Bodi ya Wachumi Tanzania

Bowbow

JF-Expert Member
Oct 20, 2007
541
31
Ndugu wana JF,

Nimesukumwa sana kuleta hoja hii hapa mbele yenu baaada ya kuona ni namna gani Uchumi wa nchi unaendeshwa bila kuzingatia maslahi ya nchi.

Kwa sasa Tanzania haina Bodi ya wachumi ambayo ingekuwa inatoa maoni(proffessional advice) mbalimbali, kukemea, kuelimisha, kushauri, kutafiti n.k kwa manufaa ya serikali, umma, na vyombo mbalimbali kuhusiana na sera mbalimbali, matokeo mbalimbali(Volatility of Oil prices, Gold, Increase in electricity cost, umasikini, afya, finance,n.k)

Kwa sasa serikali inategemea wachumi waliopo kwenye ofisi zake, ESRF, REPOA na Universities katika kuandaa na kutekeleza sera zake ikiwa wote wanategemea funding kutoka serikalini thus hawawezi kuishauri serikali vinginevyo pale inapotokea sera zake hazikuleta matunda yaliyotarajiwa.

Hivyo bodi inahitajiwa ili kuwahusisha wachumi wote walioma ndani nje ya serikali, pamoja nje ya nchi na wengine wanaopenda kujiunga na bodi hiyo kuisadia serikali kwa kushauri, kuelimisha, kutafiti, kukemea sera chafu kama za madini(kuanzia utafutaji, uchimbaji, uuuzaji, na hata ulipaji kodi), Sera za ubinafsishaji na Uwekezaji zisizomjali Mtz, ukusanyaji wa kodi, unemployment n.k).

Chombo hiki kilikuwepo wakati wa Mwl.JK ila baada ya Mh AHM kuingia madarakani viongozi wote wa chombo hiki na wengi wa members wao walipewa madaraka na majukumu makubwa serikalini wakashindwa kufanya kazi za chama na hata kuitisha vikao ili kuchagua viongozi wengine mwisho wake kikatoweka.

Je nini maoni yenu wana JF kwa kutaka kuanzisha kwa bodi hiyo?
Naamini humu kuna wachumi humu JF, wewe kama mchumi nini mchango wako kwa Tz?

Hint: Tumeona body ya wahandisi, wahasibu, boharia, wanasheria (refer to Ms. Karume issue)n.k jinsi wanavyoplay role yao collectively. Ni lini sisi wachumi tutaplay part yetu?

Nakaribisha maoni hapo na pia kwenye PM yangu
 
Kuna watu wameniuliza, kwa nini tusiendeleze Tanzania Economic Forum
kwa wanaotaka kuifahamu vizuri zaidi tembelea http://tanzaniaeconomicforum.org/ angalia katiba yao na jiulize tangu kuan´zishwa kwake wamefanya nini? Na angalia viongozi wake nadhani ni wafanya biashara (ndio maana imesajiliwa kama kampuni) ila naweza kusema mallengo yake ni sahihi na ni tofauti na Bodi hiyo itakayoanzishwa kwa maana ya kazi zake.

maoni yako ni muhimu kwa mchakato huu
 
Bravo Bowbow,

Ni kweli hicho chombo ni muhimu, kwani tunahitaji bodi hiyo itusaidie kwenye mambo yafuatayo

1. Kufanya tafiti mbalimbali kwenye nyanja zenye utata especially economic interests.

2. Kuongoza mijadala na makongamno ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii mambo ya kiuchumi

3. Kukusanya taarifa mbalimbali na kutoa vielelezo muhimu vya uchumi kwa umma na serikali

4. Kuendeleza jamii ya wachumi pamoja na wanafunzi wanojiunga na fani hiyo

5. kama ulisema kwenye post zako.
 
