Bollywood | Special Thread

Bollywood | Special Thread

Bollwood wanachofeli siku hizi ni kulazimisha kuzirudia filamu za zamani zilizowahi kufanya vyema. Au kuleta muendelezo wa zile filamu za zamani.
Mfano Gadar 2, Disco dancer nayo wanataka kuleta part two yake na filamu nyinginezo nyingi.
 
naona bado wameshindwa kupata script ya uhakika, Ila kwa hali inavyokwenda hizi spy films zao zinavyoboronga wataitilia mkazo
Dhoom haina haja ya muendelezo.

Ila Krrish ina haja kubwa ya muendelezo, Krrish 3 walizingua kimtindo , naipa 60%.
 
kuna mambo yanataka jicho la tatu kuyaona mkuu, Jamaa ana six years without Hit, Hata opening zake zimekuwa below standard kabisa. War 2 ilitakiwa lazima ianze na 50 cr + day one ndani ya Hindi belt. kuishia 28cr big time failure.
Nani anatoa hit ?

Ukitoa Gadar 2 na Pathan, filamu ipi angalau imepenya ?

Maa ya Kajol japo sijaiona sidhani kama nayo imetoboa.
 
kabisa jamaa wana loyal fans, War 2 day one south makusanyo yanakaribiana na ya original vision ya hindi, ni aibu sana Kwa Hrithik kama si fedheha kabisa.
Naona hata don 3 ina elekea kule kule, srk ali shituka hizi script za siku hizi ni hovyo.

race 3 nayo mbaya, sijui wao hawa oni hilo😂😂.
 
Back
Top Bottom