isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,152
- 6,601
Bolivia, Estado Plurinacional de Bolivia, Plurinacional States of Bolivia au Tetã Hetãvoregua Mborivia
Jamhuri ya watu wenye asili mbalimbali katika Bolivia ikifahamika kama BOLIVIA ni taifa linalopatikana bara la Amerika Kusini likiwa na mipaka baina ya Ajentina, Brasil, Chile, Paraguái na Peru.
Moja kati ya bendera tatu za Bolivia
Bolivia inayopatikana katika uwanda wa juu wa milima ya Andes, yenye ukubwa wa eneo zipatazo kilomita za mraba millioni 1,098,580 sawa na maili za mraba 424,164 nyumbani kwa watu takribani millioni 11,673,021 kufikia Julai 1, 2020.
Jengo la Ikulu ya rais, jijini La Paz ©Freyas Adre / Presidential Palace
Kauli kuu ya taifa ni “La Unión es la Fuerza” | “Umoja ni Nguvu”, Miji mikuu ya taifa ni La Paz na Sucre. Lugha 38 ni rasmi kwa taifa huku Kihispaniola kikizungumzwa zaidi kwa asilimia 85. Pesa rasmi ni Boliviano (BOB), Boliviano 1 ni sawa na Centavos 100.
Jijini La Paz ©BoliviaSol
Santa Cruz, La Paz, Cochabamba, Sucre, Potosí na Oruro ndio miji yenye maendeleo zaidi kwa Bolivia. La Paz ndio mji wa kwanza Amerika ya Kusini kuwa na umeme huku Potosí ndio mji uliokuwa mkubwa zaidi mnamo mwaka 1545.
La Residencía La Paz ©Fraga Paz
Bolívar na Bolivia
Unapozumgumzia Bolivia huwezi kuacha kumtaja kiongozi mpambanaji wa wakati huo mVenezuela, Bw. Simón José Antonio de la Santísima Trinidad Bolívar y Palacios Ponte-Andrade y Blanco aliyekuwa kiongozi wa juu wa taifa la Gran Colombia iliyokuwa muungano wa mataifa ya Bolivia, Colombia, Ecuador, Panama, Peru na Venezuela za sasa.
Mwanamapinduzi Simón Bolívar alipigania haki za kiutawala, utendaji, uchumi, mipaka na asili za Gran Colombia akihakikisha mataifa hayo yanaondokana na mabavu ya Uhispania. Kupitia juhudi zake aliweza kuing'oa Uhispania na kwa heshima yake akawa rais wa Gran Colombia.
Kutokana na kuvunjika kwa Gran Colombia na mataifa kujipatia majina yaliyokuwa na asili, taifa huru kwa kutambua mchango wa kiungo muhimu wa mapinduzi likatohoa jina la aliyekuwa kiongozi Bolívar.
Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Kilimo, Maendeleo na Utalii
Bolivia inatambulika kama taifa lenye kiwango cha umaskini kwa asilimia 35, kulifanya taifa maskini Amerika ya Kusini. Asilimia 83 ya raia wa Bolivia wanaishi maeneo ya vijijini.
Kilimo cha maharage ya soya mjini Potosí ©AgriBolivia
Uchumi wa taifa unachagizwa na kilimo, misitu, uchimbaji madini, mafuta na gesi, uvuvi na viwanda. Bolivia ni nyumbani kwa madini ya Ametrine, Golden Amethyst, Trystine au Bolivianite, huku ikiongoza kuwa na Lithium duniani huku ikiwa na madini ya shaba, chuma na fedha.
Madini ya Bolivianite ©BoliviaSol
Kilimo kikubwa ni maharage ya soya, pamba, kahawa, ndizi, miwa, mahindi, ngano, kokoa, pilipili na viazi, huku bidhaa nyingine za vyakula na matunda zikitumika kusindika bidhaa viwandani. Mnyama Llama mwenye muundo wa ngamia, kondoo na mbuzi anapatikana Bolivia.
Bidhaa za vyakula vya Bolivia ©Latam Farms
Magari nyaya (Cable Car's) jijini Santa Cruz ©Ciudad Santa Cruz
Viwanja vya ndege vya kimataifa El Alto, Viru Viru na Jorge Wilstermann, mifumo ya magari nyaya (Cable Car's), mifumo ya maji na umeme wa upepo na jua ni baadhi ya maendeleo katika taifa.
Salar de Uyuni, Salar ©Backpackers
Utalii unachagizwa na Salar de Uyuni eneo tambarare lenye chumvi zaidi duniani, sehemu ya ajabu yenye kuakisi kama kioo wakati wa mvua, iliyosheheni tani za chumvi zipatazo million 64 katika eneo lenye kilomita za mraba 10,582 sawa na maili za mraba 4,086. Pia utashuhudia hoteli iliyojengwa kwa chumvi Palacío de Sal Resort.
Ziwa Titicaca ©BoliviaSol
Vivutio vingine ni gereza la San Pedro, gereza la kulipia kuwaona wafungwa wanaoshi na familia zao ndani huku wakipewa ruzuku na kufanya biashara ndani ya gereza, uwepo wa vituo vya simu, soko, kumbi za starehe na kiwanda cha uzalishaji madawa yenye usaidizi hospitali.
Pomboo wa rangi ya waridi ©Laym Zarimi
Ufikapo Ziwa Titicaca utawaona pomboo wenye rangi ya waridi wanaofahamika kama Inia Geoffrensis.
Elimu, Teknolojia na Sayansi
Bolivia inatoa elimu ya awali msingi na upili kwa lazima pia elimu ya juu katika vyuo bora Universidad Mayor de San Andés, Universidad Mayor de San Simon, Universidad Técnica de Osuro, Universidad Autónoma Tomás na Nur University.
Katika sayansi na teknolojia kama taifa linamiliki satelaiti ya mawasiliano iliyoundwa na Bolivia huku ikirushwa na Uchina. Teknolojia imebebwa pakubwa na Bw. Marcelo Claure mwanzilishi wa kampuni ya Sprint Corporation.
Michezo na Sanaa
Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Bolivia ©CONMEBOL
Kupitia michezo Bolivia inawakilishwa na timu ya taifa ya mpira wa miguu. Nyumbani kwa mwandishi, mchoraji, mtunzi, mpiga picha na mfanyabiashara Francis Schwitegebel Torres na mlimbwende Jessica Anne Burton.
Hii ndio Bolivia 🇧🇴