Bodi ya Mikopo (HESLB) kuvunjwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bodi ya Mikopo (HESLB) kuvunjwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Oct 24, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Imeandikwa tarehe 24 Oktoba 2012 na Gloria Tesha | HabariLeo

  SERIKALI imesema inatarajia kuunda upya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) ili ijiendeshe yenyewe na kupunguza utegemezi wa Serikali na kuwezesha kurejesha Sh trilioni 1.1 zilizokopwa na wanafunzi.

  Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, hivi sasa Bodi hiyo inapata asilimia 75.5 ya bajeti yote ya wizara hiyo huku asilimia 25.5 pekee ikibaki wizarani.

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Celestine Gesimba aliyasema hayo jana alipo kuwa akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotaka ufafanuzi kuhusu utegemezi wa Bodi hiyo kwa Serikali utakwisha lini.

  Hoja ya wajumbe wa kamati hiyo, iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Cheyo, Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP) ilitokana na utegemezi wa asilimia 75.5 kwa bajeti ya Serikali na namna ya kulipa madeni kwa wanafunzi waliokopa.

  Akifafanua kuhusu hoja hizo na kiasi cha deni lililopo mpaka sasa na kilicholipwa baada ya ripoti ya CAG kuonesha upungufu, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Onesmas Laizer alisema mpaka Juni Bodi imekopesha Sh trilioni 1.087.

  “Hata hivyo, Bodi ina miaka saba sasa tangu ianzishwe na kabla haijaanza bodi, serikali ilishakopesha wanafunzi Sh bilioni 51.1, jumla ni Sh trilioni 1.138 zilizokopwa.

  Mikopo iliyoiva tayari kurejeshwa ni Sh bilioni 160.7,” alieleza Laizer. Hata hivyo, alisema kati ya hizo Sh bilioni 160.7 ambazo marejesho hufanywa kwa awamu, fedha zilizopaswa kuwa zimerejeshwa ni Sh bilioni 39.54 lakini mpaka Juni wameshakusanya Sh bilioni 20.15 pekee huku Sh bilioni 19 zikiwa mikononi mwa wakopaji.

  Cheyo alihoji kwa nini Bodi iendelee kiutendaji wa namna hiyo na kueleza kuwa tatizo la wizara na Bodi ni mfumo wa kumbukumbu (Data Base) na upungufu wa vyanzo mbadala vya mapato, unaorudisha nyuma ubora wa elimu nchini.

  Akifafanua hilo, Kaimu Katibu Gesimba alikiri kuwepo kwa tatizo kubwa katika utegemezi wa Bodi na kueleza kamati kuwa tayari Waziri mwenye dhamana aliliona hilo na aliunda timu kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha vyanzo vya mapato vya Bodi.

  “Ni kweli tatizo lipo, asilimia 75.5 ya bajeti inakwenda Bodi lakini siku zinavyokwenda na mahitaji ya mikopo kwa wanafunzi yanaongezeka, ila tayari mapendekezo ya awali yanaonesha kuwa Bodi itaundwa upya ili kupata vyanzo vya mapato, utendaji na kuongeza ufanisi,” alisema Gesimba.

  Ingawa hakusema timu itafanya kazi lini, Gesimba aliwambia waandishi wa habari nje ya kikao kuwa, tayari mapendekezo ya awali ya timu yamemfikia Waziri na yanachambuliwa ili kufikisha serikalini, na Serikali ikibariki, maboresho yatafanyika.
   
 2. m

  mdunya JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  aisee!
   
 3. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Wizara ya Elimu inaongozwa na 'vihiyo' akina Mulugo itawezaje kubuni na kusimamia mipango endelevu kwa ajili ya kuboresha elimu nchini? Kama Mulugo hajui tofauti ya Zimbabwe na Zanzibar, atawezaje kufikiria mapendekezo bora ya vyanzo vya mapato ya Bodi? Wadaiwa hawana ajira ya kuaminika, watawezaje kurejesha pesa hizo? Cheyo na wenzake lukuki walisoma bure, huo ujasiri wa kushinikiza wadaiwa walipe madeni wanautoa wapi? Bodi ya mikopo ivunjwe, iundwe bodi ya uwezeshaji elimu ya juu itakayo ratibu upatikanaji wa fedha za wanafunzi SIYO MIKOPO.
   
 4. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa wa HESLB ni wapuuzi sana, watu wanalipa mikopo lakini ukienda kwa taarifa zao, unaonekana hujawahi kulipa hata senti moja, bora waivunje tu waweke watu wapya kabisa, na liwe na muundo mzuri, manaje waliopo ni wazudhi tu, wanajilipa maposho makubwa kuliko pesa inayolipwa kwa wanafunzi!
   
