaratibu mpya wa kuzigawa hizi nyumba ,mimi ni maskini na sio sifa kuwa masikini ila nina flat ya national housing ninayolipa kodi ya elfu 40 tu ,ni maskini wangapi wa Tanzania wenye uwezo wa kulipia hizo nyumba lakini hawawezi kuzipata kwa sababu ya ukiritimba,ukabila ,utaifa ,ulio kithiri kwenye ugawaji wa hizi nyumba
Lengo la kuanzisha shirika hili ilikua kuwasaidia watanzania maskini ila imekua kinyume chake
Kiuhalisia na ukweli mpu hizo nyumba ni za hao wahindi walio nyang'anywa majengo yao kipindi cha azimio la Arusha wakaachwa wajiegeshe kwenye hizo nyumba, na wanalipishwa kodi kukaa kwenye majumba yao, nyumba zingine mpaka jina la ukoo unaliona, hizo nyumba si jasho la serikali yetu ni unyang'anyi mimi naona sawa wakiishi hapo , na wale masikini wenye viungo vyote wanao ng'ang'ana kuwa mjini waende vijijini wajiajili kwa kilimo, ni moja kati ya biashara nziri shida zingine za kujitakia
 
Mkuu huu utakua mjadala mpya kabisa tukisema tulijadili kwa mtazamo wako kwamba watu waende vijijini wajiajiri na kilimo ,kwa mtazamo wangu utaratibu wa kutaifisha hizo nyumba haukua wa maana kama zilitaifishwa na watu hao hao wakapewa nyumba hizo na ndio maana nimesema ni muda muafaka sasa serikali kuliangalia hili ,mbona serikali ilitaifisha pia shule za seminary lakini kanisa halikupewa kipaombele kwa wanafunzi wakristo kisa tu shule ilikua chini ya kanisa ???
 
Back
Top Bottom