Boko haram kuwaachilia Wanafunzi

Boko haram kuwaachilia Wanafunzi

Status
Not open for further replies.

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,930
Reaction score
63,674
attachment.php

Wanafunzi wa Chibok waliotekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram


Serikali ya Nigeria inasema kuwa imefikia makubaliano na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kuhusu wasichana waliotekwa nyara wa Chibok.

Mkuu wa jeshi la Nigeria Alex Badeh,aliyefichua makubaliano hayo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu kati ya nchi hiyo na Cameroon anasema kuwa wanajeshi wa Nigeria watatimiza matakwa ya makubaliano hayo.

Serikali imesema imekuwa ikifanya mazungumzo na viongozi wa Boko Haram.

Kulingana na afisaa mkuu kiatika ofisi ya Rais Goodluck Jonathan, Hassan Tukur ambaye alifafanua taarifa hiyo, wajumbe wa serikali walikutana na wapiganaji wa Boko Haram mara mbili nchini Chad chini ya uongozi wa Rais wa Chad Idris Derby.

Alisema kuwa Boko Haram wamekubali kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara mjini Chibok, hata hivyo, maelezo kuhusu kuachiliwa kwao yatakamilishwa katika mkutano mwingine utakaofanyika wiki ijayo mjini Njamena.

Pia alieleza kwamba maafisa wa ujasusi wa Chad walihusika katika mpango huo na kwamba wamethibitisha mazungumzo hayo yamefikiwa na kukubalika na kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau.



Chanzo: BBC
 

Attachments

  • 141015152806_nigeria_chibok_abducted_school_girls_640x360_bbc_nocredit.jpg
    141015152806_nigeria_chibok_abducted_school_girls_640x360_bbc_nocredit.jpg
    4.2 KB · Views: 370
  • abc_boko_haram_140512_16x9_992.jpg
    abc_boko_haram_140512_16x9_992.jpg
    60.3 KB · Views: 572
Hao bako Haramu wasije tu wakaanzisha ISIS yao Africa, wakijaribu mi ntawaponda na jiwe au ntawafinya.
 
Hao bako Haramu wasije tu wakaanzisha ISIS yao Africa, wakijaribu mi ntawaponda na jiwe au ntawafinya.
nilisikia wameungaa na shabaab? africa inahitaji spark ndogo sana iwe conflagrated. assume ADF, haram, shabaab, seleka, maghreb na wale walibya walianzishe kwa kushirikiana!
 
Waangalie wapi walipojificha, you know what to do.."Nigeria"
 
nilisikia wameungaa na shabaab? africa inahitaji spark ndogo sana iwe conflagrated. assume ADF, haram, shabaab, seleka, maghreb na wale walibya walianzishe kwa kushirikiana!

Watanyamazishwa vibaya sana, wasifanye mchezo na baadhi ya nchi
 
Nadhani ndio mwisho wao, wakiisha kabidhi watoto tu wapigwe mabomu ta sumu waishe...
 
Hamna lolote, rais wa nchi hiyo antarajiwa kutangaza nia yake ya kgombea urais tena ndani ya muda mfupi ujao, habari za boko haram kuridhia na serikali zimetolewa kabla tu ya rais kujitangaza kuwania urais tena...wachambuzi wanasema ni siasa hiyo, apate pa kuongea na kuanzia
 
Hapa ndipo utata unapozidi. Ikumbukwe kwamba utekaji nyara huo ulizusha maswali mengi mpaka baadhi kuhisi serikali ya Nigeria ina siri na ugaidi huo. Hivi karibuni serikali ikadai kumuua kiongozi wa magaidi hao. Kwa tangazo hili japo litaleta amani kwa waliopotelewa na watoto but inazidisha maswali zaidi.
 
watakuwa wameshawaribu sana hawa boko haramu wakishaachia hao watoto wanatakiwa kupuliziwa sumu wafe wote wameua watu wengi sana tena wasiokuwa na hatia nawachukia sana boko haramu kama ninavyochukia ccm
 
BH is a loose affiliation of radicals with the same ideology and no apparent leadership or sense of direction.

Have they negotiated with the real BH??

So where are the Chibok girls ? When will they be released?
 
So fun... Pamoja na evidence zote zinazoonyesha kuwa hakuna utekaji wowote uliofanyika kwa wasichana, ikinogeshwa na ukweli kuwa hakuna mzazi aliejitokeza kudai watoto wao still kuna wapuuzi wanaendelea kukoleza propaganda za kimagharibi... Tunajua kuwa Boko Harama ilitengenezwa na US ili ku-destabilize Nigeria na hatimae waendelee kujichotea mafuta/black gold...
 
afu hugo gu Abubakari Shekau si iliripotiwa gumeuawa, mbona bado gupo?! ngoja nifunge na kuomba labda gutauawa
 
Minnavyojua mtu ukisha pigana nae.hata ukimshinda.ukipata upenyo wa kufanya naemazungumzo ilimuyamalize unakubali faster.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom