Bollen Ngetti: Utawala wa Rais Magufuli na hatima ya CCM

Bollen Ngetti: Utawala wa Rais Magufuli na hatima ya CCM

Hebu tumpe muda, tuone kama Stiegler gorge na SGR zitakamilika bila nchi kuwa muflis. Hakika kama tutafilisika, austerty measures ambazo tutashauriwa kuchukuwa na WB pamoja IMF hapo baadae ni pamoja na ku lay off zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa serikali waliopo kwenye ajira hivi sasa.
 
Kama unaishi Dar kwenye minara ya 4g utajuaje kwamba kuna lishe duni kwa watanzania wengine? Maana habari unazofuatilia ni za vigodoro na porn site kwenye internet.


Asante sana ningekuwa karibu yako aisee Eid ningekuchinjia jogoo kabisa
 
Kwenye uchaguzi
Mimi naunga mkono rushwa na ufisadi
Kuwa fisadi kwa maslahi ya familia yako na watoto wako kuna kosa gani?

Kutoa rushwa ili biashara zako na kazi ziwe safi kuna kosa gani?

Kila mtu ana matatizo yake, Mbona kuna marais malaya na makahaba Wengine maahoga ulaya ila Uchumi upo juu

Mkuu, Hatujawahi Tanzania kuingia mkataba na Rais wa nchi

Nchi hii hakuna muongozo wa dira na malengo, Wewe umeyatoa wapi hayo makubaliano kisheria?

Katiba imempa Rais mamlaka ya kufanya atakalo, Wewe ni nani mpaka umpangie unachofikiria?

Kila ulaji na kundi Lake na zama zake kundi la escrow lipo segerea

Sasa ni muda wa Rais wa Dar salaama na watu wake

Mamlaka ya kuhoji umeyatoa wapi? Ni nani aliyekupa mamlaka ya kubuni mikataba hewa

Hatuna mkataba na Rais sisi, Hiyo katiba yako nina mashaka nayo

Ebu pitia manunuzi ya ndege na kuhamia dodoma Haya ndio malengo yake na mkataba na ccm yake

Wewe si Raia tu uliekatwa mkia na Huna nguvu kisheria

Iddi njema kaka, Kumbuka njaa inauma
 
Bangi
Mara nyingi ukiwa huna busara unaweza kufikiri watu wote ni wajinga kama wewe. Mwache JPM atende kazi kwa manufaa ya nchi na watanzania. Hakika atakumbukwa hadi kizazi cha tano. Watanzania wengi wenye uchungu na nchi, wanampa Big Up Sana. Pia, CCM itaendelea kuwepo na kutawala. Tanzania Kwanza.
 
Hebu tumpe muda, tuone kama Stiegler gorge na SGR zitakamilika bila nchi kuwa muflis. Hakika kama tutafilisika, austerty measures ambazo tutashauriwa kuchukuwa na WB pamoja IMF hapo baadae ni pamoja na ku lay off zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa serikali waliopo kwenye ajira hivi sasa.
Huo muda unaompa si siku. Miaka na mamlaka. Gharama yake ukiipima si ndogo.
 
Matatizo ya watanzania yataondoka siku tukiacha kushabikia siasa kama mpira.
Hapo ndo tutakuwa na uwezo wa kuondoa vyama na viongozi wasiotufaa.
Ila kwa sasa ni tabu tupu.
 
CCM inaweza ikampitisha tena mwaka 2020, Sio kwakuwa wanampenda la hasha, lakini kama chama dhaifu kinamhitaji goliath wa kukilinda hata kwa uovu
 
Jiwe kaja kuharibu kila kitu kwenye nchi yetu,mijitu mijinga mipumbavu isiyojielewa inazidi kumshangilia kila siku binafsi sijawahi mkubali huyu magufuli ni zee la ovyo sana
 
Jiwe kaja kuharibu kila kitu kwenye nchi yetu,mijitu mijinga mipumbavu isiyojielewa inazidi kumshangilia kila siku binafsi sijawahi mkubali huyu magufuli ni zee la ovyo sana
Dah...kaja kuharibu nini? Hiyo mirija yenu iliyokatwa? [emoji2960][emoji23][emoji23][emoji23]
 
uhalisia unabaki pale pale( hali ni ngumu sana kila kona) ,lakini bado tunalazimishwa kusifu viongozi ...
 
