Bob Marley na Peter Tosh nani legend wa muziki wa reggae

Bob Marley na Peter Tosh nani legend wa muziki wa reggae

Nyamgessi

Member
Joined
Mar 26, 2015
Posts
80
Reaction score
26
Wale wadau wa muziki wa Reggae tujuzane mengi kuhusu muziki huu, na nani legend wa muziki huu kat ya Bob na Tosh.
 
Wote ni legendary wa muziki huo labda tatizo ungeuliza nani alikuwa mkali kuliko mwingine.Tosh alikuwa anamchukulia bob kama kinabo flan coz hakuwa mtoto wa downtown kama yeye pili alikuwa mixture na uzungu so tosh akawa hamkubali kivile ndo kisa cha kutengana.
 
Bob, Tosh na Bunny hawakuanza na muziki wa reggae. Walianza na muziki wa SKA sikiliza ngoma zao kama vile PUT IT ON, SIMMER DOWN nk. kuhusu Tosh kumdis Bob sidhani kama ni kweli coz urafiki wao ni wa zaidi ya miaka 15.

Tosh na Bunny walijiondoa the wailers kutokana na kumlalamikia meneja wao Mr Blackwell kuwa anawanyonya. Kwa mtizamo mwingine Tosh alikua extremist kama Malcom X wakati Bob alikuwa diplomat kama Martin Luther Jr.
 
Mimi nadhani ni Tosh maana nyimbo karibu nyingi za mwanzo za wailers yy ndie alikuwa mtunzi.
 
Bob anaonekana mkali lakini Tosh ndo alimfundisha mziki, na wengi wanaamin ndo legend.
 
Bob anaonekana mkali lakini Tosh ndo alimfundisha mziki, na wengi wanaamini ndo legend

Tosh hakuwahi kumfundisha bob muziki kama unavyodai. wote wamefundishwa muziki na Joe Higgs. na ni Bob na Bunny ndio walionza kupata mafunzo kwa Higgs, baadae Tosh akajiunga na mafunzo, na Higgs akaamua kuwaunganisha wawe kundi moja wakijiita THE JUVENILES baadae wakajiita THE WAILING WAILERS na baadae wakajiita THE WAILERS. kitu pekee ambacho Tosh alikua na kipaji nacho na wala hakufundishwa na mtu ni gitaa. sasa hizo hadithi za kudai Bob amefundishwa muziki na Tosh sijui mnazitoa wapi.

hgs.jpg​
 
Ulivyoandika ni kama ni ma boy wako wa kitaa.
 
Mtunzi na mwimbaji wa BUSH DOCTOR ni mkali na ukali wake ni endelevu.

Hata Dr. Sanjay Gupta wa CNN anaishauri dunia iikubali tiba ya "herb"

Sikiliza wimbo "Buckingham Palace" ili ujiunge nae kuwafukuza ma-vampaya (vampire)
Uzuri wake rizzlla zimejaa madukani kinahitajika kiberiti tu.

PETER hakuwa mnafiki.
Ref: "peace treaty"
"i'm the toughest"

Majina kamili ni Winston Hubert Macntosh.
 
Wote wako njema ila Peter Tosh ni zaidi(according to me), nimesikiliza nyimbo zao karibia zote, Tosh alikuwa anaamini 'equal rights and justice' kama msingi wa maisha wakati Bob alikuwa anaamini 'peace and love' ndiyo msingi wa maisha, Tosh alikuwa very militant pale anapoona HAKI haitendeki alikuwa kiharakati zaidi na politically neutral wakati Bob alikuwa ana link na baadhi ya wanasiasa! Binafsi namkubali zaidi Tosh lakini wote ni wakali
 
Voice of mtwara nimekusoma about Joe higgs,ila bado bob alikuwa akipewa promo sn na wazungu kuliko tosh ......
 
Tosh ni legendary wa reggae bt hakuwa na promo za kutosha kama bob, lakini watu wengi ukiwauliza legendary wa reggae ni nani watakwambia bob sababu alipata promo kubwa kuliko Tosh.
 
Mtunzi na mwimbaji wa BUSH DOCTOR ni mkali na ukali wake ni endelevu.

Hata Dr. Sanjay Gupta wa CNN anaishauri dunia iikubali tiba ya "herb"

Sikiliza wimbo "Buckingham Palace" ili ujiunge nae kuwafukuza ma-vampaya (vampire)
Uzuri wake rizzlla zimejaa madukani kinahitajika kiberiti tu.

PETER hakuwa mnafiki.
Ref: "peace treaty"
"i'm the toughest"

Majina kamili ni Winston Hubert Macntosh.

"Any thing you can do I can do it better.... I'm the toughest x2...and I can do what you can't do, you never try to do what I do Cause I'm the toughest".....!, "......peace treaty you signed in Kingstone city......", Peter Tosh was really a stepping razor, kuna 'Sorry fi Maga dog', Reggae my litis, Rumours of war, Mark of the beast, Mystery babylon, equal rights and justice, Jah say No, Rastafari Is, Fight on etc pia utampata vema kwenye 'One foundation' ya pamoja na kina Bob
 
Back
Top Bottom