Bollen Ngetti: Taifa linavuja Damu

Bollen Ngetti: Taifa linavuja Damu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,892
TAIFA LINAVUJA DAMU!

Na Bollen Ngetti

NAWASALIMU marafiki zangu wote kwa matumaini kuwa hamjambo. Ukimya wangu unawaumiza wengi wenu na kuwafurahisha wachache wenu. Ninapitia kipindi kigumu sana kiusalama kwa hiyo nafasi inapopatikana ndipo tunaweza kutafakari kama sasa.

Hali ya mambo nchini kwa sasa ni ya kukatisha tamaa na hakuna maneno matamu zaidi Taifa kuvuja damu. Nimetafuta mchora picha anichoree Tanzania inayovuja damu nimekosa ndio maana andiko hili halina picha.

Ndugu zangu, miezi kadhaa niliandika nikionya kuwa njaa yaja nikabezwa mno na mkuu wa nchi akasema "hakuna chakula cha bure" na ole wake DC ataayegawa chakula. Sasa huko Shinyanga baa la njaa ni tete na wanagawiwa chakula cha bure. Tulipuuza maonyo, Taifa linavuja damu.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umekuja ukapita kama upepo na laana juu. Hakuna waliochaguliwa wala hakuna waliopiga kura. Wababe wamejitangazia ushindi. Taifa linavuja damu. Vijana wamekata tamaa si tu kushiriki siasa lakini hata maisha. Taifa linavuja damu.

Rais anasema huko Udom kuna watu wanamkatisha tamaa lakini hatokata tamaa. Lakini amesahau kuwa ni wateule wake ndio Mayuda Isariote wanaomsaliti kwa tamaa ya kushibisha matumbo yao. Tunaona Mkurugenzi wa moja ya mkoa kanda ya ziwa akishinda Kigamboni kuporomosha mahekalu ukimuuliza anakwambia JPM rais wa wanyonge. Taifa linavuja damu.

Niseme kidogo kuhusu Yuda aliyekuwa mwanafunzi wa mwisho kuteuliwa na Bwana Mkubwa lakini malengo yake yakiwa ni kutengeneza faida si uzalendo wa kiimani ndio maana ikawa rahisi kumuuza Yesu kwa fedha. Hawa mayuda yamemzunguka Magufuli wanaotumia umaarufu wake kutengeneza faida si kutumikia umma. Wanamsaliti Magufuli. Ndege yetu inakamatwa Canada wanamdanganya bosi wao. Taifa linavuja damu.

Miradi inayotatiza uchumi inajengwa bila ridhaa ya umma kupitia bunge sawa na baba anayejenga tiles kila mahali lakini watoto wakilala njaa. Taifa linavuja damu.

Tundu Lissu amegoma kurudi nchini akihofia kuuawa. Demokrasia imetoweka nchini Tanzania. Taifa linavuja damu.

Gharama za maisha imepanda kila mahali hadi washirikina wanalia. Taifa linavuja damu. Viongozi wa dini ambao wangeponya Taifa nao wanavuja damu. Mbele ni kiza kinene. Hata hivyo,
#AchaWoga2020

Na Bollen Ngetti
 
Atembee na silaha tusikie kamwaga gaidi mavi sio kila siku kulialia,sheria ya self defense inamruhusu hata kuuwa kwa mazingira ya kujitetea.
 
DeepPond,
Akifanya hivyo atafanya mkutano jimbo gani maana sasa hivi wanaoruhusiwa kufanya mikutano ni wabunge,madiwani na
no. 1 peke yao
 
hata wana wa israeli walipokengeuka walivamiwa na nebukadreza wa babeli hekalu lao nzuri ikabomolewa na wao kwenda utumwani babeli. sasa kuhusu tanzania babeli inakuja wakati utakapoangushwa utawala huu kwa kuwa haushauriki mana bii wengi wamenena juu yake uache madhambi lakini bado hakuna anayesikia mwisho unakuja ni sawa na kupambazuka giza inazidi kuwa nene kwa maana baada ya wana wa israeli kumaliza adhabu yao masalia waliobaki wakarudi yerusalemu wakamuabu mungu wao wakawa taifa kubwa tena.

wala watanzania wasiogope maana ukombozi wao uko karibu
 
hata wana wa israeli walipokengeuka walivamiwa na nebukadreza wa babeli hekalu lao nzuri ikabomolewa na wao kwenda utumwani babeli. sasa kuhusu tanzania babeli inakuja wakati utakapoangushwa utawala huu kwa kuwa haushauriki mana bii wengi wamenena juu yake uache madhambi lakini bado hakuna anayesikia mwisho unakuja ni sawa na kupambazuka giza inazidi kuwa nene kwa maana baada ya wana wa israeli kumaliza adhabu yao masalia waliobaki wakarudi yerusalemu wakamuabu mungu wao wakawa taifa kubwa tena.

wala watanzania wasiogope maana ukombozi wao uko karibu
Amina mtumishi achana na wale walevi wa sadaka
 
Nabii bushir 2015 keshawahi sema naona anga la tz limejaa damu,kila mtu u shahid
 
Kumbe Bollen ngeti ni mwanasiasa uliyejificha kwenye mgongo wa uandishi wa habari?

Mara ngapi kwa hila maalum umehojiwa na vyombo vya habari vya nje ukijifanya mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwanahabari?

Kumbe ni pro membe mtumiwa mkubwa wewe!

Unakumbana na ulichokistahili kabisa!

Mko wengi wa type yenu na mtakwama kwa nguvu za mungu!
Watanzania tunawaona sana,

Tunamuombea maisha marefu kiongozi wetu mpendwa JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI.

2020 - 2025[emoji1241][emoji818][emoji110]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom