Bodi ya mikopo na makato ya asilimia nane (8) ya mshahara

AmaniGK

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
1,150
369
Hapo Novemba mwaka jana Higher Education Students Loans Board Act ilirekebishwa katika Section 20 na ikawa inasomeka hivi "Deduct 8% of the basic salary for employee who is a loan beneficiary and remit the same to the Board in the manner as the Board shall describe".

Natumaini marekebisho haya yalifanywa huku wawakilishi wetu bungeni wakiiona na kuiunga mkono. Mabadiliko haya ambayo yamechukua nafasi ya yale ya mwanzoni ambako wakopaji walitakiwa kurudisha deni lao kwa kipindi cha miaka kumi, yameongeza kiwango cha ukusanyaji kwa hali ya juu.

Kwa maoni yangu: Makato haya ni makubwa ikizingatiwa viwango vya mshahara ambavyo wafanyakazi wanavyo, Pia tukizingatia karibia asilimia 30 ya mshahara huo huo yanapelekwa kwenye kodi, Asilimia 10 kuchangia kwenye mifuko ya jamii. Kwa maana hii sasa kwa wale waliokopa karibu asilimia 50 ya mapato yao ya mwezi yanaangukia kwenye makato haya ya lazima.

Nadhani ipo haja ya hili kupigiwa tena kelele kama lile la Fao la kujitoa linavyopigiwa kelele.Makusanyo haya japo yatarudisha madeni kwa uharaka, lakini hayakuangalia kipato cha mfanyakazi wa kawaida.Kuna haja ya lazima kabisa kwa hili kupitiwa tena kwa undani zaidi.
 
huu ni unyanyasaji wa wananchi wa kipato cha chini, yaani umetoka chuo bado hujajijenga unakatwa kiwango hicho? bora ingekuwa 5%!!!
 
nina uchungu sana kwa jinsi mshahara wangu inavyokatwa tena kwa amount kubwa zaid ya laki moja hapo bado natakiwa nijenge maisha yangu,hopeless country never seen
 
Mi ndo nimeishiwa pozi kabisa. Sikumaliza hata mwaka nikaanza kukatwa. Mshahara hata haujarekebishwa lkn wameshaanza kukata. Chakushangaza nimemaliza mwaka jana tu wakati kuna wengine toka miaka ya tisini bado hajaanza.
 
Aiseee baba yangu mi namaliza mwakani ila hawatanikata ata cent 5 maana nitajiajiri mwanyewe sito taka kuajiriwa,,,hii nchi yetu sote sio wale wao si tubaki
 
Back
Top Bottom