boda boda na bajaji marufuku kuingia katikati ya jiji

kipindupindu

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
1,053
170
kuanzia tarehe saba mwezi huu ni marufuku kwa pikipiki maarufu kama bodaboda na bajaji kuingia katikati ya jiji la dar es salaam.kauli hii imetolewa na sumatra.abiria watatakiwa kupanda bodaboda au bajaji kutokea pembezoni mwa mji na baadae kupanda mabasi yanayohudumia katikati ya jiji.
my take:naipongeza sumatra kwa uamuzi huu hasa ukizingatia kero inayoambatana na vyombo hivi vya usafiri ikiwa ni pamoja na uvunjaji wa sheria za nchi unaofanywa na madereva wake.ushauri wangu ni vizuri amri hii ikaenea katika miji yote nchini kwani kero ya bodaboda imekuwa ni kubwa mno.
 
hawa jamaa wa bodaboda wanajidai wababe sana sasa tuone kama wataandamana.
 
Ila kama huna gari ni pigo maana bajaji wanasaidia sana kama kama daladala zinasumbua. Kwa city centre sawa lakini maeneo kama mwenge waziache bajaji wazuie bodaboda.
 
mkuu hawa jamaa hawafuati sheria kabisa,ajali zinazosababishwa na bajaji ni nyingi sana.
 
Maweeeee,inabidi ninunue kabaiskeli
maana nitafkuzwa kazi loool,na kama hiyo pikipiki ni mali yangu
na ninaitumia mimi kwa matumizi yangu binafsi
watajuaje?
Mmmh sarakasi zinaendelea
 
lazima tuondokane na utaratibu wa kihindi(bombay)
 
kuanzia tarehe saba mwezi huu ni marufuku kwa pikipiki maarufu kama bodaboda na bajaji kuingia katikati ya jiji la dar es salaam.kauli hii imetolewa na sumatra.abiria watatakiwa kupanda bodaboda au bajaji kutokea pembezoni mwa mji na baadae kupanda mabasi yanayohudumia katikati ya jiji.
my take:naipongeza sumatra kwa uamuzi huu hasa ukizingatia kero inayoambatana na vyombo hivi vya usafiri ikiwa ni pamoja na uvunjaji wa sheria za nchi unaofanywa na madereva wake.ushauri wangu ni vizuri amri hii ikaenea katika miji yote nchini kwani kero ya bodaboda imekuwa ni kubwa mno.

Unasound kama mtu mwenye private car, Mtu ambaye hana private car hawezi kufurahia swala hili.
 
ila foleni inazingua kinyama,,, watu wa bajaaj walikuwa wanatusave kinyama... Basi waweke miundo mbinu bora ya barabara... Sasa ni bora bajaj kulilo ule mfumo wa njia/barabara 3... Wanajifikiria wao tu coz they have got range rovers, gx100s, na cruisers... Cie wenzangu na ss ndio pakununua bicycle
 
bora basikweli hazileti ajali kama ilivyo kwa bodaboda!
 
Mbeya zilipigwa marufuku siku nyingi, ndani ya jiji hazionekani kabisa, biashara yao ni nje ya jiji
 
Kweli boda boda zipigwe stop maana zinaharibu 'manzari' ya jiji. Hata hivyo hawa jamaa hawafuati kanuni za usalama. Jana nikiwa kwenye foleni na my private car ghafla boda boda ilipita na kunivunjia side mirror na hakusimama.
 
kumbe siku nyingi hawa jamaa wamekatazwa kuingia kati kati ya jiji!!? mi nilijua imeanza jana!!
 
Back
Top Bottom