Kikwete amwambia Magufuli aache Ubabe kwenye bomoa bomoa; Magufuli ataaminika tena? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amwambia Magufuli aache Ubabe kwenye bomoa bomoa; Magufuli ataaminika tena?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bazobonankira, Mar 21, 2011.

 1. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Rais Jakaya Kikwete leo amemgeukia mbogo waziri Magufuli kwa kumwambia waziwazi kuwa aache ubabe na mpango wake wa Bomoa Bomoa wakati wa ziara ya Rais alipotembelea wizara ya Ujenzi leo hii.

  Huu unaonekana ni msumari mwingine kwa mpiganaji Magufuli, kufuatia msumari wa kwanza uliogongelewa na Pinda wakati akiwa Bukoba hivi karibuni.

  Hapo awali magufuli aliwataka 'Wajenga Hovyo" kando kando ya hifadhi za barabara kuwa wanabomoa wenyewe kwa kipindi kifupi. Now Mheshimiwa JK amemuagiza kuwapa "Hata miaka miwili" na kuwalipa na fidia.

  Kazi inaendelea.... Je, Magufuli kuamua kujiuzuru kama tetesi zilivyosambaa hapo awali?

  Binafsi, sikubaliani na utaratibu huu wa kuendesha vikao na kufanya maamuzi hadharani. Masuala haya ya Pinda, JK na hata Magufuli mwenyewe wangeweza kuyafanya na kukubaiana katika vikao vya baraza la mawaziri badala ya kutengeneza sinema hadharani.

  I striongly believe they are trying to create "storyboard" for winning public attention kwenye masuala yasiyo ya msingi na kusahau yanayogusa maisha yao moja kwa moja.


  Sadick Mtulya na Gedius Rwiza
  RAIS Jakaya Kikwete amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kuzingatia utu pamoja na historia ya eneo husika wakati wa utekelezaji wa bomoabomoa kwenye hifadhi ya barabara nchi nzima.

  Pia, amemuagiza Dk Magufuli kuwalipa wote wanaostahili fidia na kwamba wasiangalie tu mazingira ambayo yataepusha mzigo wa gharama kwa Serikali.Kauli hiyo ya Rais Kikwete imekuja siku chache baada Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kusimamisha bomoabomoa hiyo mpaka shauri hilo litakapoamuliwa vinginevyo na Baraza la Mawaziri.

  Rais Kikwete alisema hayo jana baada ya Dk Magufuli kumuomba Rais Kikwete ampe ruhusa ya kuendelea na ubomoaji huo. Jana, Rais alikutana na watendaji wa Wizara ya Ujenzi katika mfululizo wa ziara zake za kukagua utekelezaji wa maagizo yake.

  "Mheshimiwa Rais, niliapa kulinda sheria na Katiba ya nchi, hivyo ninaomba nipewe ruhusa kutekeleza sheria ya kubomoa nyumba zilizojengwa ndani ya hifadhi ya barabara,'' alisema Dk Magufuli.

  Waziri Magufuli amekuwa akisisitiza kwamba waliojenga ndani ya barabara wamevunja Sheria namba 13 ya mwaka 2007 na kwamba hawastahili kulipwa fidia.

  Hata hivyo, Rais Kikwete akijibu maombi hayo alisema: ''Hili naliongea kwa umakini kwani nataka nieleweke vizuri. Bomoabomoa ipo. Usilegee katika kutekeleza sheria, lakini uangalie ubinadamu katika bomoa hiyo pamoja na historia ya eneo husika.

  Pia muwalipe wote wanaostahiki kulipwa fidia na msiwalipe wale wasiostahiki na msiangalie unafuu wa Serikali pekee.''

  Rais Kikwete alisema itakuwa ni jambo la kushangaza endapo hata vitu vya kihistoria, ikiwamo nyumba na sanaa mbalimbali ambazo zimejengwa katika hifadhi ya barabara zitabolewa.

