Bobi Wine kupinga ushindi wa Museveni mahakamani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,078
2,000
Kiongozi wa upinzani Uganda Bobi Wine amewasisitiza wafuasi wake kutofanya fujo, huku akipanga kupinga mahakamani matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Rais Yoweri Museveni.

Kiongozi wa Upinzani Uganda Bobi Wine amesema atapinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi mwengine tena Rais Yoweri Museveni mahakamani, huku akiwataka wafuasi wake kujizuia kufanya fujo.

Bobi Wine ametoa tangazo hilo Jumapili kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kwenye ukurasa wa chama chake National Unity Platform (NUP), baada ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa kumtangaza Museveni mshindi wa uchaguzi wa Alhamisi kwa kupata asilimia 58.6 ya kura zote zilizopigwa.

Kulingana na tume ya uchaguzi, Wine amepata asilimia 34.8 ya kura.

"Nachukua uamuzi huu kwa uchungu kuwasihi kujizuia kufanya aina yoyote ya fujo huku tukiwa tunajiandaa kuwasilisha mahakamani malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa na kasoro za dhahiri kwa maslahi ya ushindi wa muda mrefu ujao na kwa Uganda," Wine ameandika Wine kwenye Twitter ya chama chake cha National Unity Platform (NUP).

Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya majadiliano ya uongozi wa juu wa chama chake cha National Unity Platform NUP, Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi.

Visa vya udanganyifu wakati wa uchaguzi
Wine na chama chake wamedai kumefanyika "udanganyifu mkubwa" wakati wa uchaguzi wa Januari 14, ambao uliangaliwa kama uchaguzi wa kwanza Uganda uliotishia uongozi wa muda mrefu wa Museveni.

Museveni, 76, ni mmoja wa viongozi waliotawala kwa muda mrefu barani Afrika. Amekuwako madarakani kwa miaka 35, na kuibadilisha katiba ya nchi imruhusu kuwania muhula mwengine wa miaka mitano ya urais.

Uchaguzi huo ulifanyika chini ya kiwingu cha ghasia zilizoanza tangu wakati wa kampeni, huku kila siku kukiripotiwa visa vya matukio ya fujo.

Nyumba ya Wine iliyoko mjini Kampala ilizingirwa na wanajeshi tangu Ijumaa jioni, hali iliyomuweka kiongozi huyo wa upinzani katika kifungo cha nyumbani.

Mtandao wa intaneti ulizimwa kote nchini humo kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza na hali hiyo kuendelea hadi Jumapili.

Jiji la Kampala liko kimya Jumapili kuliko ilivyozoeleka, huku wanajeshi wa kulinda usalama wakiwa wanapiga doria katika kila barabara.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,092
2,000
Kwenye nchi fulani ya Majuha hakuna ruhusa ya kupinga matokeo ya Urais mahakamani. Hii maana yake hakuna makosa yanayoweza kutendwa kipindi cha uchaguzi mpaka yakapelekea kupingwa kwa matokeo.

Kwa majuha na kwa madikteta wengine kitu kimoja in common ni kuwa mahakama ni za madikteta.

Hukumu husomwa kwa maagizo kutoka juu.

Kutegemea haki katika mahakama za aina hiyo ni heri ya kumtumai Dr. Mapesa kutenda haki.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 

MC44

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
2,109
2,000
Yule wetu alienda kuripoti UBELGIJINI SIJUI KWSHI ISHAFUNGULIWA .....🏃🏃🏃🏃🏃
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
30,025
2,000
Sidhani kama UG ina Independent judiciary!

JUDICIAL INDEPENDENCE INFRINGED WHEN UGANDA'S CHIEF JUSTICE HAS TO 'PLEAD' FOR FUNDS - CONSTITUTIONAL COURT​


MAR
18
2020
By Carmel Rickard
Uganda’s constitutional court has found that the independence of the country’s judiciary is in jeopardy because of the way the budget of this arm of government is handled. In one of its most significant decisions under the present constitution, the court said the system made the judiciary very much the junior branch in the three arms of government, and often reduced the Chief Justice ‘to pleading for funds from the executive’.

A unanimous court of five judges set time-tables for major changes to the present situation so as to protect judicial administrative independence. The court also had strong criticism for the other arms of government whose argument, presented in court, seemed to ‘trivialise the importance of the judiciary’.


 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom