Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

A blessing by disguise, tukusanye kodi zetu wenyewe ili nasi siku moja tuwe donner country.

Mkuu usidanganyike hao ndio watawala wa ulimwengu, Libya ya Gaddafi ilikuwa Donner County sasa hivi uko wapi? The world is not fair.
 
Habari ilopo ni kwamba Tanzania wamenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya suala la Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na cyber crime legislation.

========================
Tungeshukuru Tukiupata Lakini Hawawezi Leta UBEBERU Wao Bora UMASKINI WENYE HESHIMA KULIKO UTAJIRI WA KIMBWA MBWA
 
Habari ilopo ni kwamba Tanzania wamenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya suala la Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na cyber crime legislation.

========================

Naipongeza sana Marekani na sio kwa misaada hii tu yoote ambayo imekuwa addressed kwa Tz na mataifa mengine yashawishiwe wa stop misaada Tz. Naelewa tunaoumia ni wananchi lakini hakuna namna tumechoka kutawaliwa ni mkoloni mweusi.

Viongoz Tz wanajifanya wasanii sana, wanajifanya wamepachika pamba za maskio, juzi nimesoma Magufuli amemteua Afisa wa mambo ya ndani akasaidie kusolv tatizo la Burundi wakati Tanzania inanuka kwa migogoro tokea JK ameanza kuingia madarakani.

Hili la Zanzibar wanalikwepa kwa sababu kuna maslahi yao ya ndani na zaidi Tanganyika wanaitaka Zanzibar waimeze kabisa kabisa kuwe hakuna nchi inaitwa Zanzibar.
 
Mi naona hawa huwa wana sababu zao za kutotoa msaada. Siwezi amini eti hiyo ndo sababu. Kwani wao sera zao za mambo ya nje zina hata chembe ya demokrasia?

Yani wewe ombaomba unampangia masharti anayekupa pesa?
 
MCC is (an independent body) a sort of NGO which had developed and formulated set of conditions which the would their partners should meet them. They do fund raising for the purpose of helping developing countries but under their conditions. The scoreboards boards are set of conditions which one country has to meet them before being admitted and became a beneficiarer of the the MCC funds. Yes we joined the Compact but think we overlooked the strings of conditions. One of the clauses stipulate that the MCC has discretion to admit or suspend the member according to their own evaluation. This makes the relationship between the MCC and her members to be of Master and a slave rather than a win win situation. Let us wait and time will tell. But it is high time we reduce dependency to bodied like MCC and do away with their scoreboards.
 
Hapo sehemu ya 'governance'' ni pamoja na haki za mashoga. Nashangaa Mbowe ana shabikia hili.
 
Namuomba mungu Walete tena vikwazo vya uchumi, kwa sababu viongozi walioko madarakani wako kwa maslahi yao, na wapigeni burn viongozi wa serikali wasije ulaya.na Marekani na pesa zao walizo iba Tanzania na kuweka uswiz zichukueni wapeni wakimbizi huko Syria
 
Mi naona hawa huwa wana sababu zao za kutotoa msaada. Siwezi amini eti hiyo ndo sababu. Kwani wao sera zao za mambo ya nje zina hata chembe ya demokrasia?

Si ajabu wametukomoa kutokana na ukaribu wetu na Wachina kwenye Projects zinazo gharimu hela ndefu e.g Ujenzi wa mabarabara, Bandari, Reli, Umeme na gesi nk.Hawapendi kabisa wachina wajikite sana Africa.
 
Si ajabu wametukomoa kutokana na ukaribu wetu na Wachina kwenye Projects zinazo gharimu hela ndefu e.g Ujenzi wa mabarabara, Bandari, Reli, Umeme na gesi nk.Hawapendi kabisa wachina wajikite sana Africa.

Mbona mnataka kuukwepa ukweli? Kwani jee sio kweli kuwa Zanzibar demokrasia imebakwa? Jee sio kweli kuwa sheria ya Cybercrime ina kiuka misingi ya uhuru wa kujieleza na kutoa habari?
Hii ni sawa na kuugua kipindupindu kwa kula uchafu lakini ukionyeshwa tiba unataka kusingizia jirani mwenye macho mekundu.
 
ule mradi wa umeme vijijini lazima usimame
Mbona siku za mwishoni mwishoni wa utawala wa JK nilimsikia akisema kwamba Wakubwa wamehafiki ku-release fedha zilizo baki kwa mradi wa umeme vijijini, sasa kama wametuwekea spana kwenye mradi wenye umuhimu wa pekee Nchini naona hapo watakuwa wamekosea sana - kwani watu wa vijijini wanahusikana vipi na mambo ya siasa huko Zanzibar - huu ni upuuzi ulio pitiliza mipaka na kama UKAWA ndio walihusika kutuchomea utambi basi watakuwa na akili za kichawi na ukosefu wa hekima.

Binafsi naona Serikali iendeleze Mradi huo kwa kuchukua mkopo kutoka China, wanaweza kukubaliana mkopo wao urudishwe pole pole kwa riba ndogo - hata ikituchukua nusu karne kurudisha - sawa tu.
 
Hii ndiyo statement ya The Millennium Challenge Corporation (MCC) Board of Directors!

For Immediate Release
December 17, 2015

Renee Kelly
202-521-3880

The Millennium Challenge Corporation (MCC) Board of Directors held its quarterly meeting on Dec. 16, 2015. The Board approved three countries as eligible for compacts and two countries as eligible for threshold programs. Three of the five countries are new partners for MCC and all have worked hard to improve their performance on MCC?s scorecard, which measures countries? commitment to ruling justly, economic freedom, and investing in their people.