  Kuhusu utu, alisema kulingana na ubinadamu, kubomoa nyumba ambayo imejengwa na kukaliwa kwa muda mrefu harakaharaka itakuwa ni kinyume na haki za binadamu... "Ikifikia hatua ni lazima nyumba hiyo ibomolewe, toeni muda wa kutosha ili wajiandae kwani kuwatoa kwa haraka itakuwa ni kinyume na haki za binadamu.

  Hata hivyo, Rais Kikwete aliagiza iundwe tume maalumu na ya kudumu itakayokuwa ikifuatilia hifadhi za barabara nchini kote akiwaagiza watendaji wa wizara hiyo kuwa wakali katika kusimamia fedha za miradi ya barabara na kuwataka wasiwaonee haya wanaosababisha kutokamilika au miradi kutekelezwa kinyume na makubaliano.

  "Pamoja na mambo mengine, endeleeni kutupia macho ya umakini. Rushwa imezidi na inasababisha kuharibika kwa barabara kutokana na kupitishwa kwa mizigo mizito kinyume na utaratibu,'' alisema.

  Pinda alichomwambia Magufuli Chato
  Machi 6, mwaka huu akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Chato, mkoani Kagera, Waziri Mkuu Pinda pamoja na kumsifu Dk Magufuli kwa utendaji wake, alimwagiza kusimamisha bomoabomoa zote hadi hapo Serikali itakaposema vinginevyo.

  Tamko la Pinda lilitokana na hatua aliyoichukua Dk Magufuli Januari 13, mwaka huu ya kutoa ilani kwa wananchi waliojenga nyumba ndani ya hifadhi ya barabara kuanza kubomoa nyumba hizo mapema na kwamba wasitegemee kulipwa fidia.Dk Magufuli pia alimtaka Meya wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na madiwani kujipanga na kuondoa nyumba zilizo katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya njia ya mabasi yaendayo kasi ili kuwawezesha makandarasi kuanza kazi hiyo.

  Pinda alisema kasi aliyoanza nayo Magufuli katika wizara yake mpya imeitisha Serikali... "Rais aliona kwenye barabara panalegalega na kumrudisha Magufuli kwenye wizara hiyo. Huyu Serikalini tunamwita ‘buldoza' hata hivyo, ameanza kwa speed (kasi) kubwa na tumwemwagiza asimamishe zoezi hilo mpaka litakapojadiliwa na Baraza la Mawaziri."

  Alisema baraza hilo litafanya kikao ili kuangalia upya maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya bomoabomoa na kusema kuwa kabla ya kuruhusu kuendelea lazima wakubaliane kwanza kwenye Baraza la Mawaziri, pamoja na kutolewa elimu kwanza na akasema kuwa katika maeneo mengine bomoabomoa si lazima.

  Alisema bomoabomoa hiyo ambayo imezua malalamiko imesimamishwa na Serikali kwa nia ya kujipanga upya, huku akisisitiza kuwa Serikali inamwamini Waziri Magufuli kama kiongozi mwenye uwezo na ilimpa nafasi hiyo ili pia aweze kuwabana makandarasi wazembe.

  Kasi hiyo ya Dk Magufuli imeyakumba majengo kadhaa ya Serikali, likiwapo la Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam na jengo la Makao Makuu ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco).

  Hata hivyo, baadhi ya wakazi wanaoishi kandokando ya Barabara ya Ubungo Maziwa hadi Kigogo, wamefungua kesi mahakamani kupinga kubomolewa bila fidia.

  JK akerwa na maofisa ardhi wala rushwa
  Jana akiwa katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, Rais Kikwete amewataka watendaji wake kuwachukulia hatua maofisa ardhi wanaojihusisha na vitendo vya rushwa akisema wamekuwa chanzo cha migogoro ya ardhi.
  "Wizara inatakiwa kuwachukulia hatua maofisa ardhi wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa huku wakidiriki kuuza maeneo ya wazi na kuwadhulumu wananchi.

  Hakuna kumwonea mtu huruma maana wananchi wanaonewa," alisema Rais Kikwete. Alisema hata malipo ya fidia yanatakiwa kuendana na hali halisi ya maisha na siyo kumhamisha mtu bila kumwandalia makazi ya kudumu.

  "Huwezi kumhamisha mtu bila kumwandalia makazi ya kudumu yanayoendana na hali ya maisha ya sasa, vinginevyo hakuna haja ya kumwondoa katika makazi yake.

  Tunatakiwa kutumia ubinadamu." Aliitaka Wizara kuorodhesha halmashauri zinazoongoza kwa migogoro ya ardhi ili kuona chanzo cha migogoro na kuwachukulia hatua maofisa wote wa ardhi wanaokiuka taratibu.Pia alilitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupunguza gharama za kodi kwenye nyumba zake na kuhakikisha majengo yao yanaboreshwa ili wanaopanga katika nyumba hizo waishi katika hali ya usafi.

  "Ukweli ni kwamba gharama zenu zinatisha mtu wa kawaida. Mwenye kipato cha chini hawezi kupanga nyumba zenu. Mnatakiwa kupunguza gharama hizo ili kuwawezesha wananchi kumudu gharama hizo vinginevyo wengi watazikimbia," alisema Rais Kikwete.
   
 2. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tusubiri Katibu Mkuu wa wizara aje kukanusha kwamba Magufuli hajaambiwa hivyo na rais!
   
 3. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kaaazi kwelikweli
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Duh kama kikwete amesema hivyo, Mungu ametukumbuka sasa Rais amezinduka kujenga nchni yake, Kikwete kaza kamba Baba, katika hili nakuunga mkono asilimia 100. Nitapaza sauti hadi mwisho upo sahihi sawia.

  Au Kikombe cha Babu kina ufanisi nini?
   
 5. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Vilaza wote hao JK tatua tatizo la umeme sio huu umburukenge unaofanya hivi sasa ati unatembelea wizara phew! What a thief ... .... .... kaa Magogoni ufanye kazi, kazi ya urais sio kuzurula kama mvuta bangi.
   
 6. E

  EMERALD Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Hii si maajabu sana, kwa kuwa wanaongeza tu news, ikipita hii ya magufuli utasikia mheshimiwa fulani atua kwa babu kukamata kikombe wanacheza na headlines tu kwa kweli.Inasikitisha sana kuona hao wamoja hawako na umoja na wakiulizwa lenye jibu moja wanatoa majibu tofauti.
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wanatuhamisha kwenye mambo ya msingi
   
 8. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watu wengine utadhani walizaliwa na CCM, na watakufa nayo!!!!!!!!!! Kama Pombe angekuwa yuko serious hii ni sababu tosha kujua kwamba CCM haimtaki-aondoke!!!!!!!!!!!. Tusishangae mkwere leo hii jioni akatangaza kuiidhinisha resignation ya pombe makufuli!!!!!!!!!!!! WanaJF tumkaribishe CDM kwenye chama cha watu waliomaanisha kumwondoa mkwere kwa nguvu ya umma, kama ile iliyomshghulikia na kumwondoa mubaraka wa misri!!!!!!!!!!!
   
 9. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Watu wavivu wa kufanya kazi huona wivu wenzo wanaposifika kwa kuchapa kazi, yaani huyu Rais mzima anamzuia waziri asifuate sheria! uuuuuwiiii TZ tumekwisha kabisa! kila mara majiuliza sijui, sijui ni wapi tulipokengeuka mwaka 2005 kumpa huyu bongolala Uongozi wa nchi hii, ameona watu wameshtuka ulaji wake wa pesa kupitia safari za nje, sasa anakula kwa mgongo wa ziara wizarani!
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Show ni jinsi gani mfumo wa uongozi ulivyobomoka. Aidha na JK na yeye anatafuta umaarufu kwa hizi public statements. na magufuli ameshakwisha kazi, kama angekuwa na nia ya kujiuzulu angeshajiuzu tangu siku ile Pinda alipompinda jimboni kwake
   
