Bodaboda wana papara sana !

Goodrich

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
2,091
1,177
Wandugu tuwe makini sana na hawa jamaa wa bodaboda.

Kama ni lazima utumie bodaboda basi tafuta mtu wako mmoja makini, aliyetulia, mwenye kujua sheria za matumizi ya barabara na mwenye akili timamu.

Ajali za bodaboda ni nyingi kila siku.

Ukweli ni kuwa ajali hizi kwa kiwango kikubwa husababishwa na uzembe wa bodaboda wenyewe.

Hawa jamaa wana papara sana.

Wakiwa hawajui sheria za matumizi ya barabara, wanaamini katika kuovateki muda wote, kutosimama taa nyekundu, kuvuka barabara bila kuangalia, na hata kuliovateki gari upande wa kushoto, ...kifupi wana papara sana.

Tuwe makini, tujiepushe na ajali!
 
Hawana papara.......

Labda fyuzi zipo loose...

Haiwezekani mwenye akili timamu akapita taa nyekundu.......
 
Ni kweli usemayo kabisa, nilienda mwanza, nikatokea maeneo ya kirumba kuitafuta igogo, yani m-bodaboda hakuwa makini kabisa na vile nina utaalamu na pikipiki kwani nilishawahi kuwa nayo kwa muda miaka 10, nilimwambia dereva, kaka naomba niendeshe wewe kuwa kama abiria manake utafupisha maisha yangu naona muda si mrefu, nikaendesha mpaka nilipofika nikampa chake, nikamuuliza ndugu unajua hasa kuendesha manake naona hata gia zako kuingiza mashaka na boda boda mpya hii, akasema mie nilikuwa mvuvi, nimenunua tu hii, kwa kweli sijawa mzoefu kuendesha hizi boda boda,
 
Back
Top Bottom