Bodi Ya Mikopo Kwa Wanafunzi Ivunjwe

maggid

Verified Member
Dec 3, 2006
1,084
1,500

Na Maggid Mjengwa,

TUMESOMA , kuwa wanafunzi wapatao elfu 14,000 wenye sifa za kujiunga na masomo ya elimu ya juu wamekosa sifa za kupata mikopo kutoka bodi hiyo.
Hii ni taarifa ya kusikitisha na inaonyesha kuwa wakati umefika kwa Bodi ya Mikopo kuvunjwa na badala yake wanafunzi wenye sifa za kujiunga na masomo ya elimu ya juu wasaidiwe kupata mikopo kutoka kwenye mamlaka itakayotoa mikopo hiyo . Na katika hilo, Serikali iwe mdhamini mkuu wa chombo kitakachoundwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi na kuifuatilia kwenye malipo.

Ikumbukwe, katika hotuba yake ya kukizindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma Novemba 25, 2010, Rais Jakaya Kikwete aliahidi mambo makubwa mawili kama ifuatavyo, nanukuu:

Moja: “Kuhusu mikopo ya elimu ya juu napenda kuwahakikishia wazazi na wanafunzi kuwa tutaendelea kuongeza fedha katika mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike. Tumefanya hivyo katika miaka mitano iliyopita na tutafanya hivyo siku za usoni. Serikali iliongeza fedha za mikopo kutoka shilingi bilioni 56.1 mwaka 2005/06 hadi kuwa shilingi 237 bilioni mwaka 2010/11 na wanafunzi waliopatiwa mikopo hiyo wameongezeka kutoka 16,345 hadi 69,921. Haya ni mafanikio makubwa na naahidi kuwa tutafanya vizuri zaidi ili tuwafikie wanafunzi wengi zaidi.

Pili: Pia tutautazama upya mfumo mzima wa utoaji wa mikopo ikiwepo na utendaji kazi wa Bodi ya Mikopo kwa nia ya kuuboresha na kuleta ufanisi zaidi. Mawazo ya wadau wakiwemo wamiliki wa vyuo, wahadhiri na wanafunzi, yatasaidia sana”.

Na katika kutekeleza ahadi hiyo ya Pili, Rais Kikwete aliteua Tume ya wataalam 11 kufanya mapitio ya mfumo na uendeshaji wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini kwa lengo la kuimarisha utoaji wa mikopo hiyo. Tume ilitakiwa kufanyakazi kwa siku 60, kuanzia tarehe 14 Februari 2011 na kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi tarehe 15 Aprili 2011.

Mpaka kufikia sasa, ripoti husika juu ya kupata namna bora ya kutoa mikopo haijawekwa hadharani. Na tunakumbuka, kuwa Rais aliomba pia mawazo ya wadau. Kuna tuliotoa mawazo yetu. Na hapa tunayaweka tena wazi ili wahusika wayasome na kuona kama kuna ya kuyafanyia kazi.
Nilipata kuandika, kuwa suala la wanafunzi wa vyuo vikuu kugoma sasa limekuwa ni la kila mara. Kwa sasa migomo vyuo vikuu si habari mpya bali ni suala la lini utakuja mgomo mwingine baada ya mmoja kuhahirishwa au kuzimwa, kwa nguvu za dola. Ndio, kwa jinsi tunavyoenenda, hakuna dalili za migomo kumalizika bali ni kuzimwa na kuanza tena.

Suluhisho la muda mrefu linawezekana, kinachotakikana ni dhamira halisi ya kisiasa. Kwamba tuangalie upya utaratibu wa kulipia gharama za masomo kwa Vyuo Vikuu ili watoto wa Makabwela waweze kupata fursa ya kusoma. Tukubali kuwa hakuna tena kinachoitwa kuchangia elimu ya vyuo vikuu. Wakati umebadilika, gharama za kumwudumia mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni kubwa mno. Mzigo huo hawezi kuachiwa mzazi, hauwezi kuachiwa Serikali pekee. Ni mzigo wa mwanafunzi mwenyewe, lakini asaidiwe kuubeba kwa kukopeshwa fedha za kugharamia elimu yake.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni mtu mzima, anapaswa kuwajibika kulipa deni la elimu itayomsaidia maishani mwake. Kinachotakiwa ni kufanya mawili yafuatayo;
Mosi, Serikali iandae utaratibu utakaoiwezesha kukopa fedha ili kulipia tuition ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu. Tuition hapa ina maana gharama ambazo chuo husika kinahitaji kulipwa ili kiweze kutoa mafunzo stahili kwa mwanafunzi. Kwa mantiki hii, mwanafunzi hatalizimika kulipia gharama hizi isipokuwa zitalipwa na Serikali kutokana na mapato yatokanayo na kodi.

