Bodi ya Mikopo kuwafikisha Mahakamani wadaiwa sugu 142,470 kama wakishindwa kulipa ndani ya siku 30

Jamani hebu tujadili polepole, wakati tunasaini zile fomu si tuliona kabisa kama ni mkopo na wala sio maada?
 
Huu ndio mwanzo wa kufungua macho watanzania, mwanzo tuliambiwa elimu tunayoipata ni kwa ajili ya watanzania wote (kuwahudumia) na fedha za mikopo ni kodi za wanatzania. Sasa kama hawa wawakilishi wa wananchi (serikali) inataka kuwapeleka mahakamani (kuwafunga) waliopata elimu kupitia hizi kodi ili wasaidie walipa kodi, je? ukweli huo unaingia akilini?, Au ndo kusema siku hizi elimu ni mali binafsi, mbona ujira hauendani na hiyo dhana?
Ni hatari kubinafsisha elimu, hasa kwa nchi maskini kama ya kwetu ambayo hata ajira ni shida.
Itambulike kuwa hawa waliopata mikopo wanalipa kodi, na hata wazazi wao wanalipa kodi kwanini wanawakopesha wenye fedha wakisingizia sheria! Kwani hizo fedha serikali inazitoa wapi kama siyo kodi za wananchi wenyewe, kama ni mkopo kutoka nje tuambiwe!
 
Back
Top Bottom