Ni bora ukahesabia kuwa kila kilichokuwa kikiendelea katika nchi hii kabla ya awamu ya nne kuacha uteuzi ambao ulifanyika mpaka sekunde ya mwisho kilikuwa VOID. Ushahidi ni maneno na matendo ya awamu ya tano.
Ngoja tungoje na tuone wale walioamini kuwa mabadiliko yanawezekana kwenye ccm iliyoishiwa pumzi ikiwa na Dr. Magufuli aliye hai japo kuna wanaodai kuwa Ukawa walichaguliwa na wananchi.
Kwani hiyo bodi iliyohusika na uteuzi iliundwa lini na inamaliza muda wake lini?Unajuaje kama haijamaliza muda wake na iliyopo sasa ni bodi mpya??????????Na kwanini usisubiri uchunguzi ukamilike kwanza na kama huyo Bade hana makosa ujue.....................why bodi haikuvunjwa?
Umesoma hayo maoni ya K.Msese ?
Sikusudii kubadilisha maada lakini bodi kwenye mashirika mengi ya umma Tanzania ni kichekesho. Mfano ni kwamba mwenyekiti wa bodi ya BoT ni Gavana mwenyewe ambaye bodi inatakiwa imsimamie.
Kwa TRA, Kamishna na msaidizi wake wanateuliwa na Rais. Ina maana bodi haina mamlaka ya kumuwajibisha. Labda kupeleka mapendekezo kwa Rais ambaye anaweza kuyapuuza. Maana yake ni kwamba bodi ipo kama boya tu.
Maana sioni kama kuna time frame kuwa hadi muda Fulani Bodi iwe imeshavunjwa, ama nini kiinatakiwa kuanza kushughulikiwa kwanza au nini kiwe cha mwisho given kuwa sakata ndani ya tra bado linaendelea!
Mkuu Sibonike
hivi uliona hivyo vyeo vya kina masamaki na blandina?
na wao ni makamishna wanaoteuliwa na bodi....
kamishna wa kodi-masamaki
kamishna wa nini sijui-blandina
ajabu sana
Huoni bodi kumteua 'mtuhumiwa' wa upotevu wa makonntena
moja kwa moja wanajua wanachokifanya?
why wao bodi wasichunguzwe?
Kuna uzi niliweka hapa kuhusu kina nani wanafaa ku run economy hivyo Magufuli amteue mmoja wao...katika list hiyo alikuwepo Rishad Bade.....sasa baada ya skendo la makontena TRA baadhi ya watu wamekuwa wakiniuliza kama Rishad Bade nilikosea kumtaja katika list hiyo na mwingine ni Harry Kitilya.Sasa wakati natafakari yaliyotokea TRA.
Hapa JF kuna uzi wa mkuu R.B wa mwaka 2013, kwenye huu uzi kuna mambo yamejitokeza yamenishangaza sana.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-kwa-tuhuma-makontena-kupotea-mikononi-2.html
Kumbe bodi ya TRA inateua watendaji na ilimteua Masamaki huku akiwa tayari ana tuhuma za kupotea ka makontena mengine.Nna sio hilo tu kamati ya bunge ililiona hilo na kuihoji Bodi kwa maamuzi hayo mtu mwingine ambae nae inaonekana bodi ya TRA ilimteua ni Blandina Nyoni.
Sasa kama bodi kwanza ina nguvu hivyo ya kuteua watendaji halafu pili watendaji wenye tuhuma tayari...ilikuwa ni busara kumuwajibisha Kamishna wakati mamlaka kamili ya kuteua watendaji wa chini yake yako bodi,na bodi imeachwa kama ilivyo?
Pili hii structure ya TRA ambapo kamishna anateuliwa na Rais na naibu pia na Rais halafu watendaji wa chini yake wanateuliwa na bodi nani ali design hii?
Inawezekana kweli kamishna akawa na nguvu TRA huku anateuliwa watu? na mamlaka ambazo ziko juu yake? Rais na Bodi?
Na kama hizi tuhuma sio mpya labda uchunguzi ungefanyika wa mda mrefu wa tatizo hili? kontena zimepungua kupotea au zimezidi baada ya Bade kuteuliwa?
What if zimepungua sana despite the fact hana nguvu kuliko Bodi?
Why bodi iteue watuhumiwa?
Je, wajumbe wa bodi ya TRA wanachunguzwa?wamehojiwa? why bodi haijavunjwa?
Ikidhihirika Bade alikuwa hahusiki kabisa na alikuwa anapambana na 'powerful forces' kumaliza hilo tatizo atarudishwa? Ataombwa radhi kwa kuchafuka?
1. Umejuaje au una taarifa zipi kuwa bodi haichungizwi?
2. Makosa ya bodi yanaonekana dhahiri, je mwenzetu una uhakika au taarifa yeyote kuwa sakata la TRA limeshamalizwa ili isemwe mbona wale wachafu wameachwa?