Pili, Serikali ivunje Bodi ya Mikopo na badala yake iunde chombo cha kukopesha wanafunzi ili wagharamie mahitaji yao ya msingi ya kila mwezi wa masomo ikiwamo malazi,chakula, usafiri na vitabu. Kiitengwe kiwango maalumu ambacho itakubalika kuwa kinamtosha mwanafunzi kulipia gharama hizo. Mwanafunzi aliyepata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu atakuwa na hiyari ya kuingia mkataba wa kukopeshwa kila mwezi na chombo hicho au la, kwa maana ya kuamua kujilipia kwa msaada wa wazazi au ndugu na jamaa zake.

Mwanafunzi atakuwa anaomba fedha za kila muhula wa masomo na kuzipata kwa kila mwezi kupitia akaunti yake. Na ili afuzu kupata mkopo huo kwa muhula unaofuatia,mwanafunzi huyo atahitajika kuonyesha ripoti ya kiakedemia itakayothibitishwa kuwa amefaulu kwa kiwango kitakachokubaliwa kwa masomo ya muhula uliopita ili aweze kuendelea kukopesheka.

Mwanafunzi huyo atalazimika kuanza kulipa deni lake mara tu akipata ajira baada ya kumaliza masomo yake. Deni hilo litalipwa kwa kukatwa katika kila mshahara wa mwezi. Chombo hicho cha kuwakopesha wanafunzi kitatunza kumbukumbu za mwanafunzi na kitakuwa kikifanya kazi kwa mujibu wa sheria na kupewa uwezo wa kuwafuatilia wadaiwa wake na hata kuwafungulia mashtaka kama watashindwa kutimiza masharti ya mikopo hiyo.

Tukichukua muda wetu kuifanyia kazi kwa kina hoja yangu hii, basi, naamini inaweza kuwa muharobaini wa kuondokana na kinachoitwa migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu. Hii ni kwa sababu, kuna nchi tayari zenye mfumo kama huu na ambazo msamiati wa mwanafunzi kugoma haupo tena kwenye jamii zao.

Ni utaratibu utakaowapunguzia wazazi kero na hata chuki kwa Serikali yao kwa kuwabebesha mzigo wa kusomesha hata vijana wa vyuo vikuu ambao kimsingi ni watu wazima. Na hapa ndipo mchango wa Wabunge wetu unahitajika katika kuzifanyia kazi hoja za wananchi zenye kulenga kuwasaidia watoto wa Makabwela, wanyonge wa nchi hii.
Watanzania hatupendi kuonyeshwa picha za kwenye runinga na magazetini jinsi wanafunzi wetu wakilazimishwa kufunga virago kurudi makwao. Huko nyuma kuna tuliowaona wakirudishwa kwa kuwa hawakuwa na sifa za kupata
mikopo. Kwamba hawakufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza kama ni wavulana, na daraja la kwanza au la pili kama ni wasichana. Hakika ilitushangaza wengi wetu, kuwa vijana wetu wale waliondolewa vyuoni kwa mujibu wa sheria iliyounda Bodi ya Mikopo ingawa waliofungishwa virago walistahili kubaki chuoni na kupata mikopo ya Bodi.

Na hapa ndipo tunapoona umuhimu wa kuwa na utaratibu mpya,maana huu wa sasa hautufai ikiwamo uwepo wa Bodi ya Mikopo. Kwa niaba yetu wananchi, Waheshimiwa wabunge wetu wahoji; Je ni kwanini baadhi ya wanafunzi wenye sifa za kujiunga na masomo ya Elimu ya Juu wananyimwa nafasi hizo na kupangiwa madaraja ya kufaulu ili wapate udhamini wa serikali? Je, hatuoni kuwa jambo hili linaimarisha matabaka katika jamii na kwamba litazidi kuongeza pengo kati ya masikini na tajiri?

Iweje leo, miaka 50 baada ya uhuru wetu, kijana wa Kitanzania mwenye sifa ya kusoma elimu ya juu asipate nafasi hiyo kwa vile tu amefaulu kwa daraja la pili na amechagua kusomea Biashara, Uchumi, Utawala, Michezo na masomo mengine yasiyo ya sayansi au fani ya ualimu? Matabaka haya ni ya nini? Kila eneo la mafunzo katika Chuo Kikuu lina umuhimu wake kitaifa na kimataifa na ndio maana ya kufundishwa Chuo Kikuu.

