Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
TUMEFIKA mahali ambapo tuweke kando itikadi ya vyama, dini na ubaguzi mwingine wowote tujadili na kutafakari kwa pamoja hatima ya nchi yetu na watu wake! Jamii inayojadiliana masuala ya Taifa ndiyo inaitwa jamii hai. Kinyume na hapo hiyo ni jamii mfu!
Tunahitaji watu wa kada zote kujitokeza hadharani kushiriki mjadala huu ambao mimi ni mchokoza mada tu na ninyi ndio wazungumzaji. Wasomi, wasiosoma, matajiri kwa masikini, wanadini kwa wapagani, wanafunzi, kina dada, vijana, wazee nakadhalika. Sambaza mjadala huu hadi mashambani kwa wenye simu ya vitochi na vibatari.
Swali la msingi tunalotakiwa kujiuliza ni hili: Kwa nini Rais John Magufuli apigiwe tena kura 2020 kuendelea na Urais Ikulu badala ya kurudi kijijini Chato?
Nini hasa yalikuwa matumaini ya Watanzania kwa uongozi wa Rais Magufuli 2015/20? Je, hayo matumaini yamefikiwa? Kwa kiasi na namna gani? Kama hayakufikiwa kwa nini asijiweke kando 2020 badala ya kuendekeza, "ni utamaduni wetu".
Rais Magufuli alipokea kijiti kwa Jakaya nchi ikiwa na changamoto nyingi. Moja ya changamoto ilikuwa ni CCM kuchokwa kwa kiwango kikubwa sana kutokana na matendo ya rushwa na ufisadi uliokithiri! Ilikuwa ni fedheha kusikia watu wakisema hadharani kuwa akisimamishwa mgombea na CCM na kinyesi cha ngurue watapigia kura kinyesi cha ngurue! Hii ilikuwa ni uasi mkubwa wa kijamii kwa chama changu!
Sote tunajua kuwa kulifanyika kazi ya ziada kumfanya Magufuli kushinda hata kwa bao la makalio! Alishinda!
Swali tunalojiuliza je, yale yaliyofanya watu wawe radhi kupigia kura kinyesi cha ngurue yametoka? Yamepungua kwa kiasi gani? Ni lazima tujiulize maswali haya maana tuliingia mkataba na Magufuli kutuvusha kwa miaka 5 na kama amekiuka mkataba tunamkataa kwa miaka mingine 5. Hili si la kuonea haya na tueleweke hivyo duniani!
Tukianza na suala la uchumi. Tunaimbiwa injili kuwa uchumi wetu unakuwa kwa 7% lakini ukitazama maisha halisi ya watu hasa wa maisha ya chini sasa ni dhalili kama vitoto vya mbwa koko. Watu sasa hawana uhakika wa kupata hata mlo mmoja. Maisha Yao yamekuwa magumu mara dufu!
Nimefanya utafiti. Biashara nyingi ndogo na kubwa zimefungwa maana hata wateja wa kununua bidhaa feki nao hawapo tena. Mzunguko wa fedha umekuwa mdogo sana! Je, Rais Magufuli tulikubaliana kufikia hali hii? Ni uchumi upi huo unaokuwa kama wananchi hawawezi kumudu milo miwili kwa siku? Huo ni uchumi wa makaratasi!
Rais Magufuli amebadili mifumo ya kifedha ambapo sasa benki za kibiashara hazina fedha kwa hoja mbilikimo na lemavu eti zilitumika kupiga dili. Zinafungwa! Maduka ya kuuza fedha zinafungwa. Je, hili lilikuwa kwenye mkataba wa kuingia Ikulu 2015?
Tunaambiwa kuwa fedha zinapelekwa kwenye miradi mikubwa ya kiuchumi kama ujenzi wa SGR, Stirgler Gorge, ununuzi wa ndege za kisasa, elimu bila malipo, nakadhalika. Kuhamia Dodoma inayoswaga mabilioni ya walipakodi. Ukweli ni kwamba tumeamua kutumia fedha kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu badala ya watu tofauti kabisa na falsafa ya Nyerere kuhusu maendeleo tunayedai kuvaa viatu vyake!
Inaelezwa kuwa awamu hii imevunja rekodi kwa ufisadi kwa mujibu wa ripoti ya CAG 2017/18 iliyokataliwa na Ndugai. Kila unaposoma Kuna wizi basi ni mabilioni. Ni awamu ambayo sheria ya fedha na ununuzi umekanyagwa na kutemewa mate haijawahi kutokea. Hadi Leo 2.4 Trilioni haijatolewa ufafanuzi na uchambuzi jambo linaloacha mashaka makubwa. Je, tulikubaliana kwenye mkataba (Ilani) kuwa fedha zitatumika bila idhini ya Bunge? Wananchi wanauliza hawajibiwi. Watu Wako kimya.
Wakati hayo yakiendelea kikundi kidogo kinatajirika hadi kulewa fedha na madaraka. Huku gavana wa Mbeya akidai kuwa na fedha hadi za kuhonga michepuko, mwingine Dar anasema magari ya IST ni ya kuhonga watu. Kiburi, jeuri na kiburi kilichovuka mawingu. Unyenyekevu umewatoroka viongozi wetu lakini mteuzi wao kimya. Hii ilikuwepo kwenye mkataba? Hapana!
Baada tu ya kuingia madarakani zoezi la uhakiki wa silaha lilifanyika ili silaha zibaki mikononi mwa watu salama. Kwa hakika hili tunapongeza maana uhalifu ulioshamiri kipindi cha Jakaya umepungua mno. Ni matukio machache lakini unashangaa matukio ya ujambazi yamekuwa replaced na matukio ya watu kutekwa, kuteswa, kupotea na wengine kuokotwa ndani ya viroba. Kwamba tumewashinda majambazi lakini watu wasiojulikana ni mashujaa. Hadi Leo waliomshambulia Lissu kama mnyama hawajulikani. Ilani ilisema hatutawasaka wasiojulikana? Hapana!
Demokrasia imezidi kusinyaa: magazeti yamefungiwa, wapinzani hawaongei, mitandao imetungiwa sheria kandamizi, wakosoaji Wako hatarini kumalizwa, hofu imetamalaki, uandishi wa habari za uchunguzi umetoweka kwa hofu, Bunge gizani ni. Kwa nini hatukuwaambia wananchi kabla ya kuingia nao mkataba wa utawala ili waamue?
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ni muhimu kama chama tukatolea ufafanuzi kwa wananchi kabla ya kuingia kwenye mkataba mwingine na Rais Magufuli 2020/25. Uchambuzi wa kina ufanyike na wataalamu wa Sera na Mipango ili isaidie umma mpana kufanya maamuzi sahihi na makini maana bila kufanya hivyo ninawaambia wana CCM hatutaweza upepo wa Tundu Lissu. Kumzuia asiingie Ikulu kwa kura itakuwa ni sawa na kufunika jua kwa kaniki. Tuwaeleze wananchi kwa nini haya mateso hatukuwaeleza 2020? Kwa nini tulifanya siri?
Tujadiliane kwa hoja kama huwezi piga kimya jifunze kwa wengine. Karibuni waheshimiwa, mjadala umefunguliwa.
#AchaWoga2020