Tetesi: bodaboda mjini zilindwe

BMWsimba

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
347
506
Ni wakati sasa wa serikali kutunga sheria rafiki kwa bodaboda wanaofanya kazi maeneo ya mjini kwa kuwatambua na kuwapa utambulisho maalumu ili kuondoa hadha ya kusumbuliwa na askari polisi na askari wa jiji, kwani kwa sasa bodaboda anaweza akakamatwa akalipishwa fani ya zaidi ya laki na zaidi kwa makosa mengine hata hajafanya

Pia kuna askari wa jiji hawajakuwepo kipindi chote cha kampeni ila inasemekana kwa sasa wanafanya mpango warudi, kwakweli wananchi wengi wa dar es salama wamefurahia uwepo wa zuio la ukamataji na bodaboda imekuwa suluhu ya kupunguza foleni kwani kwa sasa unaweza pata bodaboda wa bei rahisi kwenda na kutoka mjini. itoshe kusema bodaboda ni msaada mkubwa sana kwa wafanyakazi na wafanyabiashara mjini.

Ikumbuke Kuwa bodaboda ni jamii kubwa ya vijana waliokosa ajira na kuamua kujiajiri.
 
Back
Top Bottom