Ndio,mfumo tulionao sasa una kasoro. Bila kuufanyia marekebisho,migomo Vyuo Vikuu itakuwa ni jambo la lini unakuja mwingine. Hali hii ikiendelea ina athari kubwa ya kiuchumi na kijamii kwa taifa letu. Tusiache iwe hivyo. Nahitimisha.

0712 95 61 31 / 0788 111 765/ 0754 678 252 http://mjengwa.blogspot.commjengwamaggid@gmail.com
 
Nov 27, 2010
68
95
ndugu yangu tanzania imekuwa nchi ya kuongozwa na tume na si sheria husika maana hata mimi nimekosa mkopo na cjui kama ntaenda chuo maana sina uewezo wa kujilipia mwenyewe rais wetu ni mwongo namba moja anadiriki kudanganya watanzania na kama kawaida yet upole ndiyo ujinga wetu wakati umefika sasa watu tuamke na tukumbuke yaliyotokea vita kuu ya kwanza ya dunia baada mwanafunzi wa chuo kumuua rais wake.
 
MAKAKI

Senior Member
Sep 2, 2011
166
0
kama nikipigwa ban basi! PUMBAVU ZAO BODI YA MIKOPO, WAJINGA SANA NA MASABURI YAO YAKUSHOTO! WAMNYIMA JAMAA YANGU MTOTO WA MASIKIN AF HANA BABA. harafu yana sema eti yako kuwasaidia watoto wote wa masikin MM nahasira sana na haya majitu, YAMENENEPEANA KWELI MPAKA YANASHINDWA KUHEMA!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,208
2,000
Walioichagua CCM na serikali yake wawe tayari kuishi na matokeo ya uchaguzi huo. Hao vijana na wazazi walipewa nafasi ya kubadilisha serikali mwaka jana wakavaa magwanda ya kijani na njano na vibendera juu.. CCM nambari wanii wakaaimba.. sasa wanaona matokeo wanashangaa? Kwani CCM iliwaambia itabadilisha bodi ya mikopo au mfumo wake?
 
NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
326
225
Na Maggid Mjengwa, TUMESOMA , kuwa wanafunzi wapatao elfu 14,000 wenye sifa za kujiunga na masomo ya elimu ya juu wamekosa sifa za kupata mikopo kutoka bodi hiyo. Hii ni taarifa ya kusikitisha na inaonyesha kuwa wakati umefika kwa Bodi ya Mikopo kuvunjwa na badala yake wanafunzi wenye sifa za kujiunga na masomo ya elimu ya juu wasaidiwe kupata mikopo kutoka kwenye mamlaka itakayotoa mikopo hiyo . Na katika hilo, Serikali iwe mdhamini mkuu wa chombo kitakachoundwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi na kuifuatilia kwenye malipo. Ikumbukwe, katika hotuba yake ya kukizindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma Novemba 25, 2010, Rais Jakaya Kikwete aliahidi mambo makubwa mawili kama ifuatavyo, nanukuu:Moja: “Kuhusu mikopo ya elimu ya juu napenda kuwahakikishia wazazi na wanafunzi kuwa tutaendelea kuongeza fedha katika mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike. Tumefanya hivyo katika miaka mitano iliyopita na tutafanya hivyo siku za usoni. Serikali iliongeza fedha za mikopo kutoka shilingi bilioni 56.1 mwaka 2005/06 hadi kuwa shilingi 237 bilioni mwaka 2010/11 na wanafunzi waliopatiwa mikopo hiyo wameongezeka kutoka 16,345 hadi 69,921. Haya ni mafanikio makubwa na naahidi kuwa tutafanya vizuri zaidi ili tuwafikie wanafunzi wengi zaidi.Pili: Pia tutautazama upya mfumo mzima wa utoaji wa mikopo ikiwepo na utendaji kazi wa Bodi ya Mikopo kwa nia ya kuuboresha na kuleta ufanisi zaidi. Mawazo ya wadau wakiwemo wamiliki wa vyuo, wahadhiri na wanafunzi, yatasaidia sana”.Na katika kutekeleza ahadi hiyo ya Pili, Rais Kikwete aliteua Tume ya wataalam 11 kufanya mapitio ya mfumo na uendeshaji wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini kwa lengo la kuimarisha utoaji wa mikopo hiyo. Tume ilitakiwa kufanyakazi kwa siku 60, kuanzia tarehe 14 Februari 2011 na kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi tarehe 15 Aprili 2011. Mpaka kufikia sasa, ripoti husika juu ya kupata namna bora ya kutoa mikopo haijawekwa hadharani. Na tunakumbuka, kuwa Rais aliomba pia mawazo ya wadau. Kuna tuliotoa mawazo yetu. Na hapa tunayaweka tena wazi ili wahusika wayasome na kuona kama kuna ya kuyafanyia kazi. Nilipata kuandika, kuwa suala la wanafunzi wa vyuo vikuu kugoma sasa limekuwa ni la kila mara. Kwa sasa migomo vyuo vikuu si habari mpya bali ni suala la lini utakuja mgomo mwingine baada ya mmoja kuhahirishwa au kuzimwa, kwa nguvu za dola. Ndio, kwa jinsi tunavyoenenda, hakuna dalili za migomo kumalizika bali ni kuzimwa na kuanza tena. Suluhisho la muda mrefu linawezekana, kinachotakikana ni dhamira halisi ya kisiasa. Kwamba tuangalie upya utaratibu wa kulipia gharama za masomo kwa Vyuo Vikuu ili watoto wa Makabwela waweze kupata fursa ya kusoma. Tukubali kuwa hakuna tena kinachoitwa kuchangia elimu ya vyuo vikuu. Wakati umebadilika, gharama za kumwudumia mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni kubwa mno. Mzigo huo hawezi kuachiwa mzazi, hauwezi kuachiwa Serikali pekee. Ni mzigo wa mwanafunzi mwenyewe, lakini asaidiwe kuubeba kwa kukopeshwa fedha za kugharamia elimu yake. Mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni mtu mzima, anapaswa kuwajibika kulipa deni la elimu itayomsaidia maishani mwake. Kinachotakiwa ni kufanya mawili yafuatayo; Mosi, Serikali iandae utaratibu utakaoiwezesha kukopa fedha ili kulipia tuition ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu. Tuition hapa ina maana gharama ambazo chuo husika kinahitaji kulipwa ili kiweze kutoa mafunzo stahili kwa mwanafunzi. Kwa mantiki hii, mwanafunzi hatalizimika kulipia gharama hizi isipokuwa zitalipwa na Serikali kutokana na mapato yatokanayo na kodi. Pili, Serikali ivunje Bodi ya Mikopo na badala yake iunde chombo cha kukopesha wanafunzi ili wagharamie mahitaji yao ya msingi ya kila mwezi wa masomo ikiwamo malazi,chakula, usafiri na vitabu. Kiitengwe kiwango maalumu ambacho itakubalika kuwa kinamtosha mwanafunzi kulipia gharama hizo. Mwanafunzi aliyepata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu atakuwa na hiyari ya kuingia mkataba wa kukopeshwa kila mwezi na chombo hicho au la, kwa maana ya kuamua kujilipia kwa msaada wa wazazi au ndugu na jamaa zake. Mwanafunzi atakuwa anaomba fedha za kila muhula wa masomo na kuzipata kwa kila mwezi kupitia akaunti yake. Na ili afuzu kupata mkopo huo kwa muhula unaofuatia,mwanafunzi huyo atahitajika kuonyesha ripoti ya kiakedemia itakayothibitishwa kuwa amefaulu kwa kiwango kitakachokubaliwa kwa masomo ya muhula uliopita ili aweze kuendelea kukopesheka. Mwanafunzi huyo atalazimika kuanza kulipa deni lake mara tu akipata ajira baada ya kumaliza masomo yake. Deni hilo litalipwa kwa kukatwa katika kila mshahara wa mwezi. Chombo hicho cha kuwakopesha wanafunzi kitatunza kumbukumbu za mwanafunzi na kitakuwa kikifanya kazi kwa mujibu wa sheria na kupewa uwezo wa kuwafuatilia wadaiwa wake na hata kuwafungulia mashtaka kama watashindwa kutimiza masharti ya mikopo hiyo. Tukichukua muda wetu kuifanyia kazi kwa kina hoja yangu hii, basi, naamini inaweza kuwa muharobaini wa kuondokana na kinachoitwa migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu. Hii ni kwa sababu, kuna nchi tayari zenye mfumo kama huu na ambazo msamiati wa mwanafunzi kugoma haupo tena kwenye jamii zao. Ni utaratibu utakaowapunguzia wazazi kero na hata chuki kwa Serikali yao kwa kuwabebesha mzigo wa kusomesha hata vijana wa vyuo vikuu ambao kimsingi ni watu wazima. Na hapa ndipo mchango wa Wabunge wetu unahitajika katika kuzifanyia kazi hoja za wananchi zenye kulenga kuwasaidia watoto wa Makabwela, wanyonge wa nchi hii. Watanzania hatupendi kuonyeshwa picha za kwenye runinga na magazetini jinsi wanafunzi wetu wakilazimishwa kufunga virago kurudi makwao. Huko nyuma kuna tuliowaona wakirudishwa kwa kuwa hawakuwa na sifa za kupata mikopo. Kwamba hawakufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza kama ni wavulana, na daraja la kwanza au la pili kama ni wasichana. Hakika ilitushangaza wengi wetu, kuwa vijana wetu wale waliondolewa vyuoni kwa mujibu wa sheria iliyounda Bodi ya Mikopo ingawa waliofungishwa virago walistahili kubaki chuoni na kupata mikopo ya Bodi. Na hapa ndipo tunapoona umuhimu wa kuwa na utaratibu mpya,maana huu wa sasa hautufai ikiwamo uwepo wa Bodi ya Mikopo. Kwa niaba yetu wananchi, Waheshimiwa wabunge wetu wahoji; Je ni kwanini baadhi ya wanafunzi wenye sifa za kujiunga na masomo ya Elimu ya Juu wananyimwa nafasi hizo na kupangiwa madaraja ya kufaulu ili wapate udhamini wa serikali? Je, hatuoni kuwa jambo hili linaimarisha matabaka katika jamii na kwamba litazidi kuongeza pengo kati ya masikini na tajiri? Iweje leo, miaka 50 baada ya uhuru wetu, kijana wa Kitanzania mwenye sifa ya kusoma elimu ya juu asipate nafasi hiyo kwa vile tu amefaulu kwa daraja la pili na amechagua kusomea Biashara, Uchumi, Utawala, Michezo na masomo mengine yasiyo ya sayansi au fani ya ualimu? Matabaka haya ni ya nini? Kila eneo la mafunzo katika Chuo Kikuu lina umuhimu wake kitaifa na kimataifa na ndio maana ya kufundishwa Chuo Kikuu. Ndio,mfumo tulionao sasa una kasoro. Bila kuufanyia marekebisho,migomo Vyuo Vikuu itakuwa ni jambo la lini unakuja mwingine. Hali hii ikiendelea ina athari kubwa ya kiuchumi na kijamii kwa taifa letu. Tusiache iwe hivyo. Nahitimisha.0712 95 61 31 / 0788 111 765/ 0754 678 252 http://mjengwa.blogspot.commjengwamaggid@gmail.com [/QKAKA UMENENA VEMA MAANA UTARATIBU HUU UNAOTUMIWA BADO HAUJAWA NA NAMNA YA KUWEZA KUWATAMBUA WANAO STAHILI MKOPO KTK KIPENGELE CHA UCHUMI UJNAKUTA MTU AMBAE WAZEE MAMBO SAFI ANA LIJIMKOPO LIKUBWA TENA WENGINE WATOTO WA VIONGOZI AMBAO MAJINA YA BABA ZAO YAPO KWENYE HIYO MIFOMU LAKINI MAKABWELA KABISA HAWANA!NINAYO MIFANO DHAHIRI WAKUU!NIKIANZA NA MTOTO AMBAE BABA YAKE HUJIITA MTOTO WA MKULIMA ANASOMO CHUO KIMOJAWAPO HAPA NCHINI ANALIJIMKOPO HILOOOO
 
