Inawezekana nisiwe right. No Woman, No Cry ni wimbo unawaomba wanawake wasilie. Wimbo huu unahusu mwanaume kukulia kwenye maisha ya ghetto na kuweza kumshawishi mwanamke ampende kwa vile mambo yatakuwa mazuri hapo baadae.
Wapo wengine wanaosema kuwa jina la wimbo lina maana kuwa kama huna mwanamke, basi huwezi kulia. Wengine wanadai mwanamke kwenye No Woman, No Cry ni malkia wa Uingereza alivyoitawala Jamaica. Kwamba, kama sio yeye basi Wajamaica wasingelia.
Wengine wanadai Bob aliimba huo wimbo kwa aili ya rafiki yake V. Ford ambaye alikuwa mtungaji wa nyimbo. Huyu rafiki yake Bob alikuwa maskini na alikuwa anaishi maisha ya ghetto. Wanasema wakati V. Ford akiwa amelazwa hosipitalini kwa ugonjwa wa cancer, mke wake (V. Ford) alikuwa pembeni mwa kitanda chake akilia na V. Bob alimwambia "no woman, no cry" which inspired Marley to write the song.