Bodaboda mbona mnatuwahisha hivi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bodaboda mbona mnatuwahisha hivi!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Baba Mkwe, Oct 8, 2012.

 1. B

  Baba Mkwe Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3]Ajali Yaua Wawili Papohapo[/h]

  [​IMG]
  Dereva wa Bodaboda na abiria wake, ambao hawakuweza kufahamika majina yao kwa haraka, wakiwa wamelazwa pembeni mwa barabara ya Bagamoyo eneo la Makongo, baada ya kugongwa na gari aina ya Starlet yenye namba za usajiri T 838 BKB, wakati wakiwa katika Pikipiki yao yenye namba za usajiri T 491 BFY, na kufariki dunia papo hapo. Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi, Pichani ni raia akijaribu kutambua mwili wa marehemu katika ajali hiyo. (Picha Sufian Mafoto Blog)
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,141
  Trophy Points: 280
  Mvua kubwa sana inanyesha hapa Jengo la Hali ya Hewa kama walivyotabir. Vipi huko kwenu jamani! Mmeiona huko kwingine jamani? Ila boda boda ni nouma
   
 3. AMEND

  AMEND Member

  #3
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni masikitiko makubwa kuendelea kupoteza maisha ya Watanzania kila siku katika ajali ambazo zinaweza kuzuilika. Usafiri wa bodaboda hasa katika jiji letu la Dar es Salaam bado ni mgeni na kwa kweli madereva wa vyombo hivi wanatia sana mashaka. Tuwe makini hasa kuwakemea pale wanapokiuka sheria, maisha ni yako mwenyewe usiache dereva mzembe ayahatalishe. Hili si sahihi, simamia haki yako ya msingi ya kuishi. Ajali zinazuilika na wala tusingoje jeshi la polisi na serikali kutoa suruhisho.
   
 4. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,296
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Bodaboda wakati mwingi wanalaumiwa bure, kwanza wenye magari hawaheshimu kabisa watu wa bodaboda hili nimeliona sana, ebu angalia hapo huyo mwenye starlet anaonekana hayupo kabisa kwenye laini yake!

  Bodaboda ziendelee kwani zinasaidia kuwahi sehemu kwa kuepuka foleni na vilevile zinatusaidia wale tunaokaa mbali na barabarni ila waelimishwa sheria za usalama wa barabarani, na wenye magari wapewe adhabu kali sana wakisababisha ajali za bodaboda!
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Umehitimisha vipi kuwa hayuko katika line yake? Vipi kama gari iligeuka direction baada ya impact? Vipi kama gari ilihama line baada ya impact?
   
 6. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,296
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  oka wewe ni trafiki angalia picha then pima

   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  bodaboda ni janga.....
  Hapa uswazi vijana wanafundishwa asubuhi jioni wanakabidhiwa pikipiki......
  Mwenda wanaoendesha akipita mwenyewe utashika kichwa spidi wanazoendesha, wengine wanapatwa mzuka wanapoendesha hadi wanasimamia ..... Kuna umuhimu wa kuweka sheria kali, waende shule wajifunze sheria za barabarani pia.......

  Nilishuhudia dereva wa pikipiki akiingiza chini ya uvungu wa prado, mwenyewe akaruka na kumuachia msala abiria....isingekua dereva wa prado kuwahi kuruudi nyuma tungeongea mengine.........

  Siku nyingine kwa msuguri, bodaboda mwenyewe aliingia chini ya uvungu wa hilux........

  Wanapaswa wafundishwe sheria za barabarani na kuonywa kuhusu mwendo kasi..... Maana wengine spidi zinazidi wanashindwa kuzicontrol......

  Na kwa madereva wa magari muwe makini humo barabarani kwa usalama wenu na watumiaji wengine wa barabara....
   
 8. Kig

  Kig JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 1,060
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160


  Nchi inahitaji jambo la ziada zaidi ya sheria za barabarani. Kuna madereva wanajua sheria za barabarani na wengine hawajui kabisa. Lakini ukiwaona wakiwa barabarani wote wapo sawa yaani hakuna ambaye anathamini sheria za barabarani.
   
Loading...