2simamesote

Senior Member
Jun 27, 2011
109
0
hivi majjid ikiwa kila kitu kitavunjwa. nchi itaelekea wapi? mimi wakati nasoma. bodi ya mkopo ilikuwa hakuna. matatizo mengi sana yalikuwepo kuliko hata haya yaliopo sasa.
<br />
<br />
ucfananishe enzi zenu na sasa,kama ndo hivyo na mishahara ibaki kama wakati wa mwl maana pia tabu zilikua nyingi kuliko sasa,nenda kwenye kale ka forum kako ukaandike hiki si hapa jf
 
Eshacky

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
962
225
Walioichagua CCM na serikali yake wawe tayari kuishi na matokeo ya uchaguzi huo. Hao vijana na wazazi walipewa nafasi ya kubadilisha serikali mwaka jana wakavaa magwanda ya kijani na njano na vibendera juu.. CCM nambari wanii wakaaimba.. sasa wanaona matokeo wanashangaa? Kwani CCM iliwaambia itabadilisha bodi ya mikopo au mfumo wake?
<br />
<br />
Uchaguz umeshapita, acha kulalama, toa mapendekezo yenye tija kwa taifa yaweze kubadili mfumo mzima wa utoaji wa mipoko, hata usemeje hii ndo serikal iliyopo madarakan huna budi kuikubali. Nyie mna influence kubwa kwa jamii toeni makala kama hizi zitazosaidia jamii kujua kasoro zilizopo juu ya bodi hii ili wakisikia vijana wamegoma machuoni wajue vijana wao wanatetea haki zao za msingi, na wawasupport kwa maana umma una nguvu na ndio walioweka viongoz wa serikal pale walipo kupitia sanduku la kura.
 
