Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ( HESLB) imetengeneza chuki kubwa kwa riba ya asilimia 15%

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Wanabodi, Moja kati ya ukatili uliofanyika na kuwaumiza watumishi wa uma na sekta binafsi ni tamko la Kuongeza riba ya mikopo ya wanafunzi kutoka asilimia 8% mpaka 15%

Vyama vya wafanyakazi na wadau wapaze sauti kuhusu riba hii ya asilimia 15% kwa vijana wetu kushushwa.Haya maamuzi ya kupandisha yalifanywa na mtu mmoja bila kushirikisha wadau ambao ni waajiri na vyama vya wafanyakazi

Serikali hata ikiongeza mishahara watumishi wa uma ni sawa na sifuri kwa sasa. Kwani mshahara ukiongezeka na makato ya Bodi ya mikopo ya wanafunzi inaongezeka.

Ni wakati muafaka Mama Samia kubadili ule uamuzi uliofanywa na mtangulizi wake kwa kupunguza riba ya mikopo ya wanafunzi.

Hotuba ya Mama Samia hata akisema Bungeni ataongeza mishahara bado hilo ongezeko litakatwa riba ya asilimia 15% ya Bodi a ya mikopo.

Kijana aliyeanza kazi na mshahara wa TZS 1,600,000 Graduate anakatwa karibu TZS 240,000 ya Bodi ya mikopo, Hapo bado kodi ya Paye, Bado NSSF. Hata ukimuongeza huyu kijana mshahara mpaka TZS 1,800,000 mambo ni yale yale tu.

Tuwaunge mkono vijana wetu kupaza sauti wanaumia sana na riba ya asilimia 15%.

Serikali ijaribu kushusha riba hii.

Tamko lolote la Kuongeza mishahara kwa watumishi wa uma halitakuwa na maana kama bado deni la Bodi ya mikopo litabaki asilimia 15%.
 
Mwenyezi Mungu akinijalia afya na uzima tele, nitahakikisha watoto wangu kamwe hawaangukii kwenye huu unyonyaji wa hawa wadhulumaji wa ccm wanaoitwa Bodi ya Mikopo.
Sasa inabidi watanzania tubadilike, tuanze kufungua akaunti za akiba kwa ajili ya watoto na siyo kusubiria mikopo. Mkopo uje uwe ni suluhisho la mwisho.

Ukijiwekea mpango wa akiba kwa kweli utapunguza machungu kwa kiasi kikubwa.

Waswahili wamesema: Haba na haba hujaza kibaba.
 
Ndugu yangu, ujue mikopo ni sehemu ya biashara ndio maana Kuna hiyo riba hawakukopeshi kwa lengo tu la kukunufaisha Bali ata wao wapate faida.Ukitaka kuepukana na kadhia hiyo weka malengo ya mda mrefu ili usiingie kwenye mikopo kwani ata mafundisho ya dini yanasema kuwa mkopo ni haramu.

Hakikisha unajipanga mapema kuwasomesha watoto ila mikopo ni janga atakopeshwa atasoma atasota mtaani kwa kuwa kwa Sasa kusoma na kuajiriwa ni sawa na mbingu na ardhi mwisho was siku utakuwa na Cha kurudisha.
 
Ndugu yangu, ujue mikopo ni sehemu ya biashara ndio maana Kuna hiyo riba hawakukopeshi kwa lengo tu la kukunufaisha Bali ata wao wapate faida.Ukitaka kuepukana na kadhia hiyo weka malengo ya mda mrefu ili usiingie kwenye mikopo kwani ata mafundisho ya dini yanasema kuwa mkopo ni haramu. Hakikisha unajipanga mapema kuwasomesha watoto ila mikopo ni janga atakopeshwa atasoma atasota mtaani kwa kuwa kwa Sasa kusoma na kuajiriwa ni sawa na mbingu na ardhi mwisho was siku utakuwa na Cha kurudisha.
Mkopo unatolewa na Bodi ya mikopo siyo mkopo wa kibiashara. Awali hali ilikuwa fresh, ila marekebisho yaliyofanyika mwaka 2016 yalikuwa ya hovyo sana, kiwango cha marejesho kwa mwezi kilitoka asilimia 7% iliyokuwepo kwenye mkataba hadi asilimia 15%, ikaingizwa faini ya 10 % mtu akishindwa kuanza marejesho kwa muda, na value retention fee ya asilimia 7 hivi. Masharti haya mapya yaliharibu maafikiano ya mkataba wa mkopo kwa asilimia kubwa.
 
Balaa kubwa la Bodi Ya Mikopo (HESLB) sio sasa hivi, subirini hao waliopewa hio mikopo ambao wapo darasani wamalize vyuo (Watakao Disco & Supp - Na waliohukua Course Za Education, Agriculture, Certificate In Avocado Farming), halafu wakutane na hio riba takatifu ya 15% na penalty jumlisha hakuna ajira. Kasheshe ndio litakapo pamba moto kisawasawa.

Wanaomtukana Magufuli sasa hivi ni wachache sana, na wanaonekana wendawazimu. Ila hao watakao maliza vyuo ndio akili zitawakaa sawa na kuelewa kwamba yule Marehemu na CCM yake walilaaniwa (Wanaomchukia wataongezeka kwa 99%).
 
Ndio maana wengine hatuipendi kabisa CCM kwani ni chanzo cha umasikini wa hii nchi na watu kwa kuwa na sera mbovu,kulea wizi na ubadhirifu serikalini, n.k.

Sheria hii ni moja ya sheria mbovu na katili sana kwa waajiriwa wa serikali na wale wa sekta binafsi.
 
Unapochagua mbunge wa Ccm jua umepotea, wao ndio walipitisha hii sheria kandamizi!
 
Wanabodi, Moja kati ya ukatili uliofanyika na kuwaumiza watumishi wa uma na sekta binafsi ni tamko la Kuongeza riba ya mikopo ya wanafunzi kutoka asilimia 8% mpaka 15%

Vyama vya wafanyakazi na wadau wapaze sauti kuhusu riba hii ya asilimia 15% kwa vijana wetu kushushwa.Haya maamuzi ya kupandisha yalifanywa na mtu mmoja bila kushirikisha wadau ambao ni waajiri na vyama vya wafanyakazi

Serikali hata ikiongeza mishahara watumishi wa uma ni sawa na sifuri kwa sasa. Kwani mshahara ukiongezeka na makato ya Bodi ya mikopo ya wanafunzi inaongezeka

Ni wakati muafaka Mama Samia kubadili ule uamuzi uliofanywa na mtangulizi wake kwa kupunguza riba ya mikopo ya wanafunzi

Hotuba ya Mama Samia hata akisema Bungeni ataongeza mishahara bado hilo ongezeko litakatwa riba ya asilimia 15% ya Bodi a ya mikopo

Kijana aliyeanza kazi na mshahara wa TZS 1,600,000 Graduate anakatwa karibu TZS 240,000 ya Bodi ya mikopo, Hapo bado kodi ya Paye, Bado NSSF. Hata ukimuongeza huyu kijana mshahara mpaka TZS 1,800,000 mambo ni yale yale tu

Tuwaunge mkono vijana wetu kupaza sauti wanaumia sana na riba ya asilimia 15%

Serikali ijaribu kushusha riba hii

Tamko lolote la Kuongeza mishahara kwa watumishi wa uma halitakuwa na maana kama bado deni la Bodi ya mikopo litabaki asilimia 15%
Mama Samia asipo lizungumzia hili ktk address yake leo...it will be a hopeless address to the HESLB victims..
 
Unapochagua mbunge wa Ccm jua umepotea, wao ndio walipitisha hii sheria kandamizi!
Bunge Zima lilikuwa Bribed na Jiwe wakapitisha hii sheria ya kishetani kabisa. Hata makina Lema na Mbowe yalikuwepo.
 
Ndugu yangu, ujue mikopo ni sehemu ya biashara ndio maana Kuna hiyo riba hawakukopeshi kwa lengo tu la kukunufaisha Bali ata wao wapate faida.Ukitaka kuepukana na kadhia hiyo weka malengo ya mda mrefu ili usiingie kwenye mikopo kwani ata mafundisho ya dini yanasema kuwa mkopo ni haramu. Hakikisha unajipanga mapema kuwasomesha watoto ila mikopo ni janga atakopeshwa atasoma atasota mtaani kwa kuwa kwa Sasa kusoma na kuajiriwa ni sawa na mbingu na ardhi mwisho was siku utakuwa na Cha kurudisha.
Unajua makubaliano Kati ya HESLB na wanufaika yalivyokuwa,kabla ya Utawala wa Farisayo(Magufuli)?
Au unadhani Kuna mtu alisaini riba ya 15%?
 
Waambie chama chako warudishe makato asilimia 7 sio unajichekelesha tu hapa jukwaani
Mshikaji wangu toka ameanza kulipa deni haliishi, alikopeshwa 13m ila sasa deni liko 14m na amelipa karibu miaka 6, bodi hawana maana.

Nashukuru sana niliepuka huo msala.
 
Wanabodi, Moja kati ya ukatili uliofanyika na kuwaumiza watumishi wa uma na sekta binafsi ni tamko la Kuongeza riba ya mikopo ya wanafunzi kutoka asilimia 8% mpaka 15%

Vyama vya wafanyakazi na wadau wapaze sauti kuhusu riba hii ya asilimia 15% kwa vijana wetu kushushwa.Haya maamuzi ya kupandisha yalifanywa na mtu mmoja bila kushirikisha wadau ambao ni waajiri na vyama vya wafanyakazi

Serikali hata ikiongeza mishahara watumishi wa uma ni sawa na sifuri kwa sasa. Kwani mshahara ukiongezeka na makato ya Bodi ya mikopo ya wanafunzi inaongezeka

Ni wakati muafaka Mama Samia kubadili ule uamuzi uliofanywa na mtangulizi wake kwa kupunguza riba ya mikopo ya wanafunzi

Hotuba ya Mama Samia hata akisema Bungeni ataongeza mishahara bado hilo ongezeko litakatwa riba ya asilimia 15% ya Bodi a ya mikopo

Kijana aliyeanza kazi na mshahara wa TZS 1,600,000 Graduate anakatwa karibu TZS 240,000 ya Bodi ya mikopo, Hapo bado kodi ya Paye, Bado NSSF. Hata ukimuongeza huyu kijana mshahara mpaka TZS 1,800,000 mambo ni yale yale tu

Tuwaunge mkono vijana wetu kupaza sauti wanaumia sana na riba ya asilimia 15%

Serikali ijaribu kushusha riba hii

Tamko lolote la Kuongeza mishahara kwa watumishi wa uma halitakuwa na maana kama bado deni la Bodi ya mikopo litabaki asilimia 15%
Hakika huu ni unyonyaji mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom