JOSEPHAT J BAZA
Member
- May 4, 2013
- 27
- 22
Hivi karibuni bodi ya mokopo ya elimu ya juu imepandisha makato kufikia 15% kuanzia mwezi huu wa Februari. Uamzi huu umetusikitisha sana sote tuliosoma kupitia bodi hii; licha ya ongezeko hilo kuwa nje na mkataba, bado bodi haikuzingatia kiwango cha mshahara anachoweka mkononi mfanyakazi baada ya makato kufanyika.
Kama mjuavyo hali ya kipato cha mwalimu, karibu 75% ya walimu wana mikopo ktk taasisi mbalimbali za fedha ukiondoa makato mengine kama CWT, INCOME TAX, NHIF, PENSHENI nk.
Hebu wadau tujiulize, baada ya makato hayo mwalimu huyo anabaki na nini? Mfano mimi kama mmoja wa wahanga ktk janga hili take home salary yangu ni 400000/=
Baada ya kutoa 15% nitabaki na sh. 325000/= Je, kwa pesa hiyo maisha haya yatakuwaje? hapa kweli kazi itafanyika darasani? Sisi sote ni watanzania na bodi ni ya watanzania ni vema makato haya yakabaki kama yalivyokuwa awali otherwise, tutakimbia vituo vya kazi kwa ajili ya ukata.