 11. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kama movie vile...... another episode plz........ at the end the truth will be revealed and resignation letter will be signed
   
 12. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,062
  Likes Received: 3,928
  Trophy Points: 280
  hata wakimwekea fitina, hata wafanye nini, kama nyota yake iko juu iko juu tu. hata kumweka wizara hiyo unajua walikuwa wanategemea atafanya vitu kama hivyo ili wananchi wamchukie kuondoa popularity yake kwaajili ya kumfunika tena mwaka 2015...we fikiria nyota ya jamaa inavyong'aa, hata baada ya kuagiza bomoabomoa, watu bado tu wanampenda ajabu...viongozi wa ccm wako tayari tukae kwenye miundombinu mibovu maisha yetu yote, barabara finyu na mafoleni kibao kwasababu wao wanapita na ving'ora...alimradi tu wanawapiga wananchi changa la macho wawapende..hap ivi na yeye anajaribu kutafuta kupendwa kwa wananchi....hivi hata mtoto mdogo anaweza kutumia strategy kama hiyo?nchi ikiongozwa na mkwere wote mnakuwa wakwera aisee....(mi mtani wao lakini hawa dagaa/njuka wa kikwere)..
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0


  nyie ndio msioeleweka

  one minute mnataka TRANSPARENCY

  next minute mnasema ohhh fanyeni SIRI

  you can be on both sides...chose a side kisha tujue moja

  mimi naonabora hivi hivi wazi wazi maana siri ndizo zimetufikisha pabaya
   
 14. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,062
  Likes Received: 3,928
  Trophy Points: 280
  kwahiyo na wewe unasapoti alichokifanya kikwete, kwasababu tu unadai alifanya kwa uwazi..wewe nawe mkwere wewe bila shaka...bomoa bomoa hii inatusaidia sana watz kwasababu itatengeneza miundombinu kwaajili ya kuharakisha maendeleo yetu sisi wenyewe, tutakaa hivihivi mpaka lini? umeridhika na miundo mbinu yetu hii ya tz iliyokaa kama mswahili aliyekunja miguu kubugia ubwabwa na pilau? dah..we wa mwaka arobaini na saba.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  mbona habari ninazozipata zinaonekana kuchanganya! wengine wanadokeza kuwa kasema aendelee na shughuli zake bila ya kuogopa
   
 16. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0

  Ninachosema SHERIA IFUATE MKONDO WAKE

  be it TANESCO UBUNGO au mabondeni

  sasa whats so wrong with kuachia sheria ifuate mkondo wake?

  maybe TOWN PLANNERS na TANROADS wanaweza kufikiria beyond 100 years next time
   
 17. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0

  Haya ndio mambo ya kuingiliwa na wanasiasa

  WAZIRI ANATOA ODERS as if yeye ndio sheria

  WAZIRI MKUU ana m rebuke kuwa atuleze ball

  WAZIRI ANAANDIKA BARUA YA KURESIGN (allegedly)

  RAIS anamwambia aaache kuwa mbabe (allegedly)

  Radi Mbao za JF zinakuambia ahhhh WHY IN THE PUBLIC

  Nadhani tatizo liko kwa waziri

  hana haja ya kutangaza mambo publicly yeye awawashie moto watendaji wake akiulizwa aseme wao wanafuata sheria thats it
   
 18. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Wakati wa kampeni alisema anataka flyover pale Ubungo....sasa magufulki anaanza kazi wanamzuia hiyo fyover itapita wapi? Huu msongamano utaisha kweli?
   
 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Magufuli asipo jiuzulu naye ana yataka. Maana ukidhalilishwa hivi na bado ukabaki inaonyesha ume kubali kutukanwa.
   
 20. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  vip mkuu ulikuwa kwenye danger ya kubomolewa
   
Loading...