Labda nikupe ushauri kwa muono wangu.Maana hapa najua kesho haifiki post itafutwa.Maan unabahati kwamba Boss kubwa (Max)leo alikuwa kikaangoni EAT Tv.
Ni wazo zuri sana kuwa na kikundi na umoja huo.
Ningeshauri jichangisheni ili mtengeneze vipeperushi,kisha mvisambaze kwa kila abiria mnaemchukua.Wengne watavitupa na wengine watahifadhi kwa ku pick number za sim.
Sasa watakaovitupa wasiwakatishe tamaa,nyie pambaneni tu,kwani hata vipeperushi vya Bank watu wanavitupa vile vile ila wengine wanavitumia kwa kumbukumbku.
Hakikisheni vinakuwa vidogo ili visimkeri abiria kuchukua,na tafute mtu mzuri wa kuwaandalia texts za kuandika.Maana kama utakuwa wewe nauandishi wako huo inaweza ikawa kituko.Maana Unabahatisha.
Kuna sehem umendika kwamba Dereva anaendesha kwa Speed anayoitaka abiria,duhh sasa hapo kazi kweli kweli,wengine wanataka moto mkali,sasa hapo inakuaje kwamba Dereva Hana msimamo.
Ni Lazima Dereva wawe na Speed maalum kisheria kulingana na eneo na ukubwa wa Barabara na mazingira ya njia.
Pili,number za sim zote ni za madereva,hili ni tatizo kubwa sana.Na itasababisha sana ajali na mtagongwa kama kuku.Maana utaona sim ikiita unalazimsiha kusimama kwa kujipa matumaini kwamba kuna dili la abiria.Na mbaya ziaid unaweza kukuta hauisikii ikiita,na hapo abiria ataona ni wapuuzi na kuchukua ustaarabu mwingine
Nashauri kwamba tafuteni sehem au hata kibanda cha mbao,changeni mkitengeneze na mkiweka sehem,hata kama ni meza na kiti tu sio mbaya.
Hapo Muajirini mdada mmoja ndio awe Customer care au tuseme Service Center.Yaani yeye tu ndio awe na access ya kupokea sim za abiria.Maana atakuwa anajua muda huu Dereva fulani kaelekea sehem fulani.
Maana unaweza kukuta kwamba abiria anapiga sim yupo mbali na labda kuna dereva ameelekea njia ya huko au karibu na huko.hapo mnaweza kufanya kwamba yule Dereva alie karibu ndio akamchukue ili ku save mafuta na kupunguza gharama kwa mteja,ni bora yule wa karibu aunganishe.Hapa mtakuwa mmempunguzia mteja gharama kubwa tofauti na kwamba mngetuma dereva mwingine kutoka kituoni.
La sivyo mkapoteza wateja muhim,mtu ataona kwamba akiwaiat akiwa mbali mnacharge bei kubwa na kufanya adandie bodaboda za mitaani wakati wa kurudi.
Angalizo:Hapo najua mtarogana nyie kwa nyie mpaka basi,mie simo