Nakumbuka siku za nyuma kuna Chama cha wachumi Tanzania. Nakumbuka pia walikuwa na ofisi huko mjini maeneo ya posta lakini sijui hiki chama kiliishia wapi. Nitawacheki wa jamaa wa Idara ya uchumi wa mlimani wanaweza kuniambia zaidi kuusu hili. Ni muhimu sana kuwa na chombo kama hiki sio kwa ushauri tuu bali hata kwa kuandika makala mbalimbali za uchumi, kutoa mawazo yao kuhusu sera za kiuchumi, kuchanganua budget marainaposomwa bungeni. Naamini chombo kama hihi ndio kingekuwa kinatoa analysis ya budget kuliko ilivyo sasa kusubiri Deloite kutoa. Jamani ni wazo zuri sana kwa wachumi mlioko nyumbani mnaweza kulifanyia kazi.
 
Nakumbuka siku za nyuma kuna Chama cha wachumi Tanzania. Nakumbuka pia walikuwa na ofisi huko mjini maeneo ya posta lakini sijui hiki chama kiliishia wapi. Nitawacheki wa jamaa wa Idara ya uchumi wa mlimani wanaweza kuniambia zaidi kuusu hili

Nilikuwa bongo last summer na Niliongea na 3 senior lecturers na wote waliwahi kuwa wakuu wa idara ya uchumi kwa nyakati tofauti na walisupport sana hiyo idea ya Bowbow.

Kinachoonekana ni nani aanzishe. Mimi kwa sasa nasoma na ninataka kuandika thesis yangu kwenye suala la madini Tanzania But siwezi kupata literature yeyote online hadi ulipie tena firms za kimarekani.

Je kungekuwa na hiyo organisation ingekuwa rahisi kupata reaserch findinds/report kutoka kwao maana wangekuwa wanafanya research.

Naomba kama kuna mtu mwenye policy documents, past researches on mining sector in Tanzania anipatie, asanteni
 
Nilikuwa bongo last summer na Niliongea na 3 senior lecturers na wote waliwahi kuwa wakuu wa idara ya uchumi kwa nyakati tofauti na walisupport sana hiyo idea ya Bowbow

Fundi wa KKt,
Nimemtumia email mkuu wa idara ya uchumi, mlimani, Tumaini, Mzunmbe, IFM, chief economists, kwenye wizara za serikali(kwa zile ambazo nimepata contact zao), baadhi ya wachumi ninao wafahamu, please kama unamfahamu mchumi yeyote mjulishe na sikia maoni yake. JK kama mchumi nae anakaribishwa ili aweze kupata msasa wa maswala ya kichumi pale bodi itakapoanzishwa
 
Just to inform you what is happening behind the curten

Nimepokea response nyingi sana kupitia email yangu na kuna support kubwa sana na kuna habari zisizo rasmi(kuwa hata mkuu wa kaya anasupport and he is more than willing to finance for he first meeting). Ni Habari kutoka kwa naibu waziri mmoja ambaye pia ni Mchumi

Nimepokea email kutoka kwa baadhi Watanzania waliopo China na Japan wamesema wanasupport na watatoa mchango wao kwa kutengeneza website ya bodi hiyo na watalipia hosting fee ya mwaka.

Pia kuna email kutoka kwa wadau mbalimbali kwa ujumla wanapenda bodi hiyo ianzishwa hata leo hii. So far nimepata emails 138 watu wanaoiunga mkono, 53 bado wanahisi(hesitant) bodi hiyo haitaleta mabadiliko so haihitajiki, 9 totally rejected the idea.
Ikumbukwe haya na maoni kutoka kwenye email niliotuma kwa watu 98, hivyo kusambaza kwa watu wengine hadi kufikia hiyo idadi ya watu 200 hadi leo saa nne asubuhi.

Hivyo endelea kufuatilia hapa kuona nini kinaendelea na maoni yako yanakaribishwa ili kujenga uchumi imara wa Tanzania kwa faida ya Watanzania wote
 
Hi wanaJF msichoke kwa updates.

