Unyakyusani na sherehe za Krismasi na Mwaka mpya miaka ya zamani

Tychob

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
3,655
4,626
Kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya leo nimejikuta nimekumbuka nyuma kidogo mwanzoni mwaka miaka ya 2000 kurudi nyuma. Namna ambavyo sherehe hizi zilivyokuwa zinafana na kupendeza kwa namna yake huko UNYAKYUSANI. Achana na watoto kununuliwa nguo mpya na kupika chakula cha ukweli.

Kulikuwa na nyimbo za kinyakyusa zilizo kuwa zinatawala na kuleta furaha ya aina yake isiyo mithilika, nyimbo hizi zilikuwa zinaimbwa na vikundi vya vijana na watu wa rika mbalimbali ambao walikuwa wanajisikia kuimba, vikundi hivi vilikuwa vikizunguka katika kila nyumba huku wakiimba nyimbo za hizo siku(Christmas na mwaka mpya).

Kila nyumba ambayo walikuwa wakipita walikuwa wakipewa zawadi mfano pesa, chakula, mahindi, ndizi n.k . Hizi zilikuwa ni siku za furaha kwelikweli ...hapa chini ni baadhi ya nyimbo kwa kifupi zilizo kuwa zinaimbwa

Krisimasi.

Mwe ujesu mwe apapighwe ,ku nndindwana marija ungolofu...×2

Mwe ujesu mwe apapighwe ,

Nkajha ka ndabhiti...×3

Tafsiri

(Jamani yesu jamani alizaliwa,

Kwa msichana bikira Maria.×2

Jamani yesu jamani alizaliwa,

Kwenye mji wa Daudi...×3)


Mwaka mpya.

Tulobhwike tulobhwike mwe tulobhwike nnkyinja ikipya kya jhanuari... (Mwe naloli mwe ...×3)

Tafsiri.

Tumevuka tumevuka jamani tumevuka kwenye mwaka mpya wa januari... ( Jamani kweli jamani...×3)

Kama unakumbuka sherehe hizi zilivyo kuwa zinafanyika huko unyakyusani karibu uchangie

"Ukyala nnkota usetano ibhole"
 
Jamani Leo simba imeshindaaaaa x3.
Jamani Leo simba imeshindaaaaa x3.
Jamani Leo simba imeshindaaaaa x3.
 
MZee babaa Mbona Kuna Chumvi?


Solo:Jesu Mwe X3
All:Apapigwe

Solo:Jesu Mwe X3
All:Apapigwe Kundindwana marija ungorofu

Unarudia Mara 3 Kipengele Chote juu
Kisha Unamalizia na Kibwagizo

Solo:Andendesa
All:Andendesa
Solo:Andendesa
All:Andendesa Andendesa Andendesa


Wakati Wa Mwaka Mpya

Solo:Tulo Mwe X3
All:Tulobwike

Solo:Tulo Mwe X3
All:Tulobwike Nkyinja ikipya Tulobwike

Solo:Andendesa
All:Andendesa
Solo:Andendesa
All:Andendesa Andendesa Andendesa


Ila umenikumbusha mbali sana mkuuu hongera kwa kumbukumbu
 
Duuuh umenikumbusha mbali kweli kweli wanyakyusa raha tupu kesho ndo kutakucha nadhani wanaendelea ndagha fijo nkamu ghwangu
 
MZee babaa Mbona Kuna Chumvi?


Solo:Jesu Mwe X3
All:Apapigwe

Solo:Jesu Mwe X3
All:Apapigwe Kundindwana marija ungorofu

Unarudia Mara 3 Kipengele Chote juu
Kisha Unamalizia na Kibwagizo

Solo:Andendesa
All:Andendesa
Solo:Andendesa
All:Andendesa Andendesa Andendesa


Wakati Wa Mwaka Mpya

Solo:Tulo Mwe X3
All:Tulobwike

Solo:Tulo Mwe X3
All:Tulobwike Nkyinja ikipya Tulobwike

Solo:Andendesa
All:Andendesa
Solo:Andendesa
All:Andendesa Andendesa Andendesa


Ila umenikumbusha mbali sana mkuuu hongera kwa kumbukumbu
Hahaha ahsante mkuu , si unajua niliimba zamani, nashukuru kwa kunikumbusha kwa usahihi...
 
MZee babaa Mbona Kuna Chumvi?


Solo:Jesu Mwe X3
All:Apapigwe

Solo:Jesu Mwe X3
All:Apapigwe Kundindwana marija ungorofu

Unarudia Mara 3 Kipengele Chote juu
Kisha Unamalizia na Kibwagizo

Solo:Andendesa
All:Andendesa
Solo:Andendesa
All:Andendesa Andendesa Andendesa


Wakati Wa Mwaka Mpya

Solo:Tulo Mwe X3
All:Tulobwike

Solo:Tulo Mwe X3
All:Tulobwike Nkyinja ikipya Tulobwike

Solo:Andendesa
All:Andendesa
Solo:Andendesa
All:Andendesa Andendesa Andendesa


Ila umenikumbusha mbali sana mkuuu hongera kwa kumbukumbu
Wewe utakuwa ni Wa Kyela Tukuyu hatuimbi hivyo
 
Back
Top Bottom