Bodi ya mikopo acheni kutuibia walipaji waaminifu

Bodi ya mikopo acheni kutuibia walipaji waaminifu

yoga

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2013
Posts
2,004
Reaction score
10,399
Habari za hapa wana JF wapendwa, natumaini mposalama wa salmin !! Leo nataka ni wasemee hawa watu wa BODI YA MIKOPO TANZANIA!! Kwa kitendo chao cha wao kuto kuwa waaminifu dhidi yetu sisi tunaowalipa fedha zao kwa uaminifu na kwa wakati!!!

Kwanza niseme naishukuru bodi hii kwa kuniwezesha kupata kaelimu kangu kadogo ambako kamenisaidia kupata ajira inayonifanya kuweza kupata kipato ambacho kimeweza kunihudumia mimi mwenyewe na wanaonitegemea(familia)

Nilimaliza kaelimu kangu hako ka shahada ya kwanza mwaka 2011, na nilipata ajira mnamo mwaka 2012, toka nimepata ajira yangu mwaka huo mwezi wa tatu bodi imekuwa ikikata fedha zao mpaka leo hii!!

Kilicho nifanya kuwaita hawa watu ni wezi, ni kwamba deni linaloonekana limebaki kwenye salary slip nitofauti kabisa na kinacho onekana kwenye mfumo wao wamalipo!!

Nikiwa mwaka 2012 nilipo anza kulipa fedha za bodi, salio langu la deni lilikuwa m8 mwaka huu linasoma m2 na point kwenye salary slip!! Nilipata dhamira yakutaka kuliclear kabisa, nilipo watembelea kuchukua statement kwenye mfumo wao, jamani nimekuta linasoma m8 tena na point!!

Nilishangaa na mpaka sasa na shangaa!!

Nilihoji imekuwaje? Ili deni mbona limekuwa likilipwa toka mwaka 2012? Kwanini halija pungua nalinaonekana kuongezeka?? Na kwanini kwenye salary slip linaonekana kukaribia kuisha while huku limekua tena??


Majibu niliyo pewa yanasikitisha!!! nikaambiwa haya nimabadiliko ya thamani ya mkopo kwamba toka sheria mpya ile ipite nikwamba thamani ya mkopo niliokopa 2008- 2011 imekadiliwa sawa na anye kopa mwaka 2018!!


This isn't fair, na kibaya zaid taarifa hizi kuzipata ni mpaka kutembelea ofisi zao, hakuna mfumo ambao mtu anaweza log in akiwa popote pale akakuta taarifa zake akajua balance yake na kujipanga namnagani anaweza limaliza deni lake!!

Niseme wazi huu ni wizi, hata tukipiga total amount ya fedha zote kama ningelikuwa nalipa mwenyewe tution fee na mengimeyo zisingeweza fika hiz m19 nnazo ambiwa nimelipiwa!!


Nalaumu sana kuzaliwa familia yakipato hiki cha chini kilicho pelekea kujikuta napata mkopo ambao sasa umekuwa kama zimwi!!!


Je akija rais mwingine akasema mkopo huo tena uwekwe kwenye thamani sawa na mwaka wake aliopo madarakani kweli mkopo huu utaisha???


Lakini wakati naomba mkopo mwaka 2008 jamani nilipewa kijimkataba, amabacho kilikuwa na miongozo yake, je ni haki kunibadirishia term za mkataba bila kuzingatia hali ya uchumi wa sasa???

Ikumbukwe lengo ni deni lilipwe ila kwa staili hii, nasema wazi haya madeni yatakua ya life charge hayatakwisha!!!

Niwaombe pia nyie watu wabodi, tengenezeni mfumo watu waingie waone wanadaiwa shingapi kuliko hiki kinacho onekana kwenye masalary slip yetu!!! Mtu anaona kabakiza milion 1 kumbe ana 9 hazionekani!!!

Mungu ibariki tanzania!!!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kweli hata vivyo vyama vya wafanyakazi mnazolipia ada wameshindwa kutafuta kampuni zenye uwezo waishtaki bodi kuhusu ile sheria ya 15% kuwakata hata walionyuma ya sheria??

Kama bongo hakuna wanasheria wazuri si muchukue hata uingereza??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kweli hata vivyo vyama vya wafanyakazi mnazolipia ada wameshindwa kutafuta kampuni zenye uwezo waishtaki bodi kuhusu ile sheria ya 15% kuwakata hata walionyuma ya sheria??

Kama bongo hakuna wanasheria wazuri si muchukue hata uingereza??

Sent using Jamii Forums mobile app
Waswahili wanasema ukitaka kuujua utamu wa ngoma ingia nawe uicheze.

ukweli nikwamba wazo lako liko sawa kabisa na nadhani wapo waliokwisha lijaribu ila....... nchi yetu ilivyo kwa hivi sasa tunasema tu "ee mwenyezi mungu atusaidie"

Kumshtaki mwajiri ambaye ni (..........) sio kazi ndogo, utaanza kuulizwa na uraia, na mengine ya fuate!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom