choga mkuu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2016
- 283
- 110
Bodi ya mikopo vyuon imekua ikichelewefa fedha za kujikimu kwa wanafunzi kwa sababu zisizo na tija . Aidha mpaka muda huu vyuo vingi vinategemea kuanza mtihani Wa kufunga UE lakin bodi haijatoa fedha za field hata form za kusain wanafunzi za bodi hazijatolewa mpaka muda huu. Hali hii imekuwa ikipelekea wanafunzi wengi kujiingiza kwenye vitendo vilivyo kinyume na maadili ya jamii ya Tanzania. Hata hivyo bodi imekuwa haitoi taarifa kwa muda ili kuwafanya wanafunzi kukaa wakijua fedha hizo zitachelewa kutoka . Naitaka serikali ambayo imejipambanua kuwa inajali maslahi ya wanafunzi iingilie kati ili wanafunzi wapate fedha za field mapema