Bodaboda zisiwe sababu ya utoro shuleni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
0001mwendesha.jpg

Fredy Azzah
HIVI karibuni nilifanya ziara katika mikoa ya Pwani na Tanga na kutembelea shule kadhaa za sekondari na msingi.
Karibu katika kila shule niliyokwenda, suala la utoro kwa wanafunzi lilikuwa ni wimbo usiokwisha kwenye midomo ya walimu na viongozi wengine wa Serikali za kata na vijiji.
Pamoja na sababu nyingine zilizokuwa zinatajwa kuchochea utoro huo, kubwa ni watoto wengi kuacha shule na kujiingiza katika biashara ya kuendesha pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda.


Kwa mujibu wa walimu na hata wananchi niliozungumza nao, wanasema wanafunzi wengi siyo kuwa wamepewa pikipiki hizo na wamiliki, ila wanakwenda wenyewe kuchukua kile wanachokiita kwa jina la deiwaka kwa waendashaji waliopo vijiweni.


Walimu wengi wanasema kutokana na pikipiki hizo, kwa sasa wanafunzi wengi wamekuwa watoro wa kudumu na wengine ni watoro wa siku mojamoja.


Wanasema wakiwaambia wanafunzi waende shuleni siku za mwisho wa wiki ili wajisomee, ndiyo kabisa wanakuwa hawaoni hata mtoto mmoja.


Kwa kweli hali hii inasikitisha, inaonyesha ni kwa jinsi gani watoto hawa pamoja na wazazi wao hawaoni umuhimu wa elimu.,


Nimewajumuisha wazazi wao kwa sababu, siku watoto wasipokwenda shule wanawaona na hao wazazi hawasemi chochote.


Katika hili hata siku moja wazazi hawawezi kukwepa mzigo wa lawama, na siyo wazazi wa kuwazaa tu ila hata hao wengine ambao wanajua kuwa hawa ni wanafunzi na hawachukui hatua.


Ni vema jamii ikakumbuka ni muhimu kumhamasisha mtoto asome hata kama siyo wa kwako, kwani kuna siku atakuja kukusaidia.

Siyo lazima akupe fedha, ila anaweza kusoma na siku moja akaja kuwa daktari bingwa ama mtu yeyote ambaye atalisaidia Taifa na wewe mwenyewe.


Nadhani hili ndilo jambo ambalo wazazi walio wengi wanalisahau ama kulipuuzia kwa makusudi kabisa.
Ni veema hizi pikipiki zikatumiwa kwa manufaa yetu na siyo kutuletea hasara kwa watoto wetu kuacha kwenda shule.


Hili litafanikiwa endapo kila mzazi ataona kuwa watoto wote ni wake, na kama kuna mtu anampa mwanafunzi pikipiki afanyie biashara, nadhani ni vema akachukuliwa hatua. Hilo pia litawezekana tu pale taarifa za huyu mtu zitakapotolewa kwa vyombo husika.
Bodaboda zisiwe sababu ya utoro shuleni
 
Ni kweli wanafunzi wa kiume wamekuwa watoro sana. Wanasfema wanatafuta hela ya ada, nauli ya kila siku na ya chakula. Na ya kuwa hawapati msaada wa moja kwa moja toka nyumbani.
 
Back
Top Bottom