 5. piper

  piper JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Imeshindwa kazi toka mwanzoni, good riddance.
   
 6. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  I wish wangechoma na kumbukumbu zote.
   
 7. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii bodi ni janga la Taifa.Bora ivunjwe.
   
 8. k

  kamkoda JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 396
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hiki ni kielelezo kwamba bado tunaweza kusoma bure bila mkopo, wao kwa kuwa wanasamehewa mikopo flan flan na kwa kuwa nao pia wanasamehe kodi flan flan, ni busara wafute mikopo hii waanze upya, nakumbuka wengi wamekwishafariki wengine wapo nje ya nchi wengine wapo sekta binafsi, wengine wamejiajiri lazima kuwe na mpango unaoendana na wakati kukabiliana na jambo hili.

  Kodi kwa graduate wa miaka ya mwishoni mwa miaka ya tisini inakaribia ama ni zaidi ya 1m. nafikiri huu ni mchango mzuri kwa taifa na unawezesha wadogo zetu kusoma bure bila mikopo hili linawezekana tusidanganyane na kama sio fedha zimetoka wapi kusomesha taifa kwa zaidi ya miaka kumi?
   
 9. H

  Huburya Charles Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wafanyakazi wa bodi wenyewe wezi katika kugushi nyaraka tofauti.
   
 10. k

  kasahunga Senior Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hao ni wezi tu:majani7::majani7:
   
 11. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa jamaa wana mfumo duni usio kifani wa kutunza kumbukumbu. Nimeomba mkopo mwaka wangu wa kwanza nikapata. Mwaka uliofuata yaani mwaka jana tuliomba kwa mfumo mpya wa online na nikapata. Mwaka huu nimeomba tena kupitia online wanasema sikuomba now na hakuna namna ya kufanyika sasa nipate mkopo. Nimekata tamaa ya kumalizia mwaka huu masomo kwa kuwa siwezi kujilipia.
   
 12. a

  ablood8 Senior Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Hamnaga asilimia 75.5 na asilimia 25.5 kwa sababu hazikupi asilimia 100
   
 13. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nina zaidi ya miaka mitatu nalipia mkopo wangu lakini i can bet tukienda HESLB hawatakuwa na rekodi za malipo yangu. Hii bodi bogus sana.
   
 14. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ili usilipe lile boom lako?
   
 15. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa miaka kumi mfululizo bodi ya mikopo imeshindwa kabisa kutatua matatizo ya wanafunzi licha ya kupokea fedha NYINGI kwenye makusanyo ya madeni na pia toka serikali 75.5% ya bajeti yake.Bodi imekuwa mbovu sana licha ya kubenwa na serikali, Je serikali ikijitoa itakuwaje? mmi nadhani Tatizo kubwa la bodi ya mikopo ilianzishwa kisiasa zaidi.Hapakuwepo na tathmini ya kina juu MFUMO BORA wa Uendeshaji wake na uwajibikaji wa watumishi.Hata na vyanzo vyake vya mapato.Kila siku ni migogoro kati yao na wanafunzi Haiishi.Hakuna ufanisi wala tija yeyote kwenye bodi.Hivi karibuni pameripotiwa wizi mkubwa wa fedha kutoka kwa watumishi wake.Wafanyakazi wake wameendelea kujilipa mishahara mikobwa na posho zisizokuwa na kichwa wala miguu.To Hell HESLB..!!
   
 16. j

  juju man Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ajira hakuna...........ulipe deni.................kwa njia ipi.............:confused2:
   
 17. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  yeah! nani anapenda madeni, wakati nchi kama kichwa cha mwendawazimu?
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Tuombe majibu ya tume kama 3 zilizoundwa ili tuone kama kweli kuna issue kubwa namna hiyo au kuna tatizo wizara elimu na wizara ya fedha....maana tume zote zimetoa majumuisho kuwa wako sawa sawa na wanajitahidi sana..wenye data za ile tume ya Prof Maboko aweke hapa tujadili kwa kina!
   
 19. KATUMBACHAKO

  KATUMBACHAKO JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwa maelezo hayo HESLB haivunjwi bali,inawezekana: - Ikabinafsishwa kwa mtu binafsi ili aweze kukusanya madeni ya waliokopa au - Akatafutwa wakala kama MAJEMBE au YONO AUCTIONMhh . . tutakoma! Sijui kama watoto wetu sisi hohe hahe watasoma! Ishakuwa dili hiyo bodi
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ooh boy! miaka sita baada ya wengine kuwaaambia waivunje na bado wanafikiria kuivunja!
   
Loading...