Naendelea kupata email kutoka sehemu mbali mbali na kuna ndugu zetu watanzania waliopo KPMG and Estern & Young Tanzania wamejitolea kuandaa draft constitution/Memorandum of Associtiation ya Bodi hiyo ya wachumi.

Kikubwa ambacho ni challenge ambayo naleta kwenu ni muundo wa body hiyo pamoja na kazi zake ikiwa kuna wanaosema bodi hiyo iwe na mamlaka ya kuhakiki na kutoa kibali/license za wachumi katika kada mbali kwa kotoa mitihani au iwe ni kusajili tu pale anapokuwa amemaliza cheti, shahada, stashahada au falsa ya uchumi.

Maoni yenu yanakaribishwa
 
Naomba wale wanoweza kutuma maoni moja kwa moja hapa JF
watumie hii thread maana kuna watu wengine wanapenda kuona maoni yenu naomba mfanye hivyo kuliko kwenye email yangu.
 
Hay ni baadhi ya matatizo tutaendelea kuface kama juhudi ya kuanzishwa hazitafanyika soma hii habari....Mixed feelings over the EAC-EU deal

2007-12-02 10:20:43
By Darius Mukiza

Tanzanian trade experts have received with mixed feelings the Economic Partnership Agreement (EPA) trade deal signed between the East African Community and the European Union last Tuesday in Kampala.

Despite commending the efforts made so far by the bloc, the experts have expressed fears that the East African member states will lose under the arrangement compared to those from Europe.

``Our goods do not meet the criteria set by the European countries,`` remarked Dr George Lindi, a senior lecturer in the faculty of Commerce and Management at the University of Dar es salaam.

``This means the deal aims to kill not only the external market for Tanzanian goods but also the local ones``.

Dr Lindi said the government will also lose revenue from the adverse competition.

He said the situation will benefit the EU countries more since they will be selling more to the EAC market.

He said the EU Common Agricultural Policy requires each country to import goods of a certain standard which Tanzania cannot meet.

The expert noted that Tanzanian goods will lose even the local market since EU goods will be sold cheaply in Tanzania.

Dr Lindi called on the government to make a thorough study before implementing the programme.

He said experts are available to contribute to the study. On his part Dr Haji Semboja of Economic Research Bureau required common understanding before the implementation by the East African Countries.

``There is a need for a common understanding between the East African countries on the quantity of goods to be imported and exported,``he said.

He added that the private sector is the only guarantor for fair trade dealings.

He called on the government to work closely with it. Dr Semboja pointed out that the deal will precipitate competition in locally manufactured agricultural products, in the light of their relatively lower standards compared with those of the European countries.

On his side the Minister for Trade, Industry and Marketing, Basil Mramba, said Tanzanians need not worry about their country`s position in the Economic Partnership Agreement (EPA) for it will benefit them.

``Failure to sign the agreement, Tanzanian goods entering the EU market would face 18 per cent duty charges at a time when the other East African member countries will export to the market under Free Trade Area (FTA)

He explained that EU understands the need for economic and development cooperation with EAC countries. It affirmed its commitment to ensure the EPA enhances development in the region.

The interim agreement includes a list of agricultural and industrial products that the EAC considers sensitive and in need of temporary protection to prevent local companies going bust.

SOURCE: Sunday Observer
 
Wazo zuri,hapa USA kila kitu kina bodi na ndizo zinafanikisha mambo mengi.Mimi nafikiria bodi yakusaidia miundombinu ya shule na vyuo huko Tanzania.Alumnus wakishirikishwa vizuri wanaweza kusaidia shule na vyuo walivyosoma
 
Bowbow

Excellent Idea!

nakuunga mkono, kama hii kitu haikuwepo, it is high time now kuanzishwa
 
Wakubwa heshima mbele.
Pamoja na kuunga hoja ya mheshimiwa Bowbow ,nami nina hoja ambayo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikiniumiza kichwa.

Hoja yenyewe ni kuwa,kwa mtanzania aliye na ajira ,iwe ni ya serikalini au mashirika binafsi,ni kwa nini kusiwe na utaratibu wa kumlipa sehemu ya fedha yake ya NSSF katika interval say ya miaka hata minaneminane ili imsaidie katika kujiletea maendeleo,badala ya kumshawishi kuomba mikopo kutoka mabenki ambayo yana riba kubwa?

Maana yangu kubwa ni kuwa,mtu hutengeneza maendeleo yake akiwa na mtaji wa kutosha ili aweze kufanya miradi endelevu pasi na kukabiliwa na riba.
Kwa mfano,say,mtu ana NSSF ya Tshs. 10,000,000 katika kipindi cha miaka saba au nane ya utendaji kazi wake,kama anakopeshwa sehemu ya pesa hiyo huku akiendelea na ajira anaweza kujifanyia maendeleo yake kuliko kukaa bure huku michango yake hiyo ikiendelea kutumiwa na watu au shirika la umma kwa kuendeleza majumba ya kupangisha kwa faida kubwa bila wenye michango yao kunufaika na chochote.

Kwa mtazamo wangu,huo ni upungufu wa kisera ambao humdidimiza mwenye mchango wake hali ya kuwa ni stahili yake kuutumia katika maisha yake ya kila siku.

Maisha yanatengenezwa leo na siyo kesho,hivyo imekuwa ni sera ya serikali na chama tawala kutoa mafao na kuandaa michango ya wa ajiriwa katika kipindi cha kustaafu kwao huku wakiishia kukubana tena ukae baada ya miezi sita kutoka tarehe ya kustaafu ndipo upate miachango ya NSSF yako,huo ni ufisadi mwingine wa aina yake kwa mwananchi amabaye siyo wa kundi ,nasema kundi lao nikimaanisha hao watunga sheria nakuzipitisha wakiacha watu wakitaabika baada ya kustaafu wakati wao hupata mafao yao kwa mamilioni fasta fasta baada ya kipindi cha miaka mitano nadni ya jumba kuu la Bunge.

Nimeshuhudia baadhi ya wastaafu wakiambulia kupewa mifuko ya cement eti ndio wakajenge baada ya kulitumikia taifa/kustaafu ikiwa ni kama heshima ya utumishi wao uliotukuka.Hii ni sawa na kumpa mstaafu cement akajengee KABURI lake kwa maana ya kutokuwa na kiwanja.

Hoja ya msingi kwa uelewa wangu mdogo,KODI wakate kwa sababu bila kodi nchi haiwezi kuendeshwa ,lakini michango yetu tupewe ili tujifanye maendeleo yetu.

Naombeni msaada wa kimawazo na pia sina hakika sana kama hoja hii iko mahala pake.

Asanteni sana,

Na ninaomba kuwakilisha.
 
Kwa upande wangu naona mwanzilishi amekosea kidogo. Kuna taaluma ambazo zinahitaji kupata kibali cha kufanyia kazi baada ya kumaliza masomo. Miongoni mwa hizo taaluma ni sheria, udaktari nk. Hivyo kuwepo kwa bodi kuna umuhimu wake. Lakini kuna taaluma zinazoweza kuwepo bila bodi.

Kwa mfano, kuna bodi wahandisi Tanzania, lakini chombo hiki kazi yake kubwa ni kusajili hili mhandisi apate kibali cha kufanya kazi ya aina fulani. Katika uhandisi kuna scientific principle ambazo mtu anajifunza akiwa shuleni na norms ambazo zinafuatwa na mhandisi akiwa kazini. Kwa mfano fundi umeme anajifunza kuwa waya shaba unapitisha umeme vizuri (scientific principle). Lakini akiwa kazini, mhandisi anatakiwa ajue umbali wa waya za simu na umeme wa kutumia (norms). Bodi mara nyingi zinafuatilia matumizi ya norms. Hivyo mhandisi anayetoka katika nchi zinatotumia 220V atakuwa na norms zake na yule anayetoka 110V anatakuwa na norms zake.

