SNAP J
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 7,117
- 8,096
Taarifa za kutisha zimeibuka kutoka mjini Bama, moja ya miji ambayo ilitekwa na wapiganaji wa
kiisilamu wa Boko Haram Kaskazini Mashariki ya Nigeria ambapo wakazi wake hawaruhusiwi kuwazika jamaa zao waliouawa na wapiganaji
hao.
Inaarifiwa miili imetapakaa katika barabara za mji
huo ambao Boko Haram imeuteka. Kundi hilo linasemekana kuuteka mji huo huku wapiganaji wa kundi hilo wakishika doria katika barabara zake.
Maelfu ya watu wametoroka huku idadi kubwa ya wengine wakiuawa.
Maafisa wakuu wanakisia kuwa watu 26,000
wameachwa bila makao kufuatia mapigano
katika mji wa Bama.
Boko Haram wameteka miji kadhaa Kaskazini
Mashariki ya Nigeria, katika miezi ya hivi karibuni
na kusababisha hofu kuwa huenda wakaufikia mji
mkuu Maiduguri ambao Una watu zaidi ya milioni 2.
Chanzo; BBC