Ndo kauli zenu hizi za kifala kila siku mirija mirija ,kaja kuharibu uchumi,soko la ajira,kaleta watu wasiojulikana na madhambi kibao
Dah...kaja kuharibu nini? Hiyo mirija yenu iliyokatwa? [emoji2960][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tatizo letu tunamsifu mtu badala ya kuangalia wapi tumefikia au tumekwama katika mipango yetu. Mpango si wa mtu bali wa watu.
CCM inaweza ikampitisha tena mwaka 2020, Sio kwakuwa wanampenda la hasha, lakini kama chama dhaifu kinamhitaji goliath wa kukilinda hata kwa uovu
 
Unamaanisha mini 'Hawajajiandaa kuongoza nchi'.Fafanua.Hili jambo limekuwa likirudiwa mara kadhaa na wasioamini katika vyama vya upinzani Tanzania.Mifumo ilishawekwa ,watashindwa vipi?
Sawa nakubaliana na wewe lakini sasa ujue hata wawekezaji wanaogopa sana kutia mguu TZ ila cha kushangaza hujagusia hiyo, pili hata wale wabadala hawajajiandaa kisawasawa kuongoza nchi wapo kwenye issues ndogo ndogo tu
 
Mh. Peter Msigwa afanya uchambuzi wa maamuzi ya serikali ya CCM bungeni kuhusu soko la korosho, kikokotoo, kutofanya kazi na CAG, SGR , Kuhamia Dodoma, Stiegler's Gorge, sheria ya Takwimu, Kodi , Wawekezaji kukimbia, hakuna Demokrasia ,Muswada wa Vyombo vya Habari. ...... na madhara ya maamuzi hayo kwa nchi na wananchi wanyonge

Source : Chadema media TV
 
Na Bollen Ngetti

TUMEFIKA mahali ambapo tuweke kando itikadi ya vyama, dini na ubaguzi mwingine wowote tujadili na kutafakari kwa pamoja hatima ya nchi yetu na watu wake! Jamii inayojadiliana masuala ya Taifa ndiyo inaitwa jamii hai. Kinyume na hapo hiyo ni jamii mfu!

Tunahitaji watu wa kada zote kujitokeza hadharani kushiriki mjadala huu ambao mimi ni mchokoza mada tu na ninyi ndio wazungumzaji. Wasomi, wasiosoma, matajiri kwa masikini, wanadini kwa wapagani, wanafunzi, kina dada, vijana, wazee nakadhalika. Sambaza mjadala huu hadi mashambani kwa wenye simu ya vitochi na vibatari.

Swali la msingi tunalotakiwa kujiuliza ni hili: Kwa nini Rais John Magufuli apigiwe tena kura 2020 kuendelea na Urais Ikulu badala ya kurudi kijijini Chato?

Nini hasa yalikuwa matumaini ya Watanzania kwa uongozi wa Rais Magufuli 2015/20? Je, hayo matumaini yamefikiwa? Kwa kiasi na namna gani? Kama hayakufikiwa kwa nini asijiweke kando 2020 badala ya kuendekeza, "ni utamaduni wetu".

Rais Magufuli alipokea kijiti kwa Jakaya nchi ikiwa na changamoto nyingi. Moja ya changamoto ilikuwa ni CCM kuchokwa kwa kiwango kikubwa sana kutokana na matendo ya rushwa na ufisadi uliokithiri! Ilikuwa ni fedheha kusikia watu wakisema hadharani kuwa akisimamishwa mgombea na CCM na kinyesi cha ngurue watapigia kura kinyesi cha ngurue! Hii ilikuwa ni uasi mkubwa wa kijamii kwa chama changu!

Sote tunajua kuwa kulifanyika kazi ya ziada kumfanya Magufuli kushinda hata kwa bao la makalio! Alishinda!

Swali tunalojiuliza je, yale yaliyofanya watu wawe radhi kupigia kura kinyesi cha ngurue yametoka? Yamepungua kwa kiasi gani? Ni lazima tujiulize maswali haya maana tuliingia mkataba na Magufuli kutuvusha kwa miaka 5 na kama amekiuka mkataba tunamkataa kwa miaka mingine 5. Hili si la kuonea haya na tueleweke hivyo duniani!

Tukianza na suala la uchumi. Tunaimbiwa injili kuwa uchumi wetu unakuwa kwa 7% lakini ukitazama maisha halisi ya watu hasa wa maisha ya chini sasa ni dhalili kama vitoto vya mbwa koko. Watu sasa hawana uhakika wa kupata hata mlo mmoja. Maisha Yao yamekuwa magumu mara dufu!

Nimefanya utafiti. Biashara nyingi ndogo na kubwa zimefungwa maana hata wateja wa kununua bidhaa feki nao hawapo tena. Mzunguko wa fedha umekuwa mdogo sana! Je, Rais Magufuli tulikubaliana kufikia hali hii? Ni uchumi upi huo unaokuwa kama wananchi hawawezi kumudu milo miwili kwa siku? Huo ni uchumi wa makaratasi!

Rais Magufuli amebadili mifumo ya kifedha ambapo sasa benki za kibiashara hazina fedha kwa hoja mbilikimo na lemavu eti zilitumika kupiga dili. Zinafungwa! Maduka ya kuuza fedha zinafungwa. Je, hili lilikuwa kwenye mkataba wa kuingia Ikulu 2015?

Tunaambiwa kuwa fedha zinapelekwa kwenye miradi mikubwa ya kiuchumi kama ujenzi wa SGR, Stirgler Gorge, ununuzi wa ndege za kisasa, elimu bila malipo, nakadhalika. Kuhamia Dodoma inayoswaga mabilioni ya walipakodi. Ukweli ni kwamba tumeamua kutumia fedha kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu badala ya watu tofauti kabisa na falsafa ya Nyerere kuhusu maendeleo tunayedai kuvaa viatu vyake!

Inaelezwa kuwa awamu hii imevunja rekodi kwa ufisadi kwa mujibu wa ripoti ya CAG 2017/18 iliyokataliwa na Ndugai. Kila unaposoma Kuna wizi basi ni mabilioni. Ni awamu ambayo sheria ya fedha na ununuzi umekanyagwa na kutemewa mate haijawahi kutokea. Hadi Leo 2.4 Trilioni haijatolewa ufafanuzi na uchambuzi jambo linaloacha mashaka makubwa. Je, tulikubaliana kwenye mkataba (Ilani) kuwa fedha zitatumika bila idhini ya Bunge? Wananchi wanauliza hawajibiwi. Watu Wako kimya.

Wakati hayo yakiendelea kikundi kidogo kinatajirika hadi kulewa fedha na madaraka. Huku gavana wa Mbeya akidai kuwa na fedha hadi za kuhonga michepuko, mwingine Dar anasema magari ya IST ni ya kuhonga watu. Kiburi, jeuri na kiburi kilichovuka mawingu. Unyenyekevu umewatoroka viongozi wetu lakini mteuzi wao kimya. Hii ilikuwepo kwenye mkataba? Hapana!

Baada tu ya kuingia madarakani zoezi la uhakiki wa silaha lilifanyika ili silaha zibaki mikononi mwa watu salama. Kwa hakika hili tunapongeza maana uhalifu ulioshamiri kipindi cha Jakaya umepungua mno. Ni matukio machache lakini unashangaa matukio ya ujambazi yamekuwa replaced na matukio ya watu kutekwa, kuteswa, kupotea na wengine kuokotwa ndani ya viroba. Kwamba tumewashinda majambazi lakini watu wasiojulikana ni mashujaa. Hadi Leo waliomshambulia Lissu kama mnyama hawajulikani. Ilani ilisema hatutawasaka wasiojulikana? Hapana!

Demokrasia imezidi kusinyaa: magazeti yamefungiwa, wapinzani hawaongei, mitandao imetungiwa sheria kandamizi, wakosoaji Wako hatarini kumalizwa, hofu imetamalaki, uandishi wa habari za uchunguzi umetoweka kwa hofu, Bunge gizani ni. Kwa nini hatukuwaambia wananchi kabla ya kuingia nao mkataba wa utawala ili waamue?

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ni muhimu kama chama tukatolea ufafanuzi kwa wananchi kabla ya kuingia kwenye mkataba mwingine na Rais Magufuli 2020/25. Uchambuzi wa kina ufanyike na wataalamu wa Sera na Mipango ili isaidie umma mpana kufanya maamuzi sahihi na makini maana bila kufanya hivyo ninawaambia wana CCM hatutaweza upepo wa Tundu Lissu. Kumzuia asiingie Ikulu kwa kura itakuwa ni sawa na kufunika jua kwa kaniki. Tuwaeleze wananchi kwa nini haya mateso hatukuwaeleza 2020? Kwa nini tulifanya siri?

Tujadiliane kwa hoja kama huwezi piga kimya jifunze kwa wengine. Karibuni waheshimiwa, mjadala umefunguliwa.
#AchaWoga2020


Tanzania hakuna utawala kuna uongozi, maana Tanzania ni nchi huru
 
tufanye Mbowe ni rais, zitto kabwe ni waziri mkuu, mbatia ni katibu mkuu kiongozi, lema waziri wa mambo ya ndani, tundu lissu ni mwanasheria mkuu wa serikali nk. baada ya miaka minne, tanzania itakua kama ulaya? watanzania tutakua na pesa mikononi? wote tutaishi maghorofani? ni nini unadhani watafanya? mnadhani shida ya tanzania ni rais? mnafikiri wapo watu special wa kuwapa utajiri? mnajidanganya na mnapoteza muda........
 
Back
Top Bottom