Mhasibu anajifunza taaluma ya uhasibu akiwa shuleni. Lakini akiwa kazini ni lazima aelewe sheria za nchi au mashirika zinavofanya kazi katika taaluma yake ya uhasibu. Kuna sheria za kodi, kuna sheria na kuunganisha mashirika n.k Taaluma ya uhasibu ni sawa dunia lakini jinsi unavyofanyia kazi katika nchi mbalimbali ni tofauti na hapo ndio umuhimu wa bodi unapokuja.

Mchumi, mwana-hisabati au computer programmer hawana mipaka kama taaluma zingine. Na kuwawekea bodi ni kutwanga maji.

Kinachotakiwa kwa taaluma kama hizi ni taasisi ambazo zitawapa nafasi wahusika kuendeleza taaluma zao na majukwaa ya kusema. Na hizo taasisi zisiwe za kiserikali hili kuongeza uwazi.

Vile vile tukumbuke kuwa uchumi sio rocket science ya kuwa na mawazo ya aina moja. Wakati wa Nyerere kuliwezekana kuwepo kwa chombo hicho kwa sababu wachumi wote walilazimika kufuata Jembe na Nyundo.

Kwa kipindi cha sasa ambacho wachumi wa shule mbalimbali za mawazo wanajitokeza ni jukumu la wachumi wenyewe kuanzisha taasisi binafsi au zisizo za kiserikali kueleza na kendeleza ukuaji wa mawazo yao. Itakuwa ni makosa makubwa kuwa na chombo kimoja cha kiserikali kama enzi Nyerere.

Mwanzilishi wa thread hii kwa sababu umeona upungufu huu ingekuwa vizuri uanzishe taasisi.
 
  • Thanks
Reactions: GKM

Mwana wa Mariam,

Good comment, Bodi hii itakayoanzishwa sio lazima iwe na muundo kama uliosema wewe na kazi kuu za bodi sio kusajili na kudahili.

Uchumi nao unaprinciples zake kama ilivyo taaluma ingine na pia kama ulivyosema kumekuwa na school of thought nyingi kila kukicha, Hivyo sio kila linakuja linafaa kwa mazingiza ya chumi zetu (LDC).

Lakini pia ujue hichi chomba hakitakuwa chombo cha serikali kama ulivyofikiria, Hii itakuwa independent Board sijui taratibu za huko Bongo kuanzisha hiyo board.

Thank you your comment, maana nalo ni suala ambalo lipo mezani kwa discussion.
 
Kuna taasisi binafsi huko bongo inayoitwa HAKI ELIMU. Ilisajiliwa kama taasisi binafsi. Na ilisimama imara kuishinikiza wizara ya elimu na iliingia kwenye migogoro na serikali.

Kama HAKI ELIMU waliweza sioni sababu kwanini wachumi wasiweze. Na kuna mada nyingi tu za kutoa.

Na kama una mpango wa kuanzisha taasisi ya uchumi inayofuata shule ya mawazo ya Milton Friedman naona unijulishe.
 
Ndugu wana JF
Sio lazima uwe mchumi ili uchangie hoja hii bali kila mmoja anakaribishwa kutoa mawazo yake
Muundo wa hiyo bodi maana itawasaidia watu wobila kuja dini, kabila, proffession, umri wala rangi. Therefore maoni yenu ni muhimu sana. wote mnakaribishwa
 
Nimekuwa nikifuatilia mada hii kwa kipindi. Nakanganywa na maswali machache, ambayo ningependa kueleweshwa.

1. Mlaji (consumer) wa huduma za bodi hii ni nani au atakuwa nani?

Nauliza hili kwa sababu mfumo mzima wa shughuli za kiuchumi na maendeleo Tz bado haujaruhusu matumizi huru na yamanufaa ya wachumi(na wasomi wa fani mbalimbali). Tukumbuke kwamba kwa mazingira ya sasa ya TZ mtumiaji/mlaji mkubwa wa fani ya uchumi ni serikali. Wachumi wa vyuo vikuuu ndio wanaotumiwa na serikali katika tafiti mbalimbali kwa njia za contracts. Sasa bodi hii inapoanzishwa ni vyema tukajiuliza endapo uwapo wa wachumi katika vyuo vyetu na contracts zao zinazotosheleza mahitaji ya mlaji mkuu (serikali)vitashabihiana na malengo ya bodi.

