Boeing 787: Waziri Mbarawa ametudanganya, hakuna Line Number 719

whizkid

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
357
240
Kuna taarifa imezagaa ikidai kuwa Waziri Mbarawa akisema Serikali yetu imenunua ndege mpya aina ya 787 Dreamliner ambayo wapo kwenye mchakato wa kuchagua engine. Amedai kuwa ndege yetu ni line number 719. Uwongo mkubwa. 787 hazijafikia hiyo line number, kwa maana ya ndege zilizoanza kuundwa, ushahidi huu hapa toka data za kiwandani.

NB: Ushahidi bado unaonesha kuwa tumenunua Line no. 19, kama inavyoendelea kuzungumzwa na wengi na kama inavyoonekana toka data za Boeing.

Update 1:
Kwa wenye mashaka na hii list, hizi line numbers zote na serial numbers zinaweza kuhakikiwa. Pia, taarifa rasmi ya Boeing inaonesha wamesha fanikiwa kuwasilisha ndege zaidi ya 541 kati ya order 1211. Mwaka jana wote walipokea order 58 na mwaka huu hadi sasa order 11. Fanya mahesabu uone hata hiyo 719 ambayo haijaanza hata kutengenezwa kama haitakuwa order ya nyuma. Official orders za Boeing 787: http://active.boeing.com/commercial...odels&cboAllModel=787&ViewReportF=View+Report


Screenshot_20170504_183731.jpg


Source: Boeing Production List (787 Line Numbers)

Update 2:
List kamili zaidi yenye line number 719. Soma sheet iliyoandikwa 787 Current Production, angalia row ya 17, pia angalia na row ya 186: 787 Tables

Update 3:
Hii update ya 2 hapo juu, ni data toka kwa analyst anaitwa Uresh Sheth. Mnaweza mkatafuta awape details zaidi za hiyo Line 19. Linkedin profile yake: https://www.linkedin.com/in/uresh-sheth-2752306 au Twitter: (@787Blogger): 787Blogger (@787Blogger) | Twitter au Blogger account yake: All things 787

Why this Wall Street banker Uresh Sheth is plane crazy - The Economic Times
 
Kuna taarifa imezagaa ikidai kuwa Waziri Mbarawa akisema Serikali yetu imenunua ndege mpya aina ya 787 Dreamliner ambayo wapo kwenye mchakato wa kuchagua engine. Amedai kuwa ndege yetu ni line number 719. Uwongo mkubwa. 787 hazijafikia hiyo line number, ushahidi huu hapa toka data za kiwandani.

NB: Ushahidi bado unaonesha kuwa tumenunua Line no. 19, kama inavyoendelea kuzungumzwa na wengi.

Screenshot_20170504_183731.jpg


Source: Boeing Production List (787 Line Numbers)
Tena ndege yenyewe ni mtumba. Morocco hawaitaki tunauziwa sisi ma-bashite kwa bei ya kuruka!
 
ogopa manunuzi ya cash,hata public procurement act and regulations zinakataza manunuzi ya cash sababu always yana harufu ya wizi...mkuu barafu njoo huku utusaidie kufanya mjadala kuwa mfupi
Kulingana na maelezo na mjadala wa Bungeni, inaonesha wazi kuwa hatujalipa hela cash. Maana yake, ni kuwa tumesign purchase agreement. Ukitaka kujua ni jinsi gani aina hizo za agreements ndizo zimemleta mfalme wa Moroco kuja kututembelea, au sisi kwenda Rwanda mapema mwaka jana, na baadae Rwanda kuongeza ushirikiano nasi kama ilivyokuwa kwa ahadi kadhaa za mfalme wa Morocco, pitia mkataba wa kimataifa unaosimamia manunuzi ya ndege ambao sisi tumesign. Hapa: Protocol to the Convention on International Interests in Mobile Equipment on matters specific to aircraft equipment - Wikisource, the free online library

Sioni hili likizungumzwa sana, labda watu bado hawaioni hii connection, lakini fedha tunayotarajia kununulia ndege ya bei nafuu kwa gharama kubwa zaidi, baadhi itarudi Morocco na ndio hiyo hiyo watakayofidia kwenye tuvimisaada watakavyotupa kama vile kutujengea msikiti Dodoma.

Huo ni uchambuzi wangu tu, utaelewa zaidi kama utaweza kuelewa MASHARTI ya Article III ya Capetown Protocol.
 
Hii ndiyo JF bhana Watu wanajua kusaka ' data ' kuliko hata wenye ' Mamlaka ' wanavyoweza. Kwa hizo ' data ' za Mkuu hapo juu naona sasa Waziri Mbarawa nae ameshaanza ' Kukengeuka ' Kiutendaji na ni hatari sana hasa kwa Mtu kama Yeye anayeongoza moja ya Wizara muhimu kabisa kama siyo ' nyeti ' hapa nchini Tanzania.
 
Nimependa ulivyoandika kuwa .....ikidai...

Hivyo hata wewe huna uhakika bali unadakia kumshutumu tu.
Kwa sababu sijafanikiwa kuthibitisha toka kwa Waziri na wala yeye au Wizara yake haijakanusha taarifa "sensitive" kiasi hiki. Source: Serikali yakanusha kununua ndege “Kimeo” aina Boeing & 787-Terrible teen – Mitandaoni: Siasa, Michezo na Burudani

Shutuma yangu itakuwa "negated automatically" kama Waziri husika atakanusha taarifa inayozagaa (ikiwemo hii) kumhusu yeye.

Kwenye hili, he is definitely guilty until proven innocent, not the opposite.
 
Back
Top Bottom