Boban asajiliwa timu ya Gefle IF Sweeden | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Boban asajiliwa timu ya Gefle IF Sweeden

Discussion in 'Sports' started by Lucchese DeCavalcante, Nov 24, 2009.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Haruna Moshi 'boban' secures contract with swedish side Gefle FC

  [​IMG]
  Haruna Moshi 'Boban' in Sweden​

  A new acquisition to the next season is ready for Gefle IF. Haruna Moshi with the stage name "Boban" is ready for the Gästrike Club.

  The Tanzanin who was on trial training with the club last week impressed so much on the club management that they chose to tie the 22-year-old midfielder.  That we got stuck with "Boban" as he is a skillful player with great technique and potential, says coach Pelle Olsson Gävle.

  For some reason Olsson would not say exactly how for how much the club has signed contracts with "Boban". - No, we are focused on it over several years. It is enough, "he says.

  Pelle Olsson also believes that it was important for the club to secure top players as soon as possible on the central midfield, where the club has already lost Yannick Bapupa and Yussif Chibsah is on his way out.


  Now that we have lost Bapupa and risk losing Chibsah it feels good to have signed with "Boban" said Olsson.

  Kalmar FF were also interested in "Boban" but chose to discard him. Instead, he then signed for Gefle. He comes from Simba FC and has quickly made a name in the Tanzanian national team, for whom he played 16 international matches.

  Boban arrived last night in Dar es salaam and is expected to return to Sweden when Gefle FC begin training for next season on January 4, next year.  Gefle wako league kuu ya Sweden , hongera sana Boban
   
 2. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  BOBAN uwe na nidhamu ndio siri ya mafanikio ndumu haitakufikisha popote
   
 3. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,276
  Likes Received: 4,260
  Trophy Points: 280
  Hongera BOBAN sasa unatakiwa kuprove kwa Maximo kwamba wewe ni mkali
   
 4. l

  libaba PM Senior Member

  #4
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Boban mdogo wangu, punguza bangi, ukifanikiwa kucheza huko miaka mitano, umeuaga umaskini
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Sura yenyewe tu inaoneka anakula CHA ARUSHA/TARIME huyu
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, matarajio yetu kwake ni kuwa asituangushe kwa mambo ya kukosa nidhamu. Hata kama ni mchezaji mzuri kiasi gani, kama hana nidhamu hataweza kufika popote maana dunia hii inatabia ya kuwakimbia watu wenye kukosa adabu kwenye shughuli wanazofanya.
   
 7. M

  Mundu JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kwani ni kosa gani alilofanya Boban hadi mseme kuwa amekosa nidhamu? Au kwakuwa Maximo amesema hivyo? Tatizo la ukosefu wa nidhamu ni endelevu, kama ni hivyo mbona Phil kila kukicha amekuwa akim miss Boban katika kikosi chake toka alipoenda kufanya majaribio Sweden?

  Tusihukumu wachezaji, eti kwa kuwa Maximo amesema hivyo.
   
 8. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  huko ataacha tu maana hakuna cha arusha wala monduli wala temeke wala wapi,na akijitia jeuri kukitafuta mitaani siku si nyingi mtamuona bongo na story kibaao za kulaumu watu,huko mambo hayo aache hata kufikiria polisi huko wanafatilia mambo hayo kinoma hasa kwake yeye yatamuharibia tu,usikute washampima na wameona kama anakula jani asa akiendelea watajua tu na hiyo ndio itakua imeharibu future yake vibaya,achana na ndumu bwa mdogo
   
 9. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe umenena,ndumu kweli sio nzuri.
   
 10. M

  Magehema JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kila asemalo Maximo mnadhani kweli, iko siku atwaambia yeye ndio baba yenu na wote mtaamini.
   
 11. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  dah,poa sana mtu wetu,komaa kaka,miaka hata Wanaijeria wanadanganya na wanapeta..
   
 12. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyu dogo ana future nzuri sana kwenye soccer. Naamini kama atajituma zaidi siku si nyingi ataanza kuwaniwa na klabu kubwa za Ulaya. Makocha wanahitaji kurekebisha vitu vidogo sana ili kumwezesha kuwa star. All the best Boban!
   
 13. Mlango wa gunia

  Mlango wa gunia Senior Member

  #13
  Nov 29, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Dogo ana future nzuri tu,kwa umri wake na kiwango chake,azingatie masharti ya soka na aweke maanani kuwa sasa ndio wakati wa kujenga jina,hasira ndio lilikuwa tatizo kubwa natumaini atalifanyia kazi,namtakia kila la kheri.
   
 14. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hongera boban. Mfunyukuzi mi napenda nikuite Mfukunyuzi(Mfukuaji wa Nyuzi) Unaonaje?
   
 15. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Simba yamsajili Haruna Moshi Caf


  KIUNGO Haruna Moshi aliyefuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Gefle IF ya nchini Sweden ni miongoni mwa wachezaji 27 waliosajiliwa na Simba ya Dar es Salaam kwa ajili ya michuano ya kimataifa mwakani.

  Haruna, ilielezwa hivi karibuni kuwa amefuzu majaribio kwenye klabu hiyo na anatarajiwa kwenda tena Sweden mapema mwezi ujao kujiunga na timu hiyo, lakini klabu ya Simba imeorodhesha jina lake kwenye orodha yake iliyowasilishwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana kwa ajili ya kutumwa makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

  Akizungumza jana, Msemaji wa klabu ya Simba, Clifford Ndimbo, alisema ni wachezaji watatu hawapo kwenye orodha ya Simba kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambao ni Adam Kingwande, George Nyanda na Meshack Abel wanaocheza kwa mkopo klabu ya Africa Lyon.