NIMIMI

Senior Member
Apr 2, 2011
170
170
NIMESIKITIKA SANA, Maana hata wazazi wangu nilipohitimu kidato cha IV walinihoji mwanetu pamoja na shida zote zile lakini na hatimaye kujiunga kidato cha tano, niliwajibu Mungu ndie aliyeniwezesha. Wakaniombea nikaendelea nikaendelea na masomo kuhitimu kidato cha 6, baba akaniambia mwanangu hatimaye Mungu amekuwezesha kupata daraja la kwanza tena? Nikamjibu Mungu mkubwa, mwanangu unajiunga na elimu ya juu i.e Chuo kikuu ila sina pesa mwanangu za kukusomesha,nikamjibu kuna mikopo, cha kushangaza mwaka wa kwanza nikaomba chuo nikapata nikakosa mkopo nikakaa nyumbani, mwaka uliofuata jambo lilelile nikavumilia, mwaka huu ikiwa ni mara yangu ya tatu kunyimwa mkopo najibiwa 'BUDGET EXHAUSTED' ndoto za kwenda chuo zilififia na sasa zinaelekea ukingoni kwa7bu ya kukosa mkopo. Mungu ninusuru na kiama maana nazeeka sasa!
 
kipindupindu

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
1,056
1,250
Na Maggid Mjengwa,

TUMESOMA , kuwa wanafunzi wapatao elfu 14,000 wenye sifa za kujiunga na masomo ya elimu ya juu wamekosa sifa za kupata mikopo kutoka bodi hiyo.
Hii ni taarifa ya kusikitisha na inaonyesha kuwa wakati umefika kwa Bodi ya Mikopo kuvunjwa na badala yake wanafunzi wenye sifa za kujiunga na masomo ya elimu ya juu wasaidiwe kupata mikopo kutoka kwenye mamlaka itakayotoa mikopo hiyo . Na katika hilo, Serikali iwe mdhamini mkuu wa chombo kitakachoundwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi na kuifuatilia kwenye malipo.

Ikumbukwe, katika hotuba yake ya kukizindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma Novemba 25, 2010, Rais Jakaya Kikwete aliahidi mambo makubwa mawili kama ifuatavyo, nanukuu:

Moja: "Kuhusu mikopo ya elimu ya juu napenda kuwahakikishia wazazi na wanafunzi kuwa tutaendelea kuongeza fedha katika mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike. Tumefanya hivyo katika miaka mitano iliyopita na tutafanya hivyo siku za usoni. Serikali iliongeza fedha za mikopo kutoka shilingi bilioni 56.1 mwaka 2005/06 hadi kuwa shilingi 237 bilioni mwaka 2010/11 na wanafunzi waliopatiwa mikopo hiyo wameongezeka kutoka 16,345 hadi 69,921. Haya ni mafanikio makubwa na naahidi kuwa tutafanya vizuri zaidi ili tuwafikie wanafunzi wengi zaidi.

Pili: Pia tutautazama upya mfumo mzima wa utoaji wa mikopo ikiwepo na utendaji kazi wa Bodi ya Mikopo kwa nia ya kuuboresha na kuleta ufanisi zaidi. Mawazo ya wadau wakiwemo wamiliki wa vyuo, wahadhiri na wanafunzi, yatasaidia sana".

Na katika kutekeleza ahadi hiyo ya Pili, Rais Kikwete aliteua Tume ya wataalam 11 kufanya mapitio ya mfumo na uendeshaji wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini kwa lengo la kuimarisha utoaji wa mikopo hiyo. Tume ilitakiwa kufanyakazi kwa siku 60, kuanzia tarehe 14 Februari 2011 na kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi tarehe 15 Aprili 2011.

Mpaka kufikia sasa, ripoti husika juu ya kupata namna bora ya kutoa mikopo haijawekwa hadharani. Na tunakumbuka, kuwa Rais aliomba pia mawazo ya wadau. Kuna tuliotoa mawazo yetu. Na hapa tunayaweka tena wazi ili wahusika wayasome na kuona kama kuna ya kuyafanyia kazi.
Nilipata kuandika, kuwa suala la wanafunzi wa vyuo vikuu kugoma sasa limekuwa ni la kila mara. Kwa sasa migomo vyuo vikuu si habari mpya bali ni suala la lini utakuja mgomo mwingine baada ya mmoja kuhahirishwa au kuzimwa, kwa nguvu za dola. Ndio, kwa jinsi tunavyoenenda, hakuna dalili za migomo kumalizika bali ni kuzimwa na kuanza tena.

