IBRA wa PILI
JF-Expert Member
- Oct 12, 2017
- 1,549
- 2,689
Ilikuwa ni Mei 2, 2013 ambapo Jason Airey (37) alipatikana akiwa amefariki chumbani kwake nyumbani kwao Cumbria kaskazini mwa UK. Baada ya uchunguzi ilifahamika kuwa alifariki baada ya kufungua Box la Pandora. Lilikutwa pembeni yake likiwa limeandikwa kwa wino mwekundu 'Box la Pandora'.
Ilibainika kuwa moyo wake ulisimama na kusababisha viungo vyake kufeli. Lakini haikuwahi kujulikama ni kwanini moyo huo ulisimama. Baba yake Airey Dennis (64) alisema kuwa mtoto wake alirudi nyumbani akitoka matembezini, alipofika akaingia chumbani lakini hakuonekana akitoka tena, ndipo alipoamua kumfuata.
"Uso wake ulikuwa wa bluu. Nilihisi kagongwa kwa nguvu kwenye shingo yake. Nilikiona kipakiti kidogo ndani ya box, nilifikiria labda ni bangi lakini haikuwa na harufu. Ilikuwa pakiti, lakini ilikuwa haijatumika. Ilikuwa kitandani karibu naye. Alikuwa amekufa tayari".
Je, Box la Pandora ni box la namna gani?
Kwa mujibu wa imani za wagiriki wa kale, Pandora ni jina la mwanamke aliyeumbwa na Hephaestus kwa maagizo ya Zeus. Hephaestus alikuwa ni mungu wa moto, na Zeusi alikuwa ndiye Mungu wa miungu yote ya wagiriki wa kale katika karne ya 7. Hivyo Pandora ni binadamu aliyeumbwa na miungu hawa wa Kigiriki.
Baada ya kuumbwa Pandora akawa anapewa zawadi kwa miungu yote, na hata jina lake kwa kigiriki lina maana ya "anayezawadiwa zawadi zote", hivyo Mungu mkubwa Zeus alimzawadia box, linaitwa Box la Pandora.
Walimwambia kuwa box hili lilikuwa na zawadi maalum kutoka kwao lakini hakuruhusiwa kulifungua milele yake yote.
Baadae Pandora alishindwa kuvumilia, akalifungua box n ghafla kukaanza kutokea magonjwa, vita, njaa, ukame, mapepo na mabalaa yote!, ilielezwa kuwa miungu walikuwa wanazitunza roho chafu za kishetani ndani ya box hili, hivyo lilipofunguliwa tuu likaanza kuleta majanga makubwa sana. Pandora aliogopa sana, akalifunga haraka.
Box hili la Pandora ndilo hili linaloaminika kuwa alikutwa nalo Jason mwaka 2013 na kufa hapo hapo baada ya kulifungua. Haijawahi kujulikana alilipata wapi box hili. Na haijulikani box hili lilipotelea wapi baada ya tukio hili.
Chanzo and credits FM facts