The Board selected Cote d?Ivoire, Kosovo and Senegal as newly eligible for compacts. Cote d?Ivoire, which was selected in December 2014 for a threshold program, will now transition into the compact program after showing continued improvement on its scorecard and achieving greater political stability. Kosovo, which passed MCC?s scorecard for the first time after making progress on democratic rights, is a new partner for MCC. Senegal successfully completed its first MCC compact in September and demonstrated improved scorecard performance over the life of the partnership.

In both Senegal and Cote d?Ivoire, the Board recommended that MCC explore potential investments that address regional obstacles to economic growth, in addition to domestic investments, while recognizing the need for statutory authority to optimize regional impact.

The Board also selected Togo and Sri Lanka to develop MCC threshold programs. Togo has shown a clear upward trajectory on overall scorecard performance over the past few years. Sri Lanka has embarked on a remarkable effort over the past year to reinvigorate its democratic institutions, improve governance, and restore protection of human rights.

Nepal, Niger and the Philippines were reselected by the Board to continue developing their compacts. The Board reselects all countries in compact development as part of the annual selection process. The Board deferred a vote on the reselection of Tanzania and Lesotho for compact eligibility until relevant governance concerns in both countries have been addressed.

Finally, the Board reaffirmed its commitment to developing a compact with Mongolia and its support for a strategic partnership with India to advance economic growth and poverty reduction in South Asia.

hata china inategemea misada jamani tusiwe sana mashabiki twende kwende kwenye uhalisia
 
TULIONYA MAPEMA, HILI NI SUALA LA TAIFA SI ZNZ
MIRADI ILITAFUTWA KWA GHARAMA KUBWA, KUKWAMA NI HASARA KWETU
Kama mtakumbuka, mapema sana katika jamvi la duru tulionya kuhusu mgogoro wa ZNZ na athari zake kitaifa
Tulisema, kwa muundo wa muungano, Rais wa JMT ndiye mwenye dhamana ya ulinzi na usalama na ni taswira ya nchi
Bodi ya MCC imesitisha msaada kwa Tanzania. Ikumbukwe, awamu ya 4 ilitumia muda mwingi kutafuta msaada huo
Aidha,serikali ya CCM imesifia safari za nje kwa kuonyesha MCC kama sehemu ya mafanikio ya ziara hizo
Inapotokea Taifa likakosa misaada likiwa limekeza muda na rasilimali, ni upotevu wa nguvu na rasilimali bila sababu
Awamu ya 5 nayo ilisema mgogoro utapatiwa ufumbuzi, kitu kinachoonekana hakikuwa na uhalisia
Mgogoro wa ZNZ ni wa sehemu ndogo sana ya Taifa. Madhara yake yanawagusa watu wasiohusika, inasikitisha
Hatuoni sababu za Watanganyika kubeba mzigo wa matatizo yanayosababishwa na mgogoro wa ZNZ
Hili ni sawa na kutoa 'kafara' ya watu takribani milioni 44 kwasababu tu ya wapiga kura laki 3
Lakini pia mgogoro huu hautokani na wapiga kura wa ZNZ.

Kazi yao ilikamilika, na wengi wakiwemo wa CCM walikubali matokeo.
Tatizo linatokana na wahafidhina wasiozidi 20 wa CCM waliogomea matokeo hayo kwasababu tu za kihistoria
Hivyo Taifa limewekwa rehani na kikundi cha watu ambao wanaungwa mkono na CCM. Hili linasikitisha sana
Swali la kujiuliza, kikundi hiki cha wahafidhina kina umuhimu gani katika Taifa hili kiasi cha kuliweka Taifa njia panda
Hoja ya kwamba, hatutaki misaada haina mashiko.

Kama tulijua hivyo, kwanini tuliwekeza sana katika MCC siku za nyuma?
Kuna umuhimu wa kurudi katika katiba, tuandike utaratibu utakaolinusuru Taifa na majanga kama haya
Wakati Tanganyika ikibeba mzigo mzito wa kuhudumia muungano na sehemu ya SMZ , sasa inajikuta inalipa gharama zaidi kutokana na mgogoro wa ZNZ ambao kiuhalisia hauna masilahi na mwananchi wa Tanganyika

Kilichotokea ni kuwatwisha Watanganyika mzigo zaidi licha ya ukweli kuwa wamebeba muungano mzito tayari
Watanganyika wanabebeshwa mzigo huu na CCM iliyoshindwa kukabaliana na wahafidhinaa pengine hawazidi 20
CCM inaweza kuwekwa rehani na wahafidhina kama chama, lakini ni makosa makubwa wahafidhina kuvuka mipaka na kuliweka Taifa rehani.
Haya ni matokeo ya kutumia maguvu na wingi wa CCM kuliko maarifa katika masuala yanayowagusa wananchi.
Tutaendelea hivi hadi lini?
 
Naamini ya Zanzibar yataisha lakini kama nchi tujitahidi kujitegemea ili kufikia malengo kwa muda tunaotaka.

Masharti ya misaada huwa sio mazuri na fedha huja kwa mafungu i.e tunaendelea lakini kwa speed wanayotaka wao.
Kwa kifupi tutatue matatizo wenyewe tujenge utaifa ili kuepuka kuwa controlled kimaendeleo.
 
Asie kubali kushindwa si mshindani, weka pembeni mambo ya msaada - yanayotokea Zanzibar ni dharau kwa watanzania wote. Inaonesha yangetokea Tanganyika pia kama CCM wangeshndwa
 
Back
Top Bottom