Bollen Ngetti: Utawala wa Rais Magufuli na hatima ya CCM

Zipo jamii huwa ni wazuri sana kwenye kazi za kutumia nguvu Na si za kutumia akili
 
tufanye Mbowe ni rais, zitto kabwe ni waziri mkuu, mbatia ni katibu mkuu kiongozi, lema waziri wa mambo ya ndani, tundu lissu ni mwanasheria mkuu wa serikali nk. baada ya miaka minne, tanzania itakua kama ulaya? watanzania tutakua na pesa mikononi? wote tutaishi maghorofani? ni nini unadhani watafanya? mnadhani shida ya tanzania ni rais? mnafikiri wapo watu special wa kuwapa utajiri? mnajidanganya na mnapoteza muda........
Baba bora utoa muongozo Na njia sahihi ya mafanikio ya familia yake
 
Ikiwa mikono yako imelowa damu ni ngumu sana kufanikiwa hata ukiingia kwenye Shamba lenye rutuba mazao yaliyostawi yatanyauka.Epuka sana kulowa damu,damu ni uhai damu ni maagano.Kupitia damu unamuona Muumbaji nae hasira zake hazitokwisha juu yako.
 
Ninajuta kumpigia kura yangu kama ningejua haya yatakuja kutokea nisinge mpigia kura yangu mm kwali leo nashindia mlo mmoja nakaa nyumbani wiki nzima sina kazi mm nifundi ujezi matajiri hawajengi hawakarabati.
Kikombe tulikijua Kwa nje,ukitaka kujua tabia halisi ya Mke Mme ishi nae kwanza.
 
TUMEFIKA mahali ambapo tuweke kando itikadi ya vyama, dini na ubaguzi mwingine wowote tujadili na kutafakari kwa pamoja hatima ya nchi yetu na watu wake! Jamii inayojadiliana masuala ya Taifa ndiyo inaitwa jamii hai. Kinyume na hapo hiyo ni jamii mfu!

Tunahitaji watu wa kada zote kujitokeza hadharani kushiriki mjadala huu ambao mimi ni mchokoza mada tu na ninyi ndio wazungumzaji. Wasomi, wasiosoma, matajiri kwa masikini, wanadini kwa wapagani, wanafunzi, kina dada, vijana, wazee nakadhalika. Sambaza mjadala huu hadi mashambani kwa wenye simu ya vitochi na vibatari.

Swali la msingi tunalotakiwa kujiuliza ni hili: Kwa nini Rais John Magufuli apigiwe tena kura 2020 kuendelea na Urais Ikulu badala ya kurudi kijijini Chato?

Nini hasa yalikuwa matumaini ya Watanzania kwa uongozi wa Rais Magufuli 2015/20? Je, hayo matumaini yamefikiwa? Kwa kiasi na namna gani? Kama hayakufikiwa kwa nini asijiweke kando 2020 badala ya kuendekeza, "ni utamaduni wetu".

Rais Magufuli alipokea kijiti kwa Jakaya nchi ikiwa na changamoto nyingi. Moja ya changamoto ilikuwa ni CCM kuchokwa kwa kiwango kikubwa sana kutokana na matendo ya rushwa na ufisadi uliokithiri! Ilikuwa ni fedheha kusikia watu wakisema hadharani kuwa akisimamishwa mgombea na CCM na kinyesi cha ngurue watapigia kura kinyesi cha ngurue! Hii ilikuwa ni uasi mkubwa wa kijamii kwa chama changu!

Sote tunajua kuwa kulifanyika kazi ya ziada kumfanya Magufuli kushinda hata kwa bao la makalio! Alishinda!

Swali tunalojiuliza je, yale yaliyofanya watu wawe radhi kupigia kura kinyesi cha ngurue yametoka? Yamepungua kwa kiasi gani? Ni lazima tujiulize maswali haya maana tuliingia mkataba na Magufuli kutuvusha kwa miaka 5 na kama amekiuka mkataba tunamkataa kwa miaka mingine 5. Hili si la kuonea haya na tueleweke hivyo duniani!

Tukianza na suala la uchumi. Tunaimbiwa injili kuwa uchumi wetu unakuwa kwa 7% lakini ukitazama maisha halisi ya watu hasa wa maisha ya chini sasa ni dhalili kama vitoto vya mbwa koko. Watu sasa hawana uhakika wa kupata hata mlo mmoja. Maisha Yao yamekuwa magumu mara dufu!

Nimefanya utafiti. Biashara nyingi ndogo na kubwa zimefungwa maana hata wateja wa kununua bidhaa feki nao hawapo tena. Mzunguko wa fedha umekuwa mdogo sana! Je, Rais Magufuli tulikubaliana kufikia hali hii? Ni uchumi upi huo unaokuwa kama wananchi hawawezi kumudu milo miwili kwa siku? Huo ni uchumi wa makaratasi!

Rais Magufuli amebadili mifumo ya kifedha ambapo sasa benki za kibiashara hazina fedha kwa hoja mbilikimo na lemavu eti zilitumika kupiga dili. Zinafungwa! Maduka ya kuuza fedha zinafungwa. Je, hili lilikuwa kwenye mkataba wa kuingia Ikulu 2015?

Tunaambiwa kuwa fedha zinapelekwa kwenye miradi mikubwa ya kiuchumi kama ujenzi wa SGR, Stirgler Gorge, ununuzi wa ndege za kisasa, elimu bila malipo, nakadhalika. Kuhamia Dodoma inayoswaga mabilioni ya walipakodi. Ukweli ni kwamba tumeamua kutumia fedha kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu badala ya watu tofauti kabisa na falsafa ya Nyerere kuhusu maendeleo tunayedai kuvaa viatu vyake!

Inaelezwa kuwa awamu hii imevunja rekodi kwa ufisadi kwa mujibu wa ripoti ya CAG 2017/18 iliyokataliwa na Ndugai. Kila unaposoma Kuna wizi basi ni mabilioni. Ni awamu ambayo sheria ya fedha na ununuzi umekanyagwa na kutemewa mate haijawahi kutokea. Hadi Leo 2.4 Trilioni haijatolewa ufafanuzi na uchambuzi jambo linaloacha mashaka makubwa. Je, tulikubaliana kwenye mkataba (Ilani) kuwa fedha zitatumika bila idhini ya Bunge? Wananchi wanauliza hawajibiwi. Watu Wako kimya.

Wakati hayo yakiendelea kikundi kidogo kinatajirika hadi kulewa fedha na madaraka. Huku gavana wa Mbeya akidai kuwa na fedha hadi za kuhonga michepuko, mwingine Dar anasema magari ya IST ni ya kuhonga watu. Kiburi, jeuri na kiburi kilichovuka mawingu. Unyenyekevu umewatoroka viongozi wetu lakini mteuzi wao kimya. Hii ilikuwepo kwenye mkataba? Hapana!

Baada tu ya kuingia madarakani zoezi la uhakiki wa silaha lilifanyika ili silaha zibaki mikononi mwa watu salama. Kwa hakika hili tunapongeza maana uhalifu ulioshamiri kipindi cha Jakaya umepungua mno. Ni matukio machache lakini unashangaa matukio ya ujambazi yamekuwa replaced na matukio ya watu kutekwa, kuteswa, kupotea na wengine kuokotwa ndani ya viroba. Kwamba tumewashinda majambazi lakini watu wasiojulikana ni mashujaa. Hadi Leo waliomshambulia Lissu kama mnyama hawajulikani. Ilani ilisema hatutawasaka wasiojulikana? Hapana!

Demokrasia imezidi kusinyaa: magazeti yamefungiwa, wapinzani hawaongei, mitandao imetungiwa sheria kandamizi, wakosoaji Wako hatarini kumalizwa, hofu imetamalaki, uandishi wa habari za uchunguzi umetoweka kwa hofu, Bunge gizani ni. Kwa nini hatukuwaambia wananchi kabla ya kuingia nao mkataba wa utawala ili waamue?

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ni muhimu kama chama tukatolea ufafanuzi kwa wananchi kabla ya kuingia kwenye mkataba mwingine na Rais Magufuli 2020/25. Uchambuzi wa kina ufanyike na wataalamu wa Sera na Mipango ili isaidie umma mpana kufanya maamuzi sahihi na makini maana bila kufanya hivyo ninawaambia wana CCM hatutaweza upepo wa Tundu Lissu. Kumzuia asiingie Ikulu kwa kura itakuwa ni sawa na kufunika jua kwa kaniki. Tuwaeleze wananchi kwa nini haya mateso hatukuwaeleza 2020? Kwa nini tulifanya siri?

Tujadiliane kwa hoja kama huwezi piga kimya jifunze kwa wengine. Karibuni waheshimiwa, mjadala umefunguliwa.
#AchaWoga2020

###HIMOUT##JIWEOUT###NCHI IME STALK HAKUNA KINACHOENDA NA WENYEWE WANAJITETEA ETI KWA KISINGIZIO TUNASAFISHA NCHI.DA.
 
Magufuli John, hatuna saba ya kutomchaguwa 2020 - ukiwa kiongozi lawama lazima zilingane na pongezi - siku zote CDM hamuwezi kuwa upande wa Serikali ya CCM

Tutamchaguwa na atashinda kwa KISHINDO 2020.

Msakila KABENDE
CCM Kwanza 2019
 
Magu anakubalika sasa kuliko alivyoingia, ccm ina wafiasi wengi sasa kuliko zaman, unaangalia ukuaji wa ichumi kwa tafsiri ya layman kwamba uchumi unakuwa mkubwa pale tu watu wakiwa na mihelamingi mfukoni. Zimbabwe watu wana hela hadi wanabebea kweny mikokoteni, ila uchimi upo hoi. Marekani ni nchi ya uchimi mkubwa sana ila maishaya raia magimu balaa. Ukilemaa utakufa njaa hawama time na ww
 
JPM chuma mtanena tu kwa lugha raisi wetu kaza buti kila mtu ale kwa juhudi zake
walio zoea vya ubwete kila siku maandiko tu
humu sisi tulio zoea mihongo tena mlo mmoja tunapiga kazi tu huku vijijini kwetu
kwanza magufuri tunatamani hata angeongezewa mhura ata iwe mitatu
 
Magufuli John, hatuna saba ya kutomchaguwa 2020 - ukiwa kiongozi lawama lazima zilingane na pongezi - siku zote CDM hamuwezi kuwa upande wa Serikali ya CCM

Tutamchaguwa na atashinda kwa KISHINDO 2020.

Msakila KABENDE
CCM Kwanza 2019

lini mmewahi kushinda bila polisi na tume ya uchaguzi?unajitekenya halfu unacheka mwenyewe
 
Mara nyingi hatujiukizi WHAT HAPPENED, mie si msifu kikwete ila namlaumu sana tena sana.

Jiulizeni , kwa nini Nape anaandamwa, au kwa nini kinana kabla na baada ya uchaguzi, alingangania anastaafu, na kwa nini timu yote ya uongozi wake wakati ule unaandamwa?

Tukiyajua hayo ndio tuyajua mengi yanayo tokea leo.
 
[QUOTE="selase, post: 31712280, member: 517610"lini mmewahi kushinda bila polisi na tume ya uchaguzi?unajitekenya halfu unacheka mwenyewe[/QUOTE]

Hizo ni hisia zenu, police wapo kulinda usalama wa wapiga kura na wasimamizi - tusiwatwishe zigo la lawama
 
[emoji1436]‍♂️[emoji1436]‍♂️[emoji1436]‍♂️[emoji1436]‍♂️
 
Mkuu umeongea vyema.

Tafiti zifanywe, majibu yatolewe na maamuzi yaachwe kwa wananchi.

Lakini je? Umeshawahi kujiuliza ni miradi mingapi ambayo Mh. JPM ameianzisha ambapo kwa uwepo wake tu ndio itaweza kustahimili na kukamilika kwa wakati...

Miradi na sera nyingi zimepotea kutokana na mtawala kumaliza muda wake rejea kilimo kwanza, kipindi cha JMK ambapo alikuwa na malengo mazuri na endelevu kuhusiana na kilimo lakini jiulize tu hivi leo ni nani anaekitazama kilimo kama sekta muhimu nchini.

Mi naona ingekuwepo na kitu kama Succession plan ya nchi yaani mtu ambae ataingia au atapewa madaraka anarithishwa matakwa na mitazamo pamoja na malengo ya wananchi na kupaswa kuyaendeleza pale alipoishia aliemtangulia na sio kufanya atakavyo yeye.

Chuwa. K. M
Hujui kama jiwe hapangiwi??? hujui kama alienda kuchukua form akiwa peke yake?? sifa hizo mbili zinathibitisha kuwa hata kama Succession plan ya nchi ingekuwepo, bado kama nchi hatuwezi kuwa na malengo endelevu.
 
TUMEFIKA mahali ambapo tuweke kando itikadi ya vyama, dini na ubaguzi mwingine wowote tujadili na kutafakari kwa pamoja hatima ya nchi yetu na watu wake! Jamii inayojadiliana masuala ya Taifa ndiyo inaitwa jamii hai. Kinyume na hapo hiyo ni jamii mfu!

Tunahitaji watu wa kada zote kujitokeza hadharani kushiriki mjadala huu ambao mimi ni mchokoza mada tu na ninyi ndio wazungumzaji. Wasomi, wasiosoma, matajiri kwa masikini, wanadini kwa wapagani, wanafunzi, kina dada, vijana, wazee nakadhalika. Sambaza mjadala huu hadi mashambani kwa wenye simu ya vitochi na vibatari.

Swali la msingi tunalotakiwa kujiuliza ni hili: Kwa nini Rais John Magufuli apigiwe tena kura 2020 kuendelea na Urais Ikulu badala ya kurudi kijijini Chato?

Nini hasa yalikuwa matumaini ya Watanzania kwa uongozi wa Rais Magufuli 2015/20? Je, hayo matumaini yamefikiwa? Kwa kiasi na namna gani? Kama hayakufikiwa kwa nini asijiweke kando 2020 badala ya kuendekeza, "ni utamaduni wetu".

Rais Magufuli alipokea kijiti kwa Jakaya nchi ikiwa na changamoto nyingi. Moja ya changamoto ilikuwa ni CCM kuchokwa kwa kiwango kikubwa sana kutokana na matendo ya rushwa na ufisadi uliokithiri! Ilikuwa ni fedheha kusikia watu wakisema hadharani kuwa akisimamishwa mgombea na CCM na kinyesi cha ngurue watapigia kura kinyesi cha ngurue! Hii ilikuwa ni uasi mkubwa wa kijamii kwa chama changu!

Sote tunajua kuwa kulifanyika kazi ya ziada kumfanya Magufuli kushinda hata kwa bao la makalio! Alishinda!

Swali tunalojiuliza je, yale yaliyofanya watu wawe radhi kupigia kura kinyesi cha ngurue yametoka? Yamepungua kwa kiasi gani? Ni lazima tujiulize maswali haya maana tuliingia mkataba na Magufuli kutuvusha kwa miaka 5 na kama amekiuka mkataba tunamkataa kwa miaka mingine 5. Hili si la kuonea haya na tueleweke hivyo duniani!

Tukianza na suala la uchumi. Tunaimbiwa injili kuwa uchumi wetu unakuwa kwa 7% lakini ukitazama maisha halisi ya watu hasa wa maisha ya chini sasa ni dhalili kama vitoto vya mbwa koko. Watu sasa hawana uhakika wa kupata hata mlo mmoja. Maisha Yao yamekuwa magumu mara dufu!

Nimefanya utafiti. Biashara nyingi ndogo na kubwa zimefungwa maana hata wateja wa kununua bidhaa feki nao hawapo tena. Mzunguko wa fedha umekuwa mdogo sana! Je, Rais Magufuli tulikubaliana kufikia hali hii? Ni uchumi upi huo unaokuwa kama wananchi hawawezi kumudu milo miwili kwa siku? Huo ni uchumi wa makaratasi!

Rais Magufuli amebadili mifumo ya kifedha ambapo sasa benki za kibiashara hazina fedha kwa hoja mbilikimo na lemavu eti zilitumika kupiga dili. Zinafungwa! Maduka ya kuuza fedha zinafungwa. Je, hili lilikuwa kwenye mkataba wa kuingia Ikulu 2015?

Tunaambiwa kuwa fedha zinapelekwa kwenye miradi mikubwa ya kiuchumi kama ujenzi wa SGR, Stirgler Gorge, ununuzi wa ndege za kisasa, elimu bila malipo, nakadhalika. Kuhamia Dodoma inayoswaga mabilioni ya walipakodi. Ukweli ni kwamba tumeamua kutumia fedha kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu badala ya watu tofauti kabisa na falsafa ya Nyerere kuhusu maendeleo tunayedai kuvaa viatu vyake!

Inaelezwa kuwa awamu hii imevunja rekodi kwa ufisadi kwa mujibu wa ripoti ya CAG 2017/18 iliyokataliwa na Ndugai. Kila unaposoma Kuna wizi basi ni mabilioni. Ni awamu ambayo sheria ya fedha na ununuzi umekanyagwa na kutemewa mate haijawahi kutokea. Hadi Leo 2.4 Trilioni haijatolewa ufafanuzi na uchambuzi jambo linaloacha mashaka makubwa. Je, tulikubaliana kwenye mkataba (Ilani) kuwa fedha zitatumika bila idhini ya Bunge? Wananchi wanauliza hawajibiwi. Watu Wako kimya.

Wakati hayo yakiendelea kikundi kidogo kinatajirika hadi kulewa fedha na madaraka. Huku gavana wa Mbeya akidai kuwa na fedha hadi za kuhonga michepuko, mwingine Dar anasema magari ya IST ni ya kuhonga watu. Kiburi, jeuri na kiburi kilichovuka mawingu. Unyenyekevu umewatoroka viongozi wetu lakini mteuzi wao kimya. Hii ilikuwepo kwenye mkataba? Hapana!

Baada tu ya kuingia madarakani zoezi la uhakiki wa silaha lilifanyika ili silaha zibaki mikononi mwa watu salama. Kwa hakika hili tunapongeza maana uhalifu ulioshamiri kipindi cha Jakaya umepungua mno. Ni matukio machache lakini unashangaa matukio ya ujambazi yamekuwa replaced na matukio ya watu kutekwa, kuteswa, kupotea na wengine kuokotwa ndani ya viroba. Kwamba tumewashinda majambazi lakini watu wasiojulikana ni mashujaa. Hadi Leo waliomshambulia Lissu kama mnyama hawajulikani. Ilani ilisema hatutawasaka wasiojulikana? Hapana!

Demokrasia imezidi kusinyaa: magazeti yamefungiwa, wapinzani hawaongei, mitandao imetungiwa sheria kandamizi, wakosoaji Wako hatarini kumalizwa, hofu imetamalaki, uandishi wa habari za uchunguzi umetoweka kwa hofu, Bunge gizani ni. Kwa nini hatukuwaambia wananchi kabla ya kuingia nao mkataba wa utawala ili waamue?

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ni muhimu kama chama tukatolea ufafanuzi kwa wananchi kabla ya kuingia kwenye mkataba mwingine na Rais Magufuli 2020/25. Uchambuzi wa kina ufanyike na wataalamu wa Sera na Mipango ili isaidie umma mpana kufanya maamuzi sahihi na makini maana bila kufanya hivyo ninawaambia wana CCM hatutaweza upepo wa Tundu Lissu. Kumzuia asiingie Ikulu kwa kura itakuwa ni sawa na kufunika jua kwa kaniki. Tuwaeleze wananchi kwa nini haya mateso hatukuwaeleza 2020? Kwa nini tulifanya siri?

Tujadiliane kwa hoja kama huwezi piga kimya jifunze kwa wengine. Karibuni waheshimiwa, mjadala umefunguliwa.
#AchaWoga2020

umeonge utumbo tena utumbo wa nguruwe
 
Ninajuta kumpigia kura yangu kama ningejua haya yatakuja kutokea nisinge mpigia kura yangu mm kwali leo nashindia mlo mmoja nakaa nyumbani wiki nzima sina kazi mm nifundi ujezi matajiri hawajengi hawakarabati.

Sasa Kama Katiba mpya haipo, tume huru ya uchaguzi haipo.... Mabadiliko kupitia sanduku la kupigia kura Ni ndoto za mchana.
 
Back
Top Bottom