Bob Marley alikuwa anamaanisha nini??

kaeso

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
548
Reaction score
97
Kwenye huu wimbo wake huyu nguli wa Reggae alikuwa anamaanisha nini hasa katika title ya wimbo.
"NO WOMAN NO CRY"
 
Alimaanisha wanawake ndo wanatuletea machungu haya yote unayoyaona si unakumbuka story ya nyoka eve na adam????
 
Hiyo falsafa andishi, uki-punctuate NO WOMAN NO CRY inakuwa NO! WOMAN NO CRY. kwenye uwanja wa mapambano mwanamke ni sawa mtoto, mwanamme anawajibu kumfariji, kumbembeleza hata kumtia moyo ili asije kata tamaa katikati ya mapambano hasa pale the going inapokua tough, mwanamke usilie!!!! kwenye neno ,mwanamke, weka jina la mkeo au my wife wako to be.
 
Inawezekana nisiwe right. No Woman, No Cry ni wimbo unawaomba wanawake wasilie. Wimbo huu unahusu mwanaume kukulia kwenye maisha ya ghetto na kuweza kumshawishi mwanamke ampende kwa vile mambo yatakuwa mazuri hapo baadae.

Wapo wengine wanaosema kuwa jina la wimbo lina maana kuwa kama huna mwanamke, basi huwezi kulia. Wengine wanadai mwanamke kwenye "No Woman, No Cry" ni malkia wa Uingereza alivyoitawala Jamaica. Kwamba, kama sio yeye basi Wajamaica wasingelia.

​
Wengine wanadai Bob aliimba huo wimbo kwa aili ya rafiki yake V. Ford ambaye alikuwa mtungaji wa nyimbo. Huyu rafiki yake Bob alikuwa maskini na alikuwa anaishi maisha ya ghetto. Wanasema wakati V. Ford akiwa amelazwa hosipitalini kwa ugonjwa wa cancer, mke wake (V. Ford) alikuwa pembeni mwa kitanda chake akilia na V. Bob alimwambia "no woman, no cry" which inspired Marley to write the song.
 

uko karibu na sawa bro.
Ukitazama lyrics za ule wimbo, kuna sehemu anasema, "...hey ma' little sister, don't shed no tears."
utaona ni wimbo wa kuliwaza mtu, rafiki yake, aliyemtaja kwa jina la Geogie, akikumbuka maisha yao ya kitambo huko Trenchtown.
 
hivi wamarekani weusi(especially au hardcore rappers)wanaposema 'i won't go no where' huwa wanamaanisha i won't go anywhere..same applies to 'no woman no cry' yani ni sawa na woman,don't cry.
 
Mbona mnapata shida sana wakati jibu ni jepesi alimaanisha hakuna mwanamke hakuna kilio
 
Yule mwingereza (Bob) mvuta bangi hapo aliimba kifalsafa zaidi!!
Tafsiri utakvyo mziki ni mziki tu!
 
hivi wamarekani weusi(especially au hardcore rappers)wanaposema 'i won't go no where' huwa wanamaanisha i won't go anywhere..same applies to 'no woman no cry' yani ni sawa na woman,don't cry.

"No Woman, No Cry" is not a double negative in the sense of "I won't go nowhere". It is more like "Hapana Mwanamke, Hapana Usilie"

Bob wasn't particularly good at English, Rita helped him a lot. Actually the Jamaican culture derides "proper" English as illogical .This is not entirely untrue and turns English on its head with expressions such as "overstanding" (for understanding) etc.
 
Nadhani ni kwa kusoma/kusikiliza kipande cha wimbo wenyewe au wimbo wote ("context")ndio pengine unaweza kupata maana aliyokusudia mtunzi. Lugha ya kishairi ukisema uchukue mstari mmoja mmoja pekeyake kuna mistari mingine inaweza isiwe hata na maana kabisa!

 

what if we put it this way,..no,woman no cry meaning hapana,mwanamke hapana kulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…