  Katika kikosi hicho lipo jina la mshambuliaji Mkenya aliyesajiliwa akitokea Yanga, Mike Barasa pamoja na nyota mwingine Mkenya Jerry Santo ambao wote wamesajiliwa kwenye dirisha dogo Novemba mwaka huu.

  Orodha kamili ya wachezaji wa Simba kwa michuano hiyo ni Juma Kaseja, Ally Mustapha, Deogratius Munishi, Haruna Shamte, Haruna Moshi, Salum Kanoni, Kelvin Yondan, Salim Aziz, Danny Mrwanda, Nico Nyagawa, Antony Matangalu, Mussa Mgosi, Hilary Echesa na Ulimboka Mwakingwe.

  Wengine ni Uhuru Seleman, Mohamed Banka, Ramadhan Chombo, Joseph Owino, Jabir Aziz, Juma Jabu, Juma Nyoso, Emmanuel Okwi, Mohamed Kijuso, David Naftal na Amri Kiemba.

  Kuhusiana na hofu ya Simba kuchelewesha kutuma majina hayo TFF huku siku ya mwisho ya majina kutumwa Caf ikiwa ni leo, Ndimbo alisema, hawana hofu na hilo na jana walitarajiwa kuyawasilisha TFF.

  Mwisho wa Caf kupokea majina ya wachezaji kwa ajili ya michuano ya kimataifa bila faini ni leo, ambapo baada ya hapo klabu italazimika kutuma majina hayo pamoja na faini hali ambayo juzi ilimfanya Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela kuihimiza Simba kufanya hivyo.

  Akizungumza jana, Mwakalebela alisema ana matumaini kwamba Simba ingewapa mapema usajili wao, hivyo wao watautuma Caf kama taratibu zinavyotaka bila kuiathiri klabu hiyo.


  Source: Gazeti la Habari Leo
   
 16. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  vp tena?uchawi
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Uchawi kivipi mjomba?,hizi taarifa za Boba hazieleweki hata kidogo,mara kapata timu Ulaya,mara kasajiliwa na Simba!!,ina maana atachezea timu mbili kwa wakati mmoja???.Haya soma habari nyingine hii hapa chini


  SIMBA ya Dar es Salaam imewasilisha majina ya wachezaji 27 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwakani akiwemo kiungo wake mahiri Haruna Moshi Shaaban "Boban".

  Majina hayo yamewasilishwa jana kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), siku moja baada ya shirikisho hilo kudai juzi kuwa klabu hiyo imeshindwa kufanya hivyo.

  Afisa habari wa klabu hiyo, Cilfford Ndimbo alisema jana kuwa wamewasilisha majina hayo 27 TFF , isipokuwa watatu ambao wameuzwa kwa mkopo kwenye ya klabu ya African Lyon.

  "Tumewasilisha majina ya wachezaji wote, ispokuwa Meshack Abel, George Nyanda na Adam Kingwande, hao wapo Lyon kwa mkopo.

  "Ni mataumanini yetu kuwa majina hayo tumeyawasilisha kwa muda muafaka kwa sababu kesho (leo) ndiyo mwisho ya kufanya hivyo.

  "Kwa kuzingatia muda huo ni matumaini yetu kuwa TFF itayawasilisha CAFjijini Cairo, Misri bila ya matatizo," alisema Ndimbo.

  "Kutokana na usajili imara tulioufanya msimu huu, hatuihofii timu yoyote ambayo tutakutana nayo," alisema.

  Kikosi hicho cha wachezaji 27 ambao walikuwa wameweka kambi visiwani Zanzibari kwa ajili ya michuano ya Tusker kiliwasili jijini Dar es Salaam jana kwa michuano hiyo.

  Hata hivyo taarifa za kupelekwa kwa jina la Boban katika CUF kwa ajili ya michuano ya kimataifa kumeibua maswali mengi kutoka kwa mashabiki kuwa je ni vp kiungo huyo asajiliwe na simba katika michuano ya kimataifa hali ikiwa ameripotiwa kushinda majaribio katika timu ya daraja la kwanza nchini Sweden?

  Itawezekanaje mchezaji mmoja akachezea timu mbili kwa msimu mmoja?ikizingatiwa kule Sweden atakwenda kusaini mkataba wa takriban msimu mmoja kuanzia mapema mwakani wakati ambapo pia simba itakuwa mashindanoni wanahoji wachambuzi wa masuala ya kispoti kupitia Bongo Ndiyo home!

  Wadadafuaji hao wa kispoti wamewataka viongozi wa simba,wakara wa mchezaji huyo na Haruna Moshi Mwenyewe kuwaeleza watanzania ukweli ni upi?alishindwa majaribio au alishinda? na kama alishinda iweje akimbilie kisamvu nyumbani kwao akaacha nyama ya kutosha kwa jirani asiye na mizengwe katika masuala ya misosi? au ale tu kisamvu kwa kuwa kimepikwa home?

  Wamesema wanalazimika kuhoji hivyo kwa kuwa hakuna uwiano wa ubora wa soka kati ya Tanzania km sio simba na sweden katika kikosi cha daraja la kwanza ambacho boban anatakiwa.

  Naomba kuwasilisha Je Haruna Moshi aliyekwishaichezea stars michezo 24 alishindwa majaribio Sweden?


  Source Dullonet
   
 18. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #18
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  ndio nashangaa mambo ya bongo yanaumiza kichwa
   
Loading...