Suluhisho la muda mrefu linawezekana, kinachotakikana ni dhamira halisi ya kisiasa. Kwamba tuangalie upya utaratibu wa kulipia gharama za masomo kwa Vyuo Vikuu ili watoto wa Makabwela waweze kupata fursa ya kusoma. Tukubali kuwa hakuna tena kinachoitwa kuchangia elimu ya vyuo vikuu. Wakati umebadilika, gharama za kumwudumia mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni kubwa mno. Mzigo huo hawezi kuachiwa mzazi, hauwezi kuachiwa Serikali pekee. Ni mzigo wa mwanafunzi mwenyewe, lakini asaidiwe kuubeba kwa kukopeshwa fedha za kugharamia elimu yake.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni mtu mzima, anapaswa kuwajibika kulipa deni la elimu itayomsaidia maishani mwake. Kinachotakiwa ni kufanya mawili yafuatayo;
Mosi, Serikali iandae utaratibu utakaoiwezesha kukopa fedha ili kulipia tuition ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu. Tuition hapa ina maana gharama ambazo chuo husika kinahitaji kulipwa ili kiweze kutoa mafunzo stahili kwa mwanafunzi. Kwa mantiki hii, mwanafunzi hatalizimika kulipia gharama hizi isipokuwa zitalipwa na Serikali kutokana na mapato yatokanayo na kodi.

Pili, Serikali ivunje BodiyaMikopo na badala yake iunde chombo cha kukopesha wanafunzi ili wagharamie mahitaji yao ya msingi ya kila mwezi wa masomo ikiwamo malazi,chakula, usafiri na vitabu. Kiitengwe kiwango maalumu ambacho itakubalika kuwa kinamtosha mwanafunzi kulipia gharama hizo. Mwanafunzi aliyepata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu atakuwa na hiyari ya kuingia mkataba wa kukopeshwa kila mwezi na chombo hicho au la, kwa maana ya kuamua kujilipia kwa msaada wa wazazi au ndugu na jamaa zake.

Mwanafunzi atakuwa anaomba fedha za kila muhula wa masomo na kuzipata kwa kila mwezi kupitia akaunti yake. Na ili afuzu kupata mkopo huo kwa muhula unaofuatia,mwanafunzi huyo atahitajika kuonyesha ripoti ya kiakedemia itakayothibitishwa kuwa amefaulu kwa kiwango kitakachokubaliwa kwa masomo ya muhula uliopita ili aweze kuendelea kukopesheka.

Mwanafunzi huyo atalazimika kuanza kulipa deni lake mara tu akipata ajira baada ya kumaliza masomo yake. Deni hilo litalipwa kwa kukatwa katika kila mshahara wa mwezi. Chombo hicho cha kuwakopesha wanafunzi kitatunza kumbukumbu za mwanafunzi na kitakuwa kikifanya kazi kwa mujibu wa sheria na kupewa uwezo wa kuwafuatilia wadaiwa wake na hata kuwafungulia mashtaka kama watashindwa kutimiza masharti yamikopo hiyo.

Tukichukua muda wetu kuifanyia kazi kwa kina hoja yangu hii, basi, naamini inaweza kuwa muharobaini wa kuondokana na kinachoitwa migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu. Hii ni kwa sababu, kuna nchi tayari zenye mfumo kama huu na ambazo msamiati wa mwanafunzi kugoma haupo tena kwenye jamii zao.

Ni utaratibu utakaowapunguzia wazazi kero na hata chuki kwa Serikali yao kwa kuwabebesha mzigo wa kusomesha hata vijana wa vyuo vikuu ambao kimsingi ni watu wazima. Na hapa ndipo mchango wa Wabunge wetu unahitajika katika kuzifanyia kazi hoja za wananchi zenye kulenga kuwasaidia watoto wa Makabwela, wanyonge wa nchi hii.
Watanzania hatupendi kuonyeshwa picha za kwenye runinga na magazetini jinsi wanafunzi wetu wakilazimishwa kufunga virago kurudi makwao. Huko nyuma kuna tuliowaona wakirudishwa kwa kuwa hawakuwa na sifa za kupata
mikopo. Kwamba hawakufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza kama ni wavulana, na daraja la kwanza au la pili kama ni wasichana. Hakika ilitushangaza wengi wetu, kuwa vijana wetu wale waliondolewa vyuoni kwa mujibu wa sheria iliyounda BodiyaMikopo ingawa waliofungishwa virago walistahili kubaki chuoni na kupata mikopoyaBodi.

Na hapa ndipo tunapoona umuhimu wa kuwa na utaratibu mpya,maana huu wa sasa hautufai ikiwamo uwepo wa BodiyaMikopo. Kwa niaba yetu wananchi, Waheshimiwa wabunge wetu wahoji; Je ni kwanini baadhi ya wanafunzi wenye sifa za kujiunga na masomo ya Elimu ya Juu wananyimwa nafasi hizo na kupangiwa madaraja ya kufaulu ili wapate udhamini wa serikali? Je, hatuoni kuwa jambo hili linaimarisha matabaka katika jamii na kwamba litazidi kuongeza pengo kati ya masikini na tajiri?

Iweje leo, miaka 50 baada ya uhuru wetu, kijana wa Kitanzania mwenye sifa ya kusoma elimu ya juu asipate nafasi hiyo kwa vile tu amefaulu kwa daraja la pili na amechagua kusomea Biashara, Uchumi, Utawala, Michezo na masomo mengine yasiyo ya sayansi au fani ya ualimu? Matabaka haya ni ya nini? Kila eneo la mafunzo katika Chuo Kikuu lina umuhimu wake kitaifa na kimataifa na ndio maana ya kufundishwa Chuo Kikuu.

Ndio,mfumo tulionao sasa una kasoro. Bila kuufanyia marekebisho,migomo Vyuo Vikuu itakuwa ni jambo la lini unakuja mwingine. Hali hii ikiendelea ina athari kubwa ya kiuchumi na kijamii kwa taifa letu. Tusiache iwe hivyo. Nahitimisha.

0712 95 61 31 / 0788 111 765/ 0754 678 252 http://mjengwa.blogspot.commjengwamaggid@gmail.com
bwana majid naona unataka kujipatia umaarufu usio na msingi.bodi ya mikopo iendelee kuwepo!hatuwezi kusomesha kila mtu hata wale wasio na uwezo unataka wasome?lazima tuwe na specialisation na priorities kutegemeana na mahitaji ya soko n.k.nashauri serikali ijitoe kabisa katika kusomesha vilaza kwasababu hawataweza kulisaidia taifa kusonga mbele badala yake isomeshe vipanga wenye akili na baadae iwawezeshe ili wawe chanzo cha ajira ya vilaza.hata marekani hawasomeshi vilaza kwakuwa hawana uwezo wa kiakili ambao utaleta tija katika taifa.ni heri kuwa na elites wachache waliosomeshwa na kuwekewa mazingira mazuri ya kazi ili wabebe jukumu la vilaza wengi.pia lazima tutilie maanani zile fani zenye tija kwa sasa au baadae mfano eneo la mikataba,madini umeme n.k na sio kosomesha wasusi,wanasarakasi,wacheza ngoma halafu utegemee kupata maendeleo.msimamo wangu ni bora kununua wataalamu kuliko kugharamia wataalamu ambao kutokana na mazingira wanakimbila nje ya nchi.
 
Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,531
2,000
Suluhisho pekee si kuvunjwa kwa board ya mikopo. Lazima wajitathmini waangalie matatizo yanatokea wapi. Ila tatizo kubwa ni ufinyu wa bajeti, hili ni swala la kuangaliwa. Naona wanafanya kazi vizuri, tatizo bajet haiendani na ukuaji wa wanafunzi wanaojiunga na Universities.
 
tata mvoni

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
534
195
Walioichagua CCM na serikali yake wawe tayari kuishi na matokeo ya uchaguzi huo. Hao vijana na wazazi walipewa nafasi ya kubadilisha serikali mwaka jana wakavaa magwanda ya kijani na njano na vibendera juu.. CCM nambari wanii wakaaimba.. sasa wanaona matokeo wanashangaa? Kwani CCM iliwaambia itabadilisha bodi ya mikopo au mfumo wake?
<br />
<br />
kaka naunga mkono hoja mwaka jana tulikuwa nao,2kawapa ulaji sasa tutulie tu! Na bado....hii ndo serikali ya magamba
 
JMC prod

Member
Aug 4, 2011
90
95
Hoja co badget. Ishu ni wapi tule na walofanikisha sisi tule nao watapata nini? Iyo ndo inayoleta matatizo lukuki, kila m2 heslb ana kula kulingana na cheo na mkuu wake alivyobakisha...
Hii hela sio kodi wala hela ya serekali ni ela ya mkopo toka benki kuu ya dunia kwa kusaidia elimu, kinachoitajika ni amount f stud an amount f cost on da specfc year.. Ni due to da statcs za ufauluji kwa mwaka husika.
Iweje bajeti iwe na kikomo ile nyingine huenda wapi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom