Bolingo za Kicongo za miaka ya 90`s | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bolingo za Kicongo za miaka ya 90`s

Discussion in 'Entertainment' started by Ligogoma, Oct 12, 2011.

 1. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,142
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Habari wana JF???

  Nianzie mbali kidogo, weekend hii nilikuwa natokea Arusha kuelekea Mbeya, nilipanda mabasi yetu yale ambayo kampuni pinzani wanyaita 'mahotpot' kwa jinsi yalivyokaa ila kiukweli yana raha yake bana.

  Speaker nzito, screen kubwa na siti zake ni za maana kiasi kwamba ni starehe tupu!! Promo si lengo langu but penye ukweli tuzungumze.

  Kilichonikosha zaidi ni pale walipotuwekea cd ya nyimbo za asili ya Congo za miaka ya 90`s ingawa nyingi majina yalinitoka lakini si haba wengi tuliburudika saaaaana na kukumbuka mbali kwa kweli. Vijana na wazee waliokuwemo humo wenye above 30 yrs walitikisa vichwa kwa sana.

  Ndugu zangu, mnakumbuka nyimbo za Yondo Sister? Wapiyo, mbutamutu!!! Kuna vijana wa Wenge BCBG na mikwaju yao mikali kama kala yi Boeing, Aurlus Mabele na vitu vyake kama Evelyna, Betty, mnawakumbuka soukouss satars??? mnawakumbuka kina Lokasa Yambongo, Balou Canta, Shimitta, Alin Kounkou, Diblo Dibala, Awilo Longomba na vitu kama Moyete, Bibalabala, Zipompapompa, Mayaula mayoni na Mzee mzima Madilu malti System??? Hizo ni chache tu nilizokumbuka jamani

  Kuna wale nguli kama kina Pepe Kalle na Koffie Olomide enzi zao kila albam wakitoa kali!!! Hakukuwa na bongo fleva kipindi hicho hahahahaaaa!!!

  Jamaa MP3 yao ilisimama na hizi nyimbo nilisha zisahau kwakeli, nahangaika kutafuta collection ya hizi nyimbo!!! Nazisaka kwa kila hali na ukienda kwenye hivi vistudio ukiwauliza vijana kuhusu Damien Aziwa nani anamjua?????

  Ok, tushee pamoja jamani wewe unakumbuka vibao gani hapo???? Na unakumbuka nini na wapi???

  Maana mie nilikuwa bado kabwana mdogo namsindikiza bro disko Moshi enzi hizo ukumbi wa Liberty na sinema Plaza hahahahaaaaa!!! Dah!!! Maisha haya siamini kama ndo nazeeka hivyo!!!!!!
   
Loading...