Castr
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 33,748
- 67,715
Socrates aliwahi kusema "...ni aibu iliyoje kwa mwanadamu kuzeeka bila kujua ni nguvu kiasi gani na uzuri kiasi gani mwili wake unaweza kufikia"
Nataka tujigee changamoto ya kuona ni kwa kiasi gani katika mazoezi tunaweza kuulazimisha mwili kwenda zaidi ya ulivyozoea. Hii ni kwa kila anayefanya mazoezi, iwe mazoezi yako ni kichura chura na kukimbia mpaka yule anayeruka kichura chura, kukimbia, mfanya plyometrics, mnyanyua uzito na hata mkata tumbo.
Kwa ambao tutakua tunanyanyua uzito napendekeza changamoto yetu iwe hivi;
1. Zoezi liwe na raundi 6, utapanda mzigo wako kila baada ya raundi mbili.
2. Kupumzika ni sekunde 15 kwa kila zoezi na sekunde 20 kwa kila unapomaliza zoezi moja.
Yaani mfano unapiga squats, smith machine itakua na raundi sita, utaongeza mzigo kila baada ya raundi ya pili. Ukija kwenye leg press napo utafanya idadi ya raundi hizo hizo na kupanda hivyo hivyo mpaka umalize zoezi lako.
Kwa ambao tutakua tunakimbia changamoto yetu iongezwe kwenye;
1. Idadi ya raundi tunazokimbia.
2. Tuongeze kasi kila baada ya raundi tatu.
Mfano unakimbia kiwanjani, na hua unakimbia raundi 10, fika mpaka 12, na ongeza kasi yako kila baada ya raundi tatu.
Kwa ambao tunakata tumbo;
1. Tunaongeza idadi ya reps zetu.
2. Tunapunguza muda wetu wa kupumzika.
Mfano kama ulikua unaenda reps 12 zifike mpaka 16 na pumzika kwa kupunguza sekunde tano kwa idadi ya sekunde ulizokua unapumzika mwanzo.
Kama wewe ni boxer;
1. Mwambie partner unayefanya naye sparring kua haujasikia kengele unataka raundi moja ya mwisho.
Hata hivyo hii routine itapanda kila baada ya wiki moja, hivyo hii ni routine yetu ya kuanzia. Baada ya wiki raundi zitakua saba, na kila ulipoongeza wiki hii ikifika wiki ijayo ongeza moja. Tutafanya hiki kitu kwa wiki mbili kisha tutaangalia tumefika mpaka wapi.
Mdau, tafadhali tuma picha ya mzigo wako ukiwa gym, tuma picha ya kapeti lako ukiwa unaanza kukata tumbo, tuma picha ya kiwanja utakachokimbilia, tuma picha ya ngazi unazotumia kufanya plyometrics, tuma picha ya kistuli unachowekea miguu ukiwa unapiga push ups, tuma kamba yako, tuma gloves zako, Ikiwezekana tuma picha yako ukiwa kwenye zoezi lako. Nitakua nikifanya hivyo binafsi.
Mwisho wa kila kitu ni kupeana moyo huku tukiwa tunagundua ni kwa kiasi gani tunaweza kupapita pale tulipoishia jana.
Challenge itaanza Jumatano ya tarehe 19.
##Body4lyfChallenge
Update:
Tafadhali usiniquote na kuniuliza juu ya hii mada