BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Date::7/16/2008
Bodi Benki Kuu Tanzania yabariki ukaguzi maghorofa pacha Dar
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi
KATIKA hatua ya kuondoa utata kuhusu gharama halisi za ujenzi wa majengo pacha (Twin Tower), Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu Tanzania (BoT), imebariki ukaguzi wa kitalaam wa gharama za ujenzi huo.
Uamuzi huo ulifikiwa karibuni, wakati kukiwa na wingu kuhusu gharama halisi za ujenzi wa majengo hayo yenye ghorofa 18, huku ikidaiwa kuwa kuna harufu ya ufisadi.
Taarifa kutoka ndani ya BoT, ambazo zilithibitishwa na Gavana wa benki hiyo, Profesa Benno Ndulu, jana zilisema ukaguzi huo umewahi kufanywa pia katika nchi mbalimbali zenye majengo kama hayo barani Afrika.
Akizungumzia mchakato huo, Profesa Ndulu alisema kuwa uamuzi wa bodi pia unalenga kujiridhisha na gharama hizo na kuona kiasi ambacho kinaweza kuokolewa katika ujenzi huo. Ujenzi huo bado unaendelea.
"Ndiyo, Bodi ilikaa na kuamua ufanyike ukaguzi wa kitalaam kuhusu gharama halisi za ujenzi huo, lengo ni kufanya tathmini halisi na kujiridhisha," alisema Profesa Ndulu.
Alipoulizwa kuhusu matokeo ya uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), alijibu: "Wao walifanya kwa misingi yao na taarifa wanazo wao, ila na sisi Bodi imeamua kufanya uhakiki."
Profesa Ndulu alifafanua kuwa, hatua iliyopo sasa ni kutangaza zabuni kwa ajili ya kupata kampuni itakayofanya ukaguzi huo.
Alisema kinachofanyika sasa ni misingi ya utawala bora kwa kufuata taratibu za manunuzi katika kupata kampuni hiyo.
"Haiwezakani tu kuteua kampuni bila kufuata taratibu za manunuzi. Sasa hivi tupo katika utekelezaji wa mchakato wa taratibu za manunuzi ambazo ni kutangaza zabuni, tuko katika hatua nzuri," alisema Profesa Ndulu.
Hata hivyo, Gavana huyo alisema kuwa hatua mbalimbali za ujenzi huo zimeonyeshwa katika ripoti za ukaguzi wa hesabu za hadi Juni 2007 na kwamba inasubiriwa ripoti ya Juni 2008.
Alifafanua kwamba, kila hatua itaonyeshwa, lakini gharama za jumla zitajulikana baada ya kupatikana kampuni husika ya kufanya ukaguzi.
Gavana huyo alifafanua kuwa hakuna kitu kitachofichwa kwani lengo ni kumaliza utata wa gharama za ujenzi huo, ambao hata hivyo bado uchunguzi wake uko katika hatua za mwisho.
Profesa Ndulu aliongeza kwamba, hatua nyingine ambayo inatarajiwa kufanyika hivi karibuni ni uzinduzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano.
Ujenzi wa majengo pacha ni moja ya maeneo yanayohusishwa na tuhuma za ufisadi, ambazo zimeikumba na kuitikisa BoT katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000.
Gharama hizo ambazo zinaelezwa kufikia Sh 600 bilioni ni kubwa, ikilinganishwa na gharama za ujenzi wa majengo kama hayo katika nchi za Ulaya na Marekani.