Kuuza nyumba za nhc ni kuwatunuku wazembe, watoa rushwa na matapeli: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuuza nyumba za nhc ni kuwatunuku wazembe, watoa rushwa na matapeli:

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by akajasembamba, Dec 19, 2011.

 1. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii sera ya kuuza nyumba za NHC kwa wapangaji wake WA MUDA MREFU, kwa mtazamo wangu haina mantiki kabisa wala faida kwa Watanzania. Wapangaji wengi wa NHC nyumba wanazokaa wamezipata kwa rushwa, au waliopata kihalali miaka hiyoooo enzi za Mwalimu, walizembea kujenga za kwao siyo kwamba hawana uwezo, maana haiingii akilini nyumba ikaliwe na mtu mmoja kwa miaka 50 na asipate hata uwezo wa kujenga kibanda huko Mbagala Kiburugwa. Maisha ni kupanga na kuchagua ukitumia pesa zako kwa sherehe zisizo na msingi motto kazaliwa, kaota meno, kangÂ’oa meno, kaota chuchu, kaota ndevu, kitchen party,ndundu party, matokeo yake ndiyo hayo anakaa mjini miaka 50 ktk nyumba ya NHC, na kutumia hela kwa mavazi kila fashion inapingia. Hata hivyo pia wapangaji wengi mfano wa Magomeni kota siyo wale halisi bali wajukuu zao na Vilembwe vyao.Wale wa maeneo ya matajiri ya Uhindini wengi wana nyumba zao hadi tatu hadi nne hadi juzi juzi walikuwa wakilipa kodi ya shilingi elfu hamsini, wakati wana nyumba zao wamewapangisha wapangaji na wanawalipa Dola US $ hadi 2,000 kwa mwezi, lakini hawahami nyumba hizi za NHC wakisubiri wauziwe ili nao wauze kwa hela kubwa zaidi. Sielewi Serikali inakubali vipi kuwanufaisha watu wachache kwa kupanga kuwauzia kwa masharti nafuu wakati watu hao siyo waaminifu na ni wazembe. Wapangaji wa NHC ni wachache sana mno, kukipa ushindi chama kilichopo madarakani, serikali itapata kura za wapangaji wa NHC lakini itapoteza kura za watz wengine wenye kuonja machungu ya kulipa kodi kubwa na mikupuo ya mwaka mzima kwa Maland lords wasiolipa kodi yeyote ya mapato TRA. Kama siyo kuchochea vijana wanaoanza ajira zao kuingia katika rushwa,wizi na ukahaba ni nini? Kijana anayeanza kazi anapata wapi kodi ya kumlipa mwenye nyumba laki tatu kwa miezi 12 kwa mkupuo! Kwa nini nyumba za Serikali na Mashirika ya Umma ziuzwe uzwe kwa wingi, mbona za watu binafsi haziuzwi hivyo! Huu ujinga wa kusema mtu amekaa muda mrefu katika nyumba auziwe ni ugonjwa wa ajabu wa akili,huwezi ukakaa ktk nyumba ya mtu muda mrefu then umwambie baba au mama mwenye nyumba niuzie! Falsafa hii ni ile ile iliyotumika wakati wa Rais Mkapa kupora nyumba za Serikali zilizojengwa kwa jasho la watanzania maskini, sasa watu binafsi nao wanataka wapate mgao wao wa wizi wa mali za umma. Kama hoja ni kuinua mapato ya shirika, ilipaswa shirika liongeze kodi iendane na Market Price na siyo kuweka kiwango kodi nyumba nzima ambayo ni sawa na kodi ya chumba kimoja tu huko uswahilini. Baadhi ya nyumba wangewekewa vijana wanaoanza ajira wakae walau miaka isiyozidi sita wawapishe wenzao, ili wasitumie ajira zao kuiba kula rushwa wapate kodi za kulipa. UKWELI UNAUMA ILA LAZIMA USEMWE!
   
Loading...