Bodaboda wilayani Muheza wanalalamikia kitendo cha kuambiwa wakate leseni za kubeba abiria hali inayo wafanya wengi wao wakitaka kurudisha pikipiki kwa wamiliki.Wachache wa bodaboda hao wamesema kwasiku unaweza usipate abiria hata mmoja na tunashinda juani halafu unadaiwa hesabu ya bosi halafu serikali inatukandamiza tuna omba msaada juu ya hili.
Nalifahamu kwa kiasi:
1. Sheri ya usafirishaji wa abiria ilifanyiwa marekebisho 2009 na bunge na kanuni zake kutungwa 2010.
2. Marekebisho hayo yalilenga kuruhusu pikipiki za magurudumu matatu (maarufu bajaji) na zile za magurudumu 2 maarufu bodaboda zitambulike kisheria kama vyombo vya kubeba abiria.
3. Sheria pamoja na kanuni hizo husimamiwa na SUMATRA, hata hivyo kwa bodaboda na bajaji mamlaka ya usimamizi na utoaji wa vibali (leseni za usafirishaji wa abiria) zimekasimishwa kwa Serikali za Mitaa (Halmashauri zote) baada ya kusain MoU kati ya SUMATRA na Halmashauri.
4. Tangu 2010, pikipiki zote nchini zinapaswa kutoa huduma hiyo zikiwa na leseni ambayo hutolewa kwa mwenye pikipiki baada ya; ukaguzi wa mkaguzi wa vyombo vya moto, kuwa na dereva aliyepata mafunzo na ana leseni, chombo hicho kina bima & co.........
5. Usimamizi wa sheria hii ulikuwa mdogo, kwa sasa unafatiliwa ipasavyo nchi nzima, na Halmashauri zinabanwa ipasavyo.
6. Ile namba iliyokuwa inaimbwa kipindi cha kampeni, kwa sasa imeekwa juu ya mlima Kilimanjaro, KILA MTU ANAISOMA KIVYAKE.