Bodi ya Mikopo yawakana wanafunzi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Bodi ya Mikopo yawakana wanafunzi

na Fauzia Hassan na Magreth Mkwera

amka2.gif
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (HESLB) imesema haitoongeza kiwango cha mikopo hata wanafunzi wakiandamana kwenye ofisi zake. Msemaji wa bodi hiyo, Veneranda Malima, alisema hawawezi kuongeza viwango vya mikopo kwa sababu ada iliyopandishwa na vyuo vikuu hawaitambui Alisema bodi hiyo inatambua viwango vya ada ilivyopewa na serikali mwaka 2008/2009 hivyo ongezeko lolote la ada litakalotokea litapaswa adaiwe mwanafunzi na si bodi.
Alibainisha kuwa serikali ilitoa maelekezo hayo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na vyuo vyote lakini vyuo vimekaidi agizo hilo na vimeamua kuongeza ada mara dufu.
Aliongeza kuwa vyuo hivyo sasa vinawashawishi wanafunzi wao kwenda kwenye bodi ya mikopo kudai nyongeza ya ada.
“Wanafunzi hata wakiandamana kuja kwetu haitasaidia chochote, bodi haitotoa hata senti tano nje ya viwango vilivyoelekezwa na serikali,” alisema Malima.
Malima aliongeza kuwa Desemba 16, mwaka huu, wanafunzi wapatao 4000 kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) waliandamana katika ofisi za bodi hiyo.
Alisema wanafunzi hao walikuwa wakitaka bodi ilipe ongezeko la ada katika vyuo hivyo tofauti na maelekezo ya serikali.
Kuhusu kucheleweshewa mikopo, Malima, alisema kuwa hadi sasa wanafunzi wote ambao maombi yao ya mikopo hayakuwa na hitilafu wameshapata mikopo yao kwa wakati isipokuwa wachache waliokuwa na matatizo.
Wanafunzi wanaotakiwa kupewa mikopo ya mafunzo, bodi hiyo imesema kuwa watapata fedha hizo mara baada ya kupata taarifa na orodha kutoka vyuoni ikieleza wanaenda sehemu gani na lini.
Aliongeza kuwa mikopo ya mafunzo kwa vitendo itatolewa kwa programu ambazo vyuo vimezibainisha katika mitaala kwamba vinahitaji mafunzo kwa vitendo na si vinginevyo.
Bodi hiyo imesema imeamua kutoa ufafanuzi huo kutokana na kuwapo kwa upotoshaji wa mikopo wanayoitoa ikiwemo wanafunzi kuandamana kila mara kwenda kwenye ofisi za bodi hiyo
 
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (HESLB) imesema haitoongeza kiwango cha mikopo hata wanafunzi wakiandamana kwenye ofisi zake. Msemaji wa bodi hiyo, Veneranda Malima, alisema hawawezi kuongeza viwango vya mikopo kwa sababu ada iliyopandishwa na vyuo vikuu hawaitambui Alisema bodi hiyo inatambua viwango vya ada ilivyopewa na serikali mwaka 2008/2009 hivyo ongezeko lolote la ada litakalotokea litapaswa adaiwe mwanafunzi na si bodi.
Alibainisha kuwa serikali ilitoa maelekezo hayo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na vyuo vyote lakini vyuo vimekaidi agizo hilo na vimeamua kuongeza ada mara dufu.
Aliongeza kuwa vyuo hivyo sasa vinawashawishi wanafunzi wao kwenda kwenye bodi ya mikopo kudai nyongeza ya ada.

Tatizo hapa ni uratibu mbovu wa Wizara ya Elimu kwani haiwezekani kila mmoja afanye atakavyo........................lazima iwepo sera moja inayoeleweka juu ya upandishaji wa ada ya elimu ya juu ili mkanganyiko wa namna hii usitokee.......i.e sera hiyo ionyeshe ni asilimia ngapi kwa mwaka inaruhusiwa kuongezeka kwa ajili ya inflation tu..........lakini jinsi mambo yalivyo serikali haina ujanja lazima iongeze fungu la mfuko huu kuziba pengo lililojitokeza bali kuendeleza malumbano hakuna anayefaidi.................
 
Ni kweli kabisa Ruta, kosa ni la wizara husika,ilibidi lazima iweke sera kuhusu upandishaji wa ada kwamba chuo kikitaka kupandisha ada basi kipeleke mchanganuo wake wizarani then wizara kwa kushirikiana na chuo wanafikia muafaka kisha wizara inapeleka ada mpa bodi. Kwa jinsi ilivyo sasa kila chuo kinakurupuka tu kwa sababu hakuna sera maalum na matokeo ndio haya. Hii ndio Tanzania
 
Back
Top Bottom