Kwa maneno mengine, je bodi hii inaanzishwa na mlaji wa huduma zitakazotolewa ama msambazaji wa huduma. Nina shaka kwamba bodi hii inatokana zaidi na supply kuliko demand, na hivyo inaweza isidumu.

2. Bodi ya uchumi kama zilivyo board nyingine za utafiti sio lelemama. Je nani ata finance shughuli za tafiti za kila siku? Au itakuwa ni board ya ushauri wa kiuchumi husiotokana na utafiti?

3. Nini hasa kazi (products) ya bodi hii katika maendeleo ya Tz? Je ni kutoa vibali kwa grads wa fani ya uchumi tu?

4. Bodi hii itachukuwa sura gani? Chombo cha kujitegemea cha serikali? NGO? Economic association? Private economic consultants?

Nadhani kabla hatujadandia gari kwa mbele ni bora tukaanza na maswali haya. Na katika kujibu maswali haya ni nashauri mjadala huu uwe na mtiririko ufuatao:

(a) Kwa sasa tatizo liko wapi
(b) Kwa sasa tatizo hilo linatatuliwa vipi pasipo kuwapo bodi
(c) Huduma zitakazotolewa na bodi
(d) Nani mlengwa/mlaji wa huduma za bodi
(e) Nani ata finance bodi
(f) Athari za bodi kwa wachumi binafsi wa vyuoni wanaotoa huduma sawa na zitakazotolewa na bodi
(g) Muundo wa bodi (NGO, consultants etc)
(h) Ukubwa/idadi ya walaji wa huduma za bodi
 
Nilikuwa bongo last summer na Niliongea na 3 senior lecturers na wote waliwahi kuwa wakuu wa idara ya uchumi kwa nyakati tofauti na walisupport sana hiyo idea ya Bowbow.

Kinachoonekana ni nani aanzishe. Mimi kwa sasa nasoma na ninataka kuandika thesis yangu kwenye suala la madini Tanzania But siwezi kupata literature yeyote online hadi ulipie tena firms za kimarekani.

Je kungekuwa na hiyo organisation ingekuwa rahisi kupata reaserch findinds/report kutoka kwao maana wangekuwa wanafanya research.

Naomba kama kuna mtu mwenye policy documents, past researches on mining sector in Tanzania anipatie, asanteni

FundiwaKukeketa, mtafute Zitto Kabwe atakuwa na dosier kamili ya sekta ya madini.
 
BowBow,

Naomba kuongeza kwenye hoja ya MgonjwawaUkimwi kuwa unapoanzisha chombo chochote iwe kampuni, tasisi, NGO, bodi, etc fikiria ni wapi pesa za kuendesha hicho chombo zitapatikana.

Je mtakuwa mnauza service zenu? If yes, kwa nani? Na je mmeshaonana na hao potential clients kupata goodwill yao ili msianze kuhangaika kazi ikianza?

Kama ni taasisi itakayokuwa financed kwa michango ya hiari basi hapo ni kiasi cha kuwapa proposal hao donors kupata support na pesa kabisa upfront.

Ila msianzishe chombo cha kuja kuextort wasomi wa uchumi hapo baadae kuwa ili wafanye kazi za uchumi ni lazima wawe na cheti chenu. Hapo mtakuwa hamjengi kwa kuwa uchumi kama alivyosema Mwana wa Maryam hauna mipaka kiivyo kama uhasibu, au uhandisi.

Siku zote anza na source of money. Ukishapata uhakika wa pesa watendaji wa kufanikisha mambo utawapata tu. Pesa huwa inaongea